Mabiliioni yameliwa na wajanja!

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Mabilioni yameliwa na wajanja lakini walipaji ni sisi!

Tarehe 2 Oktoba Mwaka 2000, Askofu mkuu Zacharia Kakobe wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship Church alifanya Mkutano na waandishi wa habari. Na haya ndiyo maneno aliyoyasema

“Napenda kuwashukuru waandishi wote wa habari ambao mmeweza kufika hapa kwa kuacha kazi zenu nyingi. Nahesabu kwamba jambo hili, ni la maana sana.

Kwanza, napenda nizungumze katika hatua za mwanzo kabisa ni kipi kilichonifanya kuingia katika siasa kichwa kichwa. Kwa nini imenibidi kuacha habari za kanisani kwa namna moja ama nyingine kwanza halafu nikaingia katika siasa kichwa kichwa

Pale mwanzo sikuwa na dhamira yoyote ya kuingia katika majukwaa ya siasa, na nililieleza jambo hili katika mikutano na waandishi wa habari mapema mwaka huu, na katika kipindi cha Kiti kimoto.

Lakini lipo jambo lilinilazimisha. Hali ya Tanzania ni mbaya. Hali ya nchi hii ni mbaya, na tatizo kubwa linaloifanya nchi hii kuwa na hali hii mbaya ni rushwa na siyo kitu kingine.

Tanzania ina rasilimali nyingi. Tanzania ni nchi ina madini. Ni karibu nchi ya nne katika Afrika, nchi tajiri, nchi nzuri. Ina maziwa na bahari kubwa inayoizunguka, na ardhi kubwa tofauti na nchi ya uingereza au ya Denmark, hivi ni vi-nchi vidogo vidogo ambavyo vinahangaika na ardhi

Kwa hiyo kumekuwa na kelele wakati wote kwamba nchi yetu imekithiri kwa umaskini, umaskini umekithiri. Sawa, tusingekuwa maskini kiasi hiki.

Kenya hawana sababu yoyote ya kutuzidi. Kwa sababu dola ya Kimarekani ni karibu Sh. 79 za Kenya wakati sisi ni zaidi ya Sh. 800.

Sisi tunawazidi katika maeneo mengi sana. Madini yao mengi yanatoka hapa kwetu kwa njia za panya na yanauzwa kwa jina la Kenya, lakini yanatoka hapa.

Mlima Kilimanjaro wanapiga kelele katika sehemu za Ulaya na mahali pengine duniani kwamba uko Kenya wakati mlima huo hauko Kenya.

Kwa kuwa wao wameweza kupiga kelele, watalii wanakwenda Nairobi kuangalia mlima Kilimanjaro na inajulikana nje kwamba mlima huo uko Kenya.

Nchi zote zinazotuzunguka hapa,karibu hazikuwa na sababu ya kuwa na nguvu yoyote ya kiuchumi kuliko sisi. Nchi ya Uganda kwa mfano, ambayo wanakwenda vizuri kiuchumi kuliko nchi yetu, ambayo wakati ule ilikuwa katika hatua ya mbali kabisa

Lakini wanapiga hatua sana. Sasa tatizo ni nini. Tatizo bila shaka ni rushwa. Rushwa ndiyo inayofanya nchi hii kuwa hivyo ndivyo ilivyo. Ni rushwa kubwa ya vigogo

Mnaweza kuona Nigeria. Nigeria kulingana na takwimu za shirika linalojishughulisha na kutokomeza rushwa duniani lijulikanalo kwa jina la Transparency International (TI), ndiyo nchi ya kwanza kwa rushwa duniani na katika Afrika

Na kwa kulingana na takwimu hizo za TI, nchi yetu ipo katika nchi 10 hatari duniani, zilizobobea kwa rushwa katika miaka mitatu mfululizo; mwaka juzi, jana na mwaka huu (200)
Sasa,ilivyo ni kwamba Nigeria ni nchi ambayo ni tajiri sana. Ina mafuta mengi kuliko nchi nyingine yoyote katika Afrika. Ina madini mengi sana. Ni nchi tajiri sana na ina rasirimali nyingi za ndani ya nchi.

