Mabilioni ya Escrow yaliyotoroshwa sasa kurejeshwa nchini

Mabilioni ya Escrow yaliyotoroshwa sasa kurejeshwa nchini

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,269
Reaction score
25,312
Timu kabambe ya uchunguzi ikiongozwa na wataalamu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema kuwa itahakikisha kila senti iliyofichwa nje ya nchi inarejeshwa ili haki iweze kutendeka kwa wahusika.

Msako huo wa nchi za nje unatokana na kuwepo kwa taarifa za baadhi ya wanufaika wa mgawo wa mabilioni hayo kuwa walitoroshea fedha hizo barani ulaya na maeneo mengine mbalimbali duniani. Aidha, harakati hizo za uchunguzi zinalengo moja tu kwamba hakuna fedha inayohusishwa na tuhuma hiyo ambayo haitafikiwa ikiwa ni pamoja na zile zilizokuwa zikizungumziwa bungeni zilizochotwa kwenye benki kwa mifuko ya sandarusi na ile ya rambo.

Imeelezwa kuwa eneo kubwa ambalo limelengwa na uchunguzi huo ni bara la Ulaya ambako inasemekana ndio kuna kiasi kikubwa cha fedha kimehifadhiwa na wanufaika wa mgawo huo.

Mussa Misalaba Ofisa Mahusiano wa TAKUKURU amesema kuwa ni kweli tuna maofisa wetu wa TAKUKURU wamekwenda nje ya nchi kufuatilia fedha za Escrow, kwa sasa siwezi kutaja kuwa ni nchi gani hasa tunazozifuatilia maana huu ni uchunguzi. Hata hivyo, ameongeza kuwa taasisi hiyo ya TAKUKURU imeamua kushirikisha taasisi zingine za Kimataifa katika kuwachunguza zaidi baadhi ya watuhumiwa wa Escrow kama wamehifadhi fedha hizo nje ya nchi.
 
Bongo kwa kutafuta kiki mnatuona wote mazuzu,Takukuru ilikuepo Wakati taharifa ya Bunge ikisomwa kuwa zipo zilizochotwa kwa masandarusi na zingine zilipitia Bank binafsi mlikaa kimya hamkutoa neno mpaka mkulu kipindi hicho akazitetea kuwa sio fedha za Umma..Leo hii mliokaa kimya mnapiga kelele...
 
Rais John Pombe Joseph Magufuli
Atauwa Watu Yaani Mpaka Sasa Ni Bhalaa
 
Pia wale wa tshs 400,000 kwa siku moja kwa moja TAKUKURU iwachunguze haraka sana, sbb ni ufisadi mkubwa pia
 
Niko huku walikozificha, kama wataniletea kwenye sandarusi ntawahifadhi kwenye acc yangu
 
"Walikuwa," ni akina nani hawa.Mkuu bado huja-grasp ukweli kwamba huu ni utawala mpya wenye mitazamo mipya na malengo mapya?Huu sio utawala wa Mwinyi,Mkapa au Kikwete mkuu.Wake up brother,this is a new dawn.
 
Hii ni kupotezeana bure mda wa kujadili issues za maana. Kwani si tume iliindwa wakachunguza wakawajua watu waliobeba pesa kwa sandarusi na rambo hata magunia...lakini hiyo riport iliwekwa chini ya kiti hadi Leo. Then watu wanaanza kutumia ghalama kubwa kuchunguza nje ya nchi..najiuliza mapesa yote hayo yaliwezaje kutoka nchini?
 
Bongo bahati mbaya,mbona waliochukua cash STANBIC BANK mnapata kigugumizi cha kuwataja?
Makonda alipowataja hadharani watuhumiwa wa biashara ya madawa ya kulevya akiwemo mheshimiwa wenu yule, mulilalamika sana kwamba ni uvunjifu wa sheria. Serikali ikawasikia na kusitisha zoezi hilo na badala yake kulifanya kimya kimya kama ambavyo mlipendekeza.

Sasa kwa nini mnataka hawa watuhumiwa wa ufichaji wa fedha zetu nje ya nchi watajwe hadharani wakati uchunguzi haujakamilika na watuhumiwa kufikishwa mahakamani? Itakuwaje kama kwenye hao watuhumiwa wapo pia viongozi wakuu wa chama chenu?
 
Yale yale ya pesa za uswisi,
story tu,

kule kuna numbered account,huwezi kutrace hata siku moja,
kama ni kweli wataje hao walioweka hizo pesa..

Mimi nawashauri wambane singer aachia account zake za benki kwa sharti la kuyamaliza nje ya mahakama,
then akishatoa hela zote pia akabidhi funguo za jenereta then aondoke na kandambili kama alivyokuja
 
Back
Top Bottom