Mabinti Wanaojiuza" Ni Wakuhurumiwa na Kusaidiwa", Sio Wote Wanapenda!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Wale wasichana wadogo wanaojishughulisha na biashara ya kujiuza miili yao nyakati za usiku katika maeneo mbali mbali, sio wote wanafanya biashara hiyo kwa kupenda, bali wengi wamejikuta wametumbukia kwenye biashara hiyo kutokana na hali tuu ya maisha na shida mbalimbali zinazowakabili hadi kujikuta wanalazimika kufanya biashara hiyo. Hawa si wa kulaumiwa bali ni wakuhurumiwa na ikibidi ni wa kusaidiwa kwa kuwezeshwa ili wabadilike na kufanya kazi halali.

Hebu someni hii taarifa toka Moshi.

6/02/2012 na mwandishi wetu Wadada Watanzania Zaidi ya 5,000 Wasaidiwa na DSW

Vijana na jamii kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini, wamefaidika moja kwa moja au kwa namna nyingine na mradi wa Elimu ya Afya ya Uzazi kwa kuwajengea uwezo wa kujitegemea vijana wa kike, walioko katika biashara ya kujiuza miili yao uliotekelezwa na Shirika la German Foundation for World Population (DSW) la Ujerumani kwa kushirikiana na 4H Tanzania na UMATI.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkazi wa DSW nchini Tanzania Bw. Peter Owaga, wakati wa semina ya siku moja ya kuhitimisha mradi huo, uliotekelezwa kwa miaka 4, iliyofanyika mjini Moshi hivi karibuni.

Bw. Owaga amesema mradi huo, uliofadhiliwa na fedha kutoka Jumuiya ya Ulaya (EU) umewajengea uwezo wa kiuchumi vijana wa kike zaidi ya 5,000 walio katika sekta isiyo rasmi katika wilaya tisa toka mikao ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga kwa kuwapatia elimu ya afya ya uzazi, elimu rika, elimu ya ujasiliamali na kuwapatia mitaji na vitendea kazi mbalimbali kwa ajili ya miradi midogo midogo ya kiuchumi hivyo kuwawezesha kujitegemea na kusaidia familia zao na kujenga uchumi wa taifa.

Kupita mradi huu shirika limeweza kuwakutanisha vijana na waajiri mbalimbali kujadili fursa na changamoto zinazo wakabiri vijana walio katika sekta isiyo rasmi ili kuboresha mazingira ya kazi kwa vijana hao. Pia mradi huu umeweza kufanya utetezi na ushawishi katika uboreshwaji wa sera na sheria mbalimbali zinazo husu ajira na kazi kwa vijana walio katika sekta isiyo rasmi.

Bw. Owaga ameishukuru Jumuiya ya Ulaya na ushirikiano mkubwa kutoka wizara ya Afya na ustawi wa jamii, wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana na wadau wengine kwa kuufadhili mradi huo, na kutoa wito kwa wadau mbalimbali zikiwezo asasi za kiraia, kusaidia juhudi za serikali katika kuwawezesha vijana kujiajiri na kujitegema kwani wao ni moja ya sehemu muhimu ya jamii inayokabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo hatari ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa na Ukimwi.

Meneja Mradi wa Elimu ya Afya ya Uzazi kwa Vijana wa kike, Bi. Christina Sudi, amesema wasichana wengi wamejikuta wakiharibikiwa kimaisha kwa kupata mimba za utotoni na hata kupata maambukizo ya ukimwi, kwa kukosa elimu ya afya ya uzazi.

Kwa kuwapatia elimu hiyo, DSW imewasaidia vijana wengi kujitambua hivyo kuepuka mimba zisozo tarajiwa, na pia imewapita elimu ya ujasiliamali na kuwapatia mitaji ambayo imewajengea uwezo wa kujitegemea na kuleta maendeleo yao, familia zao, jamii iliyowazunguka na taifa kwa ujumla.