Lakini kwa sababu ni nchi ya kwanza kwa rushwa duniani, imekuwa miongoni mwa nchi maskini kwa namna ambayo isingetarajiwa, kwa sababu madeni waliyonayo Nigeria ni karibu mara mbili kuliko tuliyo nayo sisi.

Na kulingana na takwimu za 1995, wakati huo sisi tukiwa na debt per person (deni kwa mtu mmoja) karibu dola 162.0 Nigeria ilikuwa ni zaidi ya dola za kimarekani 300, deni kwa mtu mmoja. Hivyo, ndivyo nchi ya Nigeria ilivyo,na hali inazidi kuwa mbaya zaidi

Sasa tatizo ni kwa nini. Kwa nini madeni . mzigo wa madeni,tunaambiwa tunalipa madeni. Mzigo wa madeni ni mkubwa, lakini Watanzania hatuambiwi haya madeni yanatoka wapi na kwa nini hali ni nzito sana kiasi hiki

Rushwa nyingi zinafanyika katika mtindo wa zabuni. Kwa hiyo, kama kuna zabuni au tenda,unaposikia kwamba huyu anapata zabuni ya kujenga kitu Fulani, labda cha SH. Milioni 200, hizo ni zile zilinazoandikwa, lakini kimsingi fedha inayotumika katka kiasi hicho kinachozungumzwa, cha Sh. Milioni 200, sicho hicho

Hapa ninazo takwimu za TI, shirika lile la kimataifa la rushwa. Katika mtandao wake wa kompyuta,ambao mtu yeyote anaweza akausoma,kuna kitu hapa kinaitwa TI: Tanzania National Chapter

Halafu, wanazungumza hapa ; The Arusha Integrate workshop. Wanazungumzia juu ya Tume ya Jaji Joseph Warioba,ambayo iliteuliwa na Rais January, 1996 na kukamilisha kazi yake, Desemba 7,1996

Tume hiyo ya Warioba,ilieleza kwamba, kwa ufupi tu hapa….nachukua dondoo kidogo tu kwa maana ni mengi sana yanazungumzwa humu. Kwamba katika mikataba 24 ya ujenzi,ambayo iliangaliwa na tume hiyo,gharama halisi ambayo ilikuwa imekisiwa kwa ajili ya miradi hiyo ilikuwa ni Sh. Bilioni 60

Lakini,kiasi hiki kilipaishwa hadi kufikia karibu Sh.bilioni 97 kwa ajili tuu ya tofauti ya gharama au bei zilizozungumzwa katikati yao hao ma- contractor na serikali

Taarifa hii inaeleza kwamba Tume ya Jaji Warioba ilipoona mambo haya ilipata shock, ilipata mstuko. Ndivyo taarifa hi inavyoeleza. Kwa sababu katika hicho kiasi cha zaidi ya Sh. Bilioni 97, yaani bilioni 36 hakikuwa na maelezo ya kuridhisha.

Maana yake nini. Gharama halisi ingekuwa shilingi bilioni 61, hii ndilo deni hailsi la watanzania. Lakini watanzania katika miradi hiyo 24, tunalazimika kulipa deni la shilingi bilioni 97, yaani bilioni 36 zaidi ya gharama halisi na hizi hazina maelezo

Zimeingia ndani ya mifuko ya vigogo na kuwa mzigo mzito unaowaelemea watanzania. Zimeliwa na watu wachache tu, wazito serikalini yaani wazito wa CCM.

Taarifa hii ya TI, inasema kiasi hiki cha fedha cha shilingi bilioni 36, kilicholiwa,kilitosha kabisa kwa wakati huo, mwaka 1994; kujenga barabara ya lami yenye kilomita 278 kwa viwango vya gharama ya wakati huo ya shilingi milioni 129.9 kwa kilomita moja

Ukiangalia kwa macho, unaweza ukaona kwamba tumekosa barabara ya lami ya kilomita hizo,na sasa tunabebeshwa madeni tulipe deni hilo la Sh. Bilioni 36

Kazi ya madeni haya ukiangalia kwa macho haipo. Lakini mzigo wa madeni unawaelemea watanzania. Hivi ndivyo inavyotokea katika nchi hizi maskni, kwa sababau fedha nyingi za miradi ya namna hiyo ,haziwi za kwetu, ni za kukopa nje.

