Sioni ubaya wowote iwapo jamaa hakufuata madaraka ndani ya Chama bali ni mwanachama wa kawaida kama wengine; inawezekana anataka kugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, that is fine as long as CHADEMA ina mfumo wa uongozi ulio wazi usioruhusu loopholes zinazoweza kuleta mfarakano ndni ya chama. Kule NCCR-Mageuzi kulikuwa na matundu kadhaa katika mfumo wao wa uongozi, kwa mfano Mrema alipewa uenyekiti bila kuwapo na uchaguzi, mwenyeketi alikuwa na mamlaka ya kuamua lolote analotaka hata bila kuwashirikisha viongozi wengine wa chama. Mfumo huo ulikuwa ndiyo chanzo cha mfarakano mkubwa katika NCCR-Megeuzi na ndiyo maana kilisambaratika. Kuna viongozi wengi, kwa mfano Profesa Baregu, waliohama NCCR-Mageuzi na kuingia CHADEMA na wanaendelea vizuri tu.