Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,353
- 26,194
Mahakama ya Rufani ya Tanzania imeiamuru TANESCO kuilipa DOWANS takribani bilioni 90. Ni baada ya DOWANS kufanikiwa kuweka pingamizi la kisheria dhidi ya TANESCO waliojaribu kupinga utekelezaji wa Tuzo ya DOWANS waliyopewa katika Mahakama ya Uamuzi wa Kibiashara huko London. Wamiliki wa DOWANS hawajawekwa wazi. Hata Rais Kikwete alikaririwa kuwa hawajui wamiliki wa DOWANS. Sasa, mabilioni ya DOWANS atalipwa nani? Ni Rostam Aziz anayedai kuwa na Nguvu ya kisheria(Power of Attorney)? Ni Wakili Msomi Fungamtama aliyeitetea DOWANS tangu shauri likianza? Au sasa mmiliki anajulikana?