Taarifa hii ya TI, inaeleza pia kwamba kulikuwapo na mradi wa Dar es salaam Road Rehabilitation Program (DRRP). Mradi wa DRRP,ulihusisha barabara saba za mkoa wa Dar es salaam ambazo zingetengenezwa, na gharama halisi iliyokadiriwa ilikuwa zaidi kidogo ya shilingi bilioni 6.0

Lakini gharama hizo zilipaishwa zaidi na kuwa shilingi bilioni 9.0, zilikuwa kama shilingi bilioni 8.9,ambayo karibu ni karibu ya bilioni 9.0. Hapa zikaongezwa shilingi bilioni 3.0

Huu ndiyo mzigo wa madeni unaowaeelemea wananchi. Lakini waliokula fedha hizo, hatuambiwi wako wapi hatuambiwi pia… haya ni madondoo mawili tu,yapo mengi

Kwa mfano;katika viwili tu hivyo nilivyovitaja hapo awali, zaidi ya shilingi bilioni 45, kati ya shilingi bilioni 64 zilizokadiriwa kwa miradi hiyo, zinazungumzwa na shirika hili la TI kwamba ziliingia katika mifuko ya watu na sasa watanzania tunalazimika kuchangia

Tuambiane ukweli basi. Kwa Rais Mkapa alipoingia madarakani mwaka 1995 alitupa matumaini makubwa sana. Nafikiri leo nisingekuwa na haja ya kupiga kelele, hata kwa kumtaja hadharani rais wangu

Mwalimu Julius Nyerere, ni mtu wa kuheshimiwa. Na hata kama unataka kuheshimiwa na sifa yako iendelee kuwapo…hapa nawaonya wanasiasa. Kama unataka kuharibu sifa yako, wewe mchokonoe Nyerere. Utaharibu sifa yako, na utaishusha chart yako mara moja.

Kwa sababu huyu mtu alikuwa anakubalika na anaheshimika. Mwanasiasa yeyote, unatakiwa uwe mjanja kuona huyu mtu anakubalika kiasi gani hata kama una ajenda zako unazificha na ujue ni lipi la kuzungumza juu yake

Na Mwalimu kwa anavyokubalika katika taifa letu. Akatueleza , jamani eh,hapa kuna watu wengi wanataka urais

Wapo hawa akina Kikwete (Jakaya kikwete), hawa kina lowassa (Edward Lowassa) na wengine hawa lakini akazungumza;wako watu kati yao wanajulikana na ingekuwa ni rahisi kwake kuwauza kwa sababu majina yao ni makubwa

Lakini akasema nini wasiwasi na usafi wao. Na hata akawanyooshea kidole baadhi ya watu hao,lakini akasema yuko mtu safi miongoni mwao, Mkapa

Akampamba…...oh,huyu kijana amekuwa waziri wetu. Lakini ingawa amekuwa waziri wetu hafahamiki. Jina lake halijulikani,lakini ni mtu safi

Akasema kwa hiyo,kwamba kwa kuwa huyu ndiye pekee msafi kati ya wote wanaotaka urais,itakuwa ni vizuri kumpitisha huyu katika kipindi hiki ambacho hali ya nchi inatisha

Mzee wetu alikuwa mkali sana katika masuala ya rushwa tangu mapema. Alikuwa mkali sana katika jambo hilo na wakati mwingine hakumuonea haya mtu, alilazimika kumchapa bakora hadharani mtu ambaye amebainika na rushwa

Akatuambia Mkapa ni safi, lakini ninapata shida kumuuza. Akasema potelea mbali niko radhi kuzunguka nchi nzima kumuuza. Na kweli, hakukuwa na mtu aliyeweza kumpa misukosuko ya wazi wazi Mkapa wakati ule wa kampeni

Basi nasi tukamkubali. Na alipoanza kazi yake tu akatangaza kwamba hatakuwa na suluhu kwa wala rushwa

