Mabinti 12 wanaswa na ‘unga’ ndani ya siku 30

Mabinti 12 wanaswa na ‘unga’ ndani ya siku 30

dubu

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
3,502
Reaction score
3,485
unga.jpg

Dawa za kulevya

Dar es Salaam. Licha ya kampeni kubwa ya kupambana na kuzuia usafirishaji, uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya nchini, bado Watanzania wameendelea kufanya biashara hiyo na katika kipindi cha siku 30 mabinti 12 wamekamatwa wakisafirisha dawa hizo ndani na nje ya nchi.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Kamishna wa Kikosi cha Kupamba na Dawa za Kulevya nchini, Godfrey Nzowa zinaonyesha kuwa idadi kubwa ya Watanzania waliokamatwa katika kipindi hicho ni mabinti wenye umri mdogo.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mabinti wanane wamekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Hong Kong na wanne katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam.

Kamishna Nzowa alisema ingawa vyombo vya habari na wafungwa walioko Hong Kong wamejaribu kuwashauri Watanzania wasifanye biashara hiyo, bado wamekuwa na ‘shingo ngumu.'

Alisema Januari 23, wanawake wawili, Rehema Ndunguru (31) na Moyo Ramadhani (31) walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere wakisafirisha dawa hizo kwenda Hong Kong.

"Rehema alikuwa amemeza pipi 78 ambazo ni sawa na kilo 1.2 na Moyo alitoa pipi 86 sawa na kilo 1.5," alisema Kamanda Nzowa.

Alisema Februari 12, mwaka huu alikamatwa mwanamke mwingine Munira Mohamed (27) akiwa amemeza pipi zenye uzito sawa na kilo 1.

Februari 9, mwaka Halmati Tango (21) alikamatwa akiwa na pipi 76 zenye uzito sawa na kilo 1.3.

Nzowa alisema Halmat alikuwa akisafirisha dawa hizo kwenda Nigeria wakati Munira alikuwa akizipeleka Mombasa.

Hong Kong

Wakati huo huo, Padri John Wotherspon aliyekuwa nchini kwa ajili ya kampeni ya kuwazuia vijana wa Kitanzania kusafirisha dawa za kulevya amelieleza Mwananchi kuwa wanawake wanane wa Kitanzania pia wamekamatwa katika uwanja wa ndege wa Hong Kong katika kipindi hicho hicho.

Padri Wotherspon alisema baadhi ya wanawake hao wamekiri kusikia na kuona barua za wafungwa wa China zilizoonya kuhusu biashara hiyo lakini wakachukua uamuzi wa kuzibeba. Kati ya wanawake hao wanane, mmoja alikuwa amemeza kete 135 za dawa za kulevya aina ya heroin na mwingine alikuwa amemeza kete 86.

Kwangu mimi vita inazaa matunda, tunapowakamata ina maana tunazuia," Nzowa. kusambazwa kwa mzigo," alisema.

Chanzo: Mwananchi
 
Elimu ni muhimu sana kwa mabinti zetu,otherwise ukiwang'ang'ania elimu aina moja tu ambayo aina ajira mwisho wake ndio huo,nadra kukuta Jane,au Winifilda au Jaquiline au Rose etc kakamatwa na hiyo midawa,the same kwa wanaume.Look at the names you will understand what I mean
 
mkuu,upo sahihi kabisa. na hata huku mitaani,wahusika wakubwa ni hao hao akina baker,ramso.huu ni wakati wa kusisitizia umuhimu wa elim dunia kwa hawa wenzetu
 
Jamani kuna watu wana roho ngumu,yani una hatarisha maisha hivi hivi,sasa unamalizia maisha yako jela bila sababu ya msingi kisa wanataka maisha ya juu,mie apana mungu aninusuru na tamaa yakijinga,ntakula ugali na bamia lakini unga sibebi,ntauza chapati lakini unga apana.
 
Elimu ni muhimu sana kwa mabinti zetu,otherwise ukiwang'ang'ania elimu aina moja tu ambayo aina ajira mwisho wake ndio huo,nadra kukuta Jane,au Winifilda au Jaquiline au Rose etc kakamatwa na hiyo midawa,the same kwa wanaume.Look at the names you will understand what I mean

Duh! eee bhana eee !
 
elimu ni muhimu mkuu, mfano nenda mikoa iliyoathirika kwa ukimwi mfano Njombe,Iringa,Mbeya waathirika wakubwa ni akina jane,jacline,winfrida, rose , wangepata elimu wasingejihusisha na ukahaba,
 
elimu ni muhimu mkuu, mfano nenda mikoa iliyoathirika kwa ukimwi mfano Njombe,Iringa,Mbeya waathirika wakubwa ni akina jane,jacline,winfrida, rose , wangepata elimu wasingejihusisha na ukahaba,

Hilo kwako nililitegemea. Uelewa na uwezo wako ni ubishi wa kwenye vijiwe vya gahawa na sio zaidi ya kejeli.
 
Hilo kwako nililitegemea. Uelewa na uwezo wako ni ubishi wa kwenye vijiwe vya gahawa na sio zaidi ya kejeli.

Wewe ndio pimbi, mwenzako kajibu kwa kutumia akili, kwani huyo aliyeleta mada alijibu kijinga. swali la kijinga hujibiwa jibu la kijinga..
 
elimu ni muhimu mkuu, mfano nenda mikoa iliyoathirika kwa ukimwi mfano Njombe,Iringa,Mbeya waathirika wakubwa ni akina jane,jacline,winfrida, rose , wangepata elimu wasingejihusisha na ukahaba,
umesahau na bukoba na maeneo ya jirani yenye wasomi wengi na ukimwi wakumwaga(wanawake wao utawakuta kwenye vibanda vya mitaa fulani ya jijini wakijiuza).
 
mnakoelekea sio kuzuri ni vema mkajikita kwenye maada
 
Back
Top Bottom