Mabehewa ya Treni kwa ajili ya usafirishaji mizigo yawasili

Chona

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
523
360
Kwa muda mrefu kumekuwa na kilio cha wadau wengi kuilalamikia serikali kwa kutoboresha reli ya kati ili iweze kusafirisha mizigo inayokwenda kanda ya ziwa, Kigoma, Burundi na Rwanda . Kilio hiki kinasababishwa na ukweli usiopingika kuwa barabara zetu zimekuwa zikitengenezwa kwa gharama kubwa huku matengenezo hayo yakidumu kwa muda mfupi kutokana na barabara hizo kutumika kupitisha gari za mizigo na wakati mwingine zikizidisha mizigo.
Kwangu mimi naona ni hatua nzuri na pengine niipongeze wizara husika chini ya waziri wake Dr. Mwakyembe licha ya kwamba wamechelewa ila wametupa matumaini. Hutuwezi kuwa tunatumia pesa nyingi kutengeneza barabara ambazo zinadumu kwa muda mfupi wakati hela hiyo ingeweza kutumika katika mipango mingine ya maendeleo. Yamewasili mabehewa 50. Mwezi ujao yatawasili mengine idadi hiyo hiyo. Lakini jumla yataletwa mabehewa 274.

Mabehewa.jpg
 
Back
Top Bottom