Hilo likanifurahisha sana. Nikasema kama huyu hatakuwa na suluhu katika suala hili la rushwa,basi nchi yetu itakuwa na mabadiliko makubwa sana katika miaka yake mitano ya mwanzo kwa sababu hili ndilo tatizo na chanzo cha umaskini wetu

Kilichotokea sasa. Mimi nikawa naangalia,nikisubiri rais wetu hatakuwa na suluhu kwa namna gani. Miezi miwili tu baada ya kuingia Ikulu,January,akafanya kitu kikubwa sana ambacho hata taasisi ya Transparency International, inakisifia kwa kueleza heshima zake kwa rais Mkapa. Akaunda Tume ya Warioba

Hicho kitu kilionyesha kwamba rais wetu alikuwa na dhamira kubwa sana ya kukabiliana na rushwa. Na aliagiza tume ili impe mapendekezo ya namana ya kukabiliana na rushwa. Hiyo ilinitia moyo sana mimi na watanzania wengine tunaochukia rushwa

Sasa hiyo 96,mwaka 1997,Mkapa akawa anaiangalia angalia ripoti ya tume ya Warioba. Nyie waandishi wa habari mkapiga kelele sana,mbona watu hao hawashughulikiwi.

Nakumbuka baada ya nyie kupiga kelele, majibu yake yalikuwa kwamba ripoti ya tume haikuwa ushaidi wa kumfikisha mtu mahakamani

Akawa mkali kama shubiri…oh, hapa hakuna ushahidi wa waziwazi wa kuweza kumfikisha mtu mahakamani…oh, hii ni ripoti inayoeleza mianya ya rushwa, bado tunaendelea kuangalia na kufanya uchunguzi wa kina

Ripoti hiyo akaiangalia mwaka 1997. mwaka 1998 bado akaiangalia tu. Mwaka 1999 bado tu anaiangalia na mwaka 2000,wakati akijua kwamba nchi yetu iko katikatika ya nchi 10 hatari hatari za rushwa iliyobobea kwa mujibu wa Transparency International, yeye bado anaiangalia angalia

Na mwaka 200 sasa, bunge letu tukufu ambalo lina wabunge wengi wa CCM, ambo ndio hao vigogo ambao ndio tunaoweza kuwatuhumu kuwa katika mambo haya ya rushwa, baada ya kuona Baba wa taifa, Mwalimu Nyerere hayupo duniani,bunge letu tukufu likapitisha sheria ya Takrima

Ndugu zangu, kama Mwalimu angekuwepo hai leo hii,sheria hii ya takrima isingepitishwa. Walitudanganya hawa watu kwamba mazishi yake (Mwalimu) yalikua karibu Bilioni moja, wote tukalia katika maombolezo yake na wengine wakafa kwa ajili ya kumlilia Mwalimu

Katika Kiswahili, neno takrima au Hospitality kama waingereza wanavyoita, ni kwamba mwenyeji unapotembelewa na mgeni, ukamfanyia cho chote kile kitu kama kumkaribisha kinywaji au chai, hapa unakuwa umemkirimu,unakuwa umemfanyia Takrima. Kumkaribisha mgeni wako ajisikie yuko nyumbani

Kwa kawaida takrima hufanywa na mwenyeji kwa mgeni wake. Lakini katika sheria ya waheshimiwa hawa,wao wagombea ubunge na udiwani ndio wanaokuwa wenyeji kule vijijini waendako kuomba kura za nyumba kwa nyumba na kutoa takrima wao,mambo ya ajabu haya (Kicheko)

Watanzania nataka mfunguke macho, kama hamjafunguka macho kwa haya ninayoyasema basi,tumekwisha. Mgeni ndiye, atoe takrima kwa mwenyeji?! Ni kinyume kabisa cha hata ya maana yenyewe ya takrima. Hiyo ndiyo rushwa ya kupeana vyakula, pilau na Khanga.

