Hali hiyo, wanaielezea ilisababisha kuanguka chini na wakazidi kumshambulia hadi wakahakikisha amekufa huku vijana wake wa kazi wakiingia mitini.
Ofisa wa Polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa kuwa yeye si msemaji wa jeshi hilo, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. Taarifa hiyo ya Polisi ilieleza kwamba, mgogoro huo ulizuka baada ya wananchi hao kumtuhumu Mabina kuwa ana mpango wa kuuza eneo lao la kijiji
kwa mwekezaji.
Ni mapema mno kuelezea tukio hili kwa undani hasa ikizingatiwa kuwa mimi siyo msemaji. Subiri msemaji wa jeshi atawapa taarifa kwa undani, alisema ofisa huyo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Christopher Fuime alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema wanaendelea kufanya uchunguzi.
Tulipata taarifa ya kuwepo kwa tukio hilo na kutuma vijana wetu kwendakutuliza vurugu, alisema Fuime. Alisema Mabina hakuwa na dhamira ya kuua, ila alijaribu kufyatua risasi hewani kwa lengo la kuwatuliza na ndipo ilipompata mmoja wao.
By Miguel Suleyman, Mwananchi
Imewekwa Monday, December 16
2013 at 08:05