Bi. Jane Lazaro kutoka wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, ni miongoni mwa waliofaidika na mradi huo wa DSW wa kuwawezesha vijana, amesema yeye ni miongoni mwa wasichana walio shindwa maisha kutokana na kupata ujauzito katika umri mdogo na kukata taamaa ya maisha.

Jane amesema ujio wa DSW ni ukombozi mkubwa kwake kwani mradi huo umempatia elimu ya afya ya uzazi, elimu ya jasiliamali, ikampatia mtaji na sasa anaendesha maisha yake kwa kujitegemea ikiwemo kumlea mwanae na kuwasaidia wazazi wake.

Dr. Anna Kimaro wa Kituo cha Afya Kaloleni Arusha mjini, amesema DSW ilivyojenga uwezo kwa kituo chake kwa kujenga jengo mahsusi la kutoa huduma rafiki ya afya uzazi kwa vijana, na wakati huo huo, kusaidia vikundi mbalimbali vya vijana kwa kuwapatia elimu ya ujasiliamali na kuwapatia mitaji.

DSW ni shirika la Ujerumani lilianza shughuli zake nchini Tanzania mwaka 1996 likijihusisha kuwajengea uwezo vijana, jamii maskini na zile zenye kipato cha wastani ili waweze kukabili changamoto zitokanazo na ongezeko la watu duniani. Shirika hili lina amini kwamba afya bora ya jamii ni msingi mkuu katika maendeleo endelevu, ndiyo maana hutumia zaidi mbinu shirikishi na zenye kuzingatia mahitaji halisi ya rika na kuwavutia vijana, hasa hasa ile ya Youth to Youth. Mbinu hii ambayo huratibiwa na vijana kwa kutoa burudani na elimu kwa pamoja, imewezesha vijana wengi kufikiwa kwa kupitia mijadala ya wazi, huduma za mafunzo ya muda mfupi, elimu ya ujasiliamari na mitaji midogo ya kuanzisha au kuendeleza biashara.(Mwisho)

My Take.
Kumbe wengi wa wale madada wanaofanya ile biashara ya usiku maeneo mbalimbali, wasilaumiwe bali wasaidiwe. Kwa vile biashara ile imeshamiri sana, ina maana soko lipo na wateja wapo ndio maana inaendelea. Natoa wito kwa wale wenzangu na mimi ambao nao huponea kwa wadada hao japo mara moja moja, basi angalau walipeni vizuri au hata kuwazidishia ili kuwasaidia katika shida zao zilizowapeleka kwenye biashara hiyo.

Wasalaam

Pasco.
 
Wanawake kujiuza au PROSTITUTION ni biashara ambayo imeanza hata kabla ya ustaarabu wa binadamu. Mwanzo ilikuwa yule mwanamume anae weza kuwalisha wanawake wengi (ALPHA MALE) ndiye anaepata wanawake. Baadae ustarabu ulipoanza yule mwenye pesa ndiye awezae kupata mwanamke amtakae.

Dini na Tamaduni zika anzisha utaratibu wa ndoa. Hii ndiyo iadhaniwa kuwa ndiyo ustarabu. Lakini binadamu kama mnyama ndiye anaesababisha katika nyakati hizi za maendeleo ya kitechnologia ndiye anaesababisha tena wanawake kurudia zile hisia za kinyama. Huwezi kupata mahitaji yeyote bila ya pesa. Na kama mwanamke hana njia nyingine ya kuchuma hiyo pesa, ndipo anapokimbilia kwenye njia anaeona ni nyepesi kwake ambayo ni kurudia ile biashara ya asili.

Lakini ukimpa uwezo huyu mwanamke, anaweza kujiendeleza na kuendeleza jamii kwa hali ya juu sana. Kumelimisha mwanamke iwe ni priority No. 1 kwa jamii yeyote inayotaka maendeleo. :A S embarassed:
 
Back
Top Bottom