Sasa yale yaliyokua haramu miaka hiyo sasa ni sheria iliyopitishwa na bunge. Kwa hiyo hutaweza tena kushitaki kosa hilo la pilua,chumvi na khanga. Lakini pia utatakiwa uwe na uwezo wa shilingi milioni 5 ili kesi yako ipokelewe pale mahakamani.

Hawataki kabisa wewe usiyekuwa na uwezo ufurukute kuingia katika kundi lao la wateule, vigogo wenye neema….wakapitisha sheria hiyo, nikakereka sana ndani ya moyo wangu.

Hapo imani ikaniisha kabisa. Nina majukumu mengi ya kanisa wakati huo sijawaza hata kupanda katika siasa

Baada ya kura za maoni ya CCM. Kwanza mimi ningependa niseme mtu wa kumlaumu ndani ya CCM, na mtu atakayewafanya hawa CCM washindwe, wasimlaumu kakobe. CCM iwalaumu nyinyi waandishi wa habari.

Ni nyie mlio high light katika magazeti yenu suala la rushwa. Nadhani mlifanya hivyo bila kujua,lakini hata mtoto mdogo aliona namna rushwa inavyofanyakazi ndani ya CCM. Mngenyamaza kimya, hawa watu wa CCM wangepeta tu lakini nyinyi mmewaharibia,siyo mimi kakobe.

Hoja hii ilitolewa na Askofu Mkuu Zacharia Kakobe miaka 11 iliyopita lakini kwa haya yanayotokea nadhani ni vizuri kupitia maudhui yake tuone kama bado hoja yake hii ina mantiki. Yaani watoa RUSHWA wanaweza kukataa kupokea rushwa?
 

Attachments

  • mabilioni yameliwa na wajanja.doc
    63.5 KB · Views: 118
Kakobe aliyaona mengi na yote aliyoyazungumzia wakati huo ndiyo hayo hayo tuna yazugumza sasa.

Tatizo kubwa la Tanzania ni tatizo la uongozi. Na hili linaendelea kutusumbua na litaendelea kutusumbua mpaka pale ambapo tutaondoa unafiki na mzizi wa fitina. Tatizo kubwa tulilonalo ni makundi, usiri usiri, umbea umbea nk, ndivyo vitu vilivyotawala siasa zetu.

Hili linafanywa na makundi ya watu waovu, MAFISADI wasiopenda maendeleo ya nchi, nafurahi sasa yameanza kusambaratika. Na nafikiri yataendelea kusambaratika tu. Hata wale wezi wakubwa huwa wanafikia wakati laana zinawafikia wanachapana wenyewe kwa wenyewe. SASA hata hayo makundi hayahaminiani. Na siku za usoni yatazidi kujichanganya na wananchi tutazidi kupata ushindi.

Siku hizi hata yule ambaye roho inamsutwa kuwa ni FISADI akisemwa/akiguswa anasema ameonewa wivu kwa sababu ana mali. Jamani jamani tuoneni aibu.

Lakini labda cha kuwakumbusha hata watawala hakuna marefu yasiyo kuwa na ncha. Kila kitu kina mwisho wake.

Ni vizuri mtu ajisafishe akiwa bado ana nguvu zake, kuliko kusubiri kubebwa kwenye machela kupelekwa mahakamani kujibu tuhuma alizo zifanya miaka 20/30 wakati ukiwa kiongozi.

Ilimradi Tanzania itaendelea kuwepo na sheria zetu zipo ndio maana mimi huwa na sema Ipo siku mnyonge atapata haki yake. Kuanzia kipindi Kakobe ameyasema haya na sasa na tunapoelekea, nakwambia itafika wakati watu watajipeleka wenyewe mahakamani.
 
Kakobe ni Mzee wa CCM maana kwenye mkutano wa CCM na JK Mkoa wa Dar likaa high table .I was there and I saw him na hata wewe ulimuna je kwa nini asimweleze JK uso kwa uso ? Kanisa lake lina waumini wengi na wenye shida sana ya maisha lakini wanaichagua CCM mbona asiwaeleze ukweli na waache kuichagua CCM ?
 
