Mabilioni ya EPA kuanza kugawiwa kwa wananchi Dar es Salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabilioni ya EPA kuanza kugawiwa kwa wananchi Dar es Salaam

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Mar 31, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,079
  Trophy Points: 280
  Huu ni utapeli wa hali ya juu. Wameshindwa kuthibitisha pesa zimekusanywa toka kwa kina nani na kiasi gani na wamezikusanya kwa njia ipi kama ni cash, cheque, money order n.k. zimewekwa kwenye account # gani na katika bank ipi. Sasa kuficha uwongo wao wanataka kuzigawa pesa hizo. Duh! JK nchi imemshinda jamani! Huo mgao utakuwa ni kiasi gani kwa kila Mtanzania? Kwa nini pesa hizi zisipelekwe TANESCO kama kweli zipo?

  Posted Date::3/31/2008
  Mabilioni ya EPA kuanza kugawiwa kwa wananchi Dar es Salaam
  *Zoezi kuanza Jumanne Makao Makuu Polisi
  *IGP, Gavana Ndulu kusimamia zoezi hilo

  *Lengo ni kupunguza makali ya maisha

  Ramadhan Semtawa na Tausi Mbowe

  WAKATI miezi sita ikiwa haijakamilika, mafisadi waliochota mamilioni katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) leo wanaanza kumwaga mapesa hayo kwa Watanzania.

  Uamuzi huo umekuja baada ya serikali kuwabana mafisadi hao walipe fedha hizo ili zitumike kupunguza makali ya maisha kwa Watanzania waliowengi, ambao wamekuwa wakipata mlo mmoja kwa siku.

  Hadi jana fedha zilizorudishwa na mafisadi, zilivuka lengo kutoka Sh 133 bilioni mabazo ziliibwa katika EPA hadi kufikia Sh200bilioni ambazo ni ongezeko la Sh67bilioni.

  Kutokana unyeti wa zoezi hilo, Jeshi la Polisi Makao Makuu ambako malipo hayo yatafanyika limeandaa ulinzi mkali ikiwemo wa mbwa kuhakikisha hakuna mtu anavuruga zoezi la malipo hayo ya mabilioni kwa kila Mtanzania.


  "Tumeamua kuweka ulinzi mkali, askari wetu wamejiandaa vya kutosha kuweza kukabaliana na vurugu za aina yoyote wakati wa malipo ya fedha hizo," alisema Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP) Said Mwema, wakati akizungumzia zoezi hilo.


  IGP Mwema alifafanua taratibu za watakaoweza kupata mgawo huo kwamba, wote ambao ni Watanzania wa kuzaliwa, ambao wanapaswa kuwa na vyeti halisi vya kuzaliwa, kitambulisho cha kupigia kura au hati ya kusafiria.


  Akizungumzia mchakato huo, Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, alisema uamuzi huo unatokana na kuona makusanyo yamezidi lengo lililowekwa.

  Profesa Ndulu alifafanua kwamba, kutokana na makusanyo hayo kuzidi lengo uongozi wa BoT uliishauri serikali kugawa ongezeko kwa wananchi wenye maisha magumu ili kutimiza ahadi ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania.

  "Tumeona ni vema ongezeko tuligawe kwa Watanzania ambao wamekuwa wakipata mlo mmoja kwa siku, hii pia ni sehemu ya kutimiza ahadi ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania,"alisistiza Profesa Ndulu.

  Hata hivyo, alipoulizwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Kuchunguza Mafisadi wa EPA, Johnson Mwanyika ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), alisema orodha kamili ya mafisadi itatangazwa baadaye kwa sasa zoezi linalofanyika ni kugawa mabilioni kwa Watanzania.

  "Jambo la muhimu kwanza lilikuwa kukusanya pesa, kinachofuata ni kuzigawa kwa Watanzania, hatua ya kutangaza majina kamili ya mafisadi hao ikiwa ni pamoja na kuwafungulia mashitaka, itafuata baada ya kukamilika mchakato," alisisitiza Mwanyika.

  Hata hivyo, IGP Mwema, Profesa Ndulu na Mwanyika wote kwa pamoja hawakueleza zoezi lingeanza saa ngapi na kukamilika kwa muda gani.

  Badala yake, walisema taarifa zaidi zitatolewa leo katika taarifa yao mpya kwa umma kupitia vyombo vya habari.

  Aprili Mosi, siku ambayo ni maarufu Duniani kama Sherehe ya Siku ya Wajinga.
   
 2. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Ndugu yangu umesahahu kwamba kesho ni tarehe moja mwezi wa nne? na unajua hiyo siku huendana na nini?Siku ya wajinga ati, ukienda kujipanga foleni kusubiri mabilioni ya EPA......shika breki! Tangu lini serikali ikagawia wananchi pesa taslimu? wajinga ndi waliwao.. kaa chonjo.
   
 3. Geeque

  Geeque JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2008
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 848
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  April Fools Day hahahahahah
   
 4. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ama kweli siku ya wajinga imekuja one day before!
   
 5. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..hii kuitoa leo ni ujinga vile vile!

  ..ila sentensi za mwanzo nilipatikana!
   
 6. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hata April Fools inabidi uweke story kidogo iliyo believable, hawa naona wanacheza yaani ukianza kuisoma tu hata kama ulisahau kuhusu April Fools unakumbuka.
   
 7. K

  Kigoma Member

  #7
  Mar 31, 2008
  Joined: Jul 10, 2006
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii habari imetoka baada ya saa sita za usiku......saa za Afrika Mashariki...kwa walio ughaibuni....muda wa April fool's day bado kwa walio TZ...tayari!

  Na isitoshe chini ya hiyo habari wameaandika hapo.....ungeisoma vizuri ungeng'amua hilo.
   
 8. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Mwananchi huchapicha habari za gazeti la kesho kwenye mtandao siku moja kabla, na ndo maana habari hiyo unaisoma sasa hivi kabla siku haijaisha.
   
 9. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..we uko wapi na mahesabu ya hizo saa umeyapata wapi?

  ..mpaka sasa bongo bado ni 31.03.2008!
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Apr 1, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,079
  Trophy Points: 280
  Nilidhani nitawapata watu na kuamua kuweka nyongeza yangu pale juu , kumbe hamjalala....:)

  Ningeondoa hiyo sentensi ya mwisho labda kuna baadhi wangechoteka....:)
   
 11. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #11
  Apr 1, 2008
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,865
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  APRIL FOOLS DAY (01/04): “BUBU ATAKA KUSEMA” Don’t fool us, we are adults !!!!!
   
Loading...