Naomba nisituhumiwe kwa udini. Kwanza nampongeza Kakobe kwa matamshi haya, yana maana na uzito uleule kipindi alichoyatoa na hata sasa. Inafaa watu wenye ufuasi wa watu wengi kama Kakobe wasimame kukemea maovu, maana sauti yao ni nguvu ya wale wasioweza au kuthubutu kusema, voice of the voiceless. Tumeona viongozi wengi wa kidini wakisimama kidete kutetea haki, kama Askofu Mkuu Desmond Tutu, Dalai Lama, nk.

Lakini nasita kuamini kuwa Kakobe (na wengine wa aina yake hapo Dar kama "nabii" Mwingira) anaweza kufananishwa japo kwa 0.1% na Desmond Tutu au Dalai Lama. Hawa aina ya kina Kakobe ni wanyemelezi (opportunists) wanaotumia shida za watu kujipatia umaarufu na kujinufaisha, na kamwe hawasimami kuwatetea! Ni watu wanaoahidi "miujiza katika yaliyoshindikana", na ni wajanja sana kutaja yaliyoko kwenye jamii husika: umasikini, magonjwa, ukosefu wa ajira, uchawi na mapepo, na yote suluhisho lake ni maombi ambayo gharama yake ni kutoa ulicho nacho "kupanda mbegu". Ukienda Kongo (DRC) leo hii, utashangaa jinsi dini za aina hii zilivyo nyingi katika maeneo yenye umasikini uliokithiri, watu wanajazana kwenye makanisa kuomba miujiza, na wengine wanadai wameipata, lakini siku nenda rudi hali ni ileile au mbaya zaidi! Huko Nigeria kuna mikanisa lukuki ya aina hii, na ndiko kunakonuka rushwa, na hakuna hata mmoja wao anayekemea rushwa maana walaji rushwa wakishaipata hiyo rushwa wanaenda kwa "nabii", "mtume" au "askofu mkuu" kutoa "fungu la kumi" au shukrani! Wengine wanakuja kutoa "ushuhuda" jinsi "walivyopanda mbegu" kwa "mchungaji" au "nabii" huyo na kufanikiwa kuukwaa uwaziri, ugavana etc! Siku moja jioni nikiwa Dar niliangalia kipindi cha televisheni cha "nabii" mmoja wa Dar, mtu mmoja akawa anatoa ushuhuda jinsi alivyopanda "mbegu" katika kanisa hilo (ni pesa fulani mtu anatoa kama kianzio kwa ahadi kuwa maombi yake yatasikika kwa Mungu) na kufanikiwa kuteuliwa kusimamia zabuni (tender) katika sehemu anakofanya kazi! Ninavyoelewa jukumu kama hilo haliendani na ongezeko la mshahara, lakini kuna fursa za kupata "cha juu" ndio maana watu wanafurahi kupata nafasi hiyo. Je huu ni uadilifu? Na ni sawa kidini?

Leo hii nasikia Kakobe yuleyule na CCM ni "damu-damu". Je CCM imebadilika nini tangu alipoisema wakati ule akimsapoti Mrema? Nikimwita "opportunist" (mnyemelezi) nitakuwa nimekosea wapi? Hii saratani ya ufisadi imeingia kila mahali, na kwa masikitiko makubwa hadi huko kwenye dini inatunzwa na kulelewa!
 
Kakobe ni Mzee wa CCM maana kwenye mkutano wa CCM na JK Mkoa wa Dar likaa high table .I was there and I saw him na hata wewe ulimuna je kwa nini asimweleze JK uso kwa uso ? Kanisa lake lina waumini wengi na wenye shida sana ya maisha lakini wanaichagua CCM mbona asiwaeleze ukweli na waache kuichagua CCM ?

Kakaa,

Kakobe alisema haya mwaka 2000 na inawezekana alipokuwa amekaa na JK katika mkutano wa CCM alikuwa ameshasahau. Nadhani haya maneno mtu ayaprint vizuri na ampatie Kakobe asome tena miaka minane baada ya kusema,

Unajua kiongozi wa dini ni kiongozi wa dini tu. Maneno ya Kakobe ni more reality today than miaka nane iliyopita. Nimesoma mara mbili mbili sentensi zake. So valid, ni kiasi cha kubadili data na kuweka za sasa lakini content ile ile na rushwa imekuwa ufisadi
 
ccm inawezekana walijua influence ya kakobe kwa wafuasi wake. .....na ndio maana baada ya maika sita, unamkuta kwenye high table ya mkutano wa ccm
 
Kakobe ni Mzee wa CCM maana kwenye mkutano wa CCM na JK Mkoa wa Dar likaa high table .I was there and I saw him na hata wewe ulimuna je kwa nini asimweleze JK uso kwa uso ? Kanisa lake lina waumini wengi na wenye shida sana ya maisha lakini wanaichagua CCM mbona asiwaeleze ukweli na waache kuichagua CCM ?

Heshima yako mkuu....hii statement jamaa katoa ambayo KAKOBE aliongea miaka nane iliyopita yaani kama aliona maono sasa leo hii yanatokea kwa kasi ya ajabu...hajaongea jana wala juzi ni ya zamani miaka ya 2000 huko leo hii yamekubuhu.
 
Lakini mbona yule mama LWakatare haonyeshi makeke yake hakemiii UFISADI na yeye ni fisadi nn wakuu naombeni kueleweshwa..kwani sijamwona akilivalia njuga swala hili ikiwa yeye ni kiongozi wa jamii kwa pande zote za dini na kisiasa akiwa kama mbunge..kanyweaa kabisa.
 
Tutafika pabaya ndugu zangu, tusimame ktk hili la kakobe kuwa yeye aliyatazama ya leo na siyo mtu uanze kumcritisize, na si vema kusema kuwa huenda kakobe kashatekwa na ccm,
Hebu mnataka kutuambia CCMkazi yake ni kuteka viongozi wa dini kwa sasa( Lwakatare mbunge,kakobe,Gamanywa - KAMISHNA wa kuzuia ukimwi)
Nadhani hizi habari za imani tusichanganye sana na siasa
 
Uongozi wa Dini na kinyang'anyiro cha siasa za Tanzania lazima uchafuke tu.
Kipindi kile Kakobe wa TLP alikuwa amemaanisha kabisa kuipinga sisiem hadi kwa waandishi wa habari akasema anazo sababu 100 kwa nini sisiem haifai.Ilisadikika kuwa karibu kila Wilaya Tanzania Bara alikuwa na tawi la kanisa lake,Na kwa ushawishi ule makanisa yake yalipewa agizo la kumpigia Lyatonga Kura.

Sisiem waliliona mapema hilo ikabidi waingize Virusi kanisani kwake hasa kwa wafuasi wake wahoji mapato ya sadaka akafukuza wachungaji 16 kipindi hicho.Kipindi hicho Emmanuel Nchimbi aliamua naye kumpinga hadharani kwa kumshambulia kuwa mwizi anaibia watu pesa, mikufu ya dhahabu na magari pale Mwenge na anatembelea Nissani ya Million 40 wakati waumini wanapiga nyayo na kuomba lifti barabarani.

Hata siku ya mwisho wa kampeni za sisem Jangwani mzee Mkapa alisema kuna watu kama AKAKOBE wanaibeza sisiem,na itashinda kwa kishindo.

Kwa hiyo kama ilivyo kwa wanasiasa wengine,Kakobe naye alianza kufuatiliwa na virusi kwa kila kitu mpaka akapotea kanisani kwa siku 113 na kwa waandishi wa habari kwa miezi kadhaa.Alipotokea hadharani pale MANZESE kwenye ofisi za TLP ilikuwa ni kurudisha kadi na Pia ni dhahiri sisiem walimwonya kuwa akiendelea na kuikosoa basi hata lile jengo la Mwenge wangechora ramini yoyote ya uongo kwa plani ya miaka kadhaa nyuma kulikuwa kupite bomba la maji.

Sisiem haina utamaduni wa kukosolewa hadharani,ukifanya hivyo be ready to face un expected,iwe kifo au mirija yako yote ya uchumi kuzibwa(mfano mfanya biashara mmoja MWANZA,LEMA ENTERPRISES ns MAREHEMU Mwanajesi GEN.MARWA walivosapoti chama cha NCCR,yaliyowapata wanaofuatilia duru za siasa nchini wanajua).
Kakobe hayumo duruni leo lakini haya maandishi yake ni mhimu sana ktk Taifa letu
 
Kakobe ni Mzee wa CCM maana kwenye mkutano wa CCM na JK Mkoa wa Dar likaa high table .I was there and I saw him na hata wewe ulimuna je kwa nini asimweleze JK uso kwa uso ? Kanisa lake lina waumini wengi na wenye shida sana ya maisha lakini wanaichagua CCM mbona asiwaeleze ukweli na waache kuichagua CCM ?

Nadhani Kakobe alifanya vizuri kurudi ccm na kuwa mmoja wa supporters wa Kikwete. Hii inaonyesha kuwa Kikwete anakubaliwa na viongozi wa dini zote na sio waislam tu kama wengine wanavyotaka kuonyesha hapa.

Hayo mengine aliyosema hapo juu sina cha kusema.
 
Kakobe ni Mzee wa CCM maana kwenye mkutano wa CCM na JK Mkoa wa Dar likaa high table .I was there and I saw him na hata wewe ulimuna je kwa nini asimweleze JK uso kwa uso ? Kanisa lake lina waumini wengi na wenye shida sana ya maisha lakini wanaichagua CCM mbona asiwaeleze ukweli na waache kuichagua CCM ?

Hapo kuna fumbo kubwa sana Kakobe pekee anatakiwa atufumbulie. Kwanza inabidi atuambie kama msimamo wake kuhusu CCM umebadilika ama ni uleule. Yaani kama bado anaamini kuwa uongozi ndani ya chama hicho unapatikana kwa rushwa.

kitendo chake cha kuonekana mbele ya jukwaa kuu la CCM ni kama vile alikuwa anatuambia kuwa tayari mambo yamekuwa safi. jee kuna hatua zozote zimechukuliwa katika kupambana na rushwa tangu mwaka 2000 alipotoa maneno haya mazito yenye mantiki isiyokanika hata sasa
 
Kakaa,

Kakobe alisema haya mwaka 2000 na inawezekana alipokuwa amekaa na JK katika mkutano wa CCM alikuwa ameshasahau. Nadhani haya maneno mtu ayaprint vizuri na ampatie Kakobe asome tena miaka minane baada ya kusema,

Unajua kiongozi wa dini ni kiongozi wa dini tu. Maneno ya Kakobe ni more reality today than miaka nane iliyopita. Nimesoma mara mbili mbili sentensi zake. So valid, ni kiasi cha kubadili data na kuweka za sasa lakini content ile ile na rushwa imekuwa ufisadi


Maneno yako kwamba kuna watu walitangulia kuweka njia kwa kizazi hiki cha wanaharakati, yanamjumuisha na Kakobe?
 
Inapofika swala la maslahi kakobe hana tofauti na binadamu wengine wengi tu ambao hawawezi kusimamia yale wanayoamini hata ikibidi kufa,kama alivyofanya anayemwigiza kuwa anampenda (angempenda YESU kweli angeweza kusimamia ukweli bila kuwaogopa wauawo mwili).Laikini si hivyo dunia na mabo yake vinampeleka puta ndiyo maana anaweza kughilibiwa na kutishiwa nyau na akafiata mkia...Ameamua kuambatana na mfumo mbovu kwa maslahi binafsi na si vinginevyo
 
Heshima yako mkuu....hii statement jamaa katoa ambayo KAKOBE aliongea miaka nane iliyopita yaani kama aliona maono sasa leo hii yanatokea kwa kasi ya ajabu...hajaongea jana wala juzi ni ya zamani miaka ya 2000 huko leo hii yamekubuhu.

Na leo ni miaka 11 imeshapita na sisi kama taifa tumefanya nini kupambana na hawa wakwapuaji wa fedha zetu? Au kama kawaida yetu sisi ni watu wa matukio na hivi sasa tuko kwenye "upepo" wa Igunga na Wikileaks?
 
Back
Top Bottom