Mabati ya Kiboko G28 yana matatizo, TBS mko wapi?

Kamakabuzi

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2007
Posts
2,904
Reaction score
1,364
Nimenunua mabati ya kiboko G28 lakini wakati wa kuezeka fundi akanieleza kuwa hayakai kwenye usawa kama ailvyozoea.
Nilipoyapima nikapata vipimo vifuatavyo
Upana: sehemu ya chini ni cm 82 na sehemu ya juu ni cm 86
Diagnal: moja ni cm 310 na nyingine ni cm 312
Kwa mshangao mkubwa mabati haya yana nembo ya TBS.
Je nifanyeje? TBS mnakagua kiwanda hiki?
 
Hiyo moja, subiri miezi sita yaanze kupata kutu ndiyo ushangae zaidi.
 
Nilitarajia watu wa kiboko waje kutueleza tufanyeje na hayo mabati yao. Kwa kuwa hawajitokezi naituma kwao nikipata email ya ofisi yao pamoja na TBS
 
Kosavkubwa ulilofanya Ni kutokumshirikishavfundi, inakuaje hadi unalipitia usikague nembo ya TBS, umegundua wakati Fundikaishaanza kazi ya kupaua.
 
Nilitarajia watu wa kiboko waje kutueleza tufanyeje na hayo mabati yao. Kwa kuwa hawajitokezi naituma kwao nikipata email ya ofisi yao pamoja na TBS
bado kupauka mkuu kama ni ya rangi....japokuwa kama huko uliko hakuna bahari basi tayavumilia kidogo
 
Hata mimi ilinitokea..Nilinunua mabati ya G28 kutoka kampuni ya Dragon ya Wachina..cha kushangaza mabati migongo yake hailingani..yaani yanapishana sana kiasi kwamba fundi alipata shida sana kuezeka na mpaka sasa nawaza kutafuta pesa ili niyaondoe niweke mengine. Naomba TBS wawe wanafuatilia sana hivi viwanda ni hasara kubwa sana tunapata kwenye bati za hivi viwanda
 
haya mabati hovyo sana mi mwenyewe niliyatumia yakawa hayakai vizur mpaka nikagombana na fundi, fundi mwingine naye hali ikawa hiyohiyo
 
Sio mabati tu. ...hata "misumari yenyewe inapinda ovyo
 
Kuna jamaa yangu amepaua nyumba cha kushangaza umande tu unavuja anajiuliza masika yakija itakuwaje? Hivi ni viwanda vichache atakavyojenga magufuli kila kona siyatakuwa majanga.
 
ANDO ROOFING ndo kimbilio la leo, wana bati NZURI NA VIGAE AMBAVYO HAVIPAUKI WALA HAVISHIKI KUTU
 
Hayo mabati kama ulinunua kwa viduka vidogo buguruni au mapambano(Veternary) umeliwa.
Aidha buguruni maeneo ya mwembeni na black six ndio kiwanda cha kugonga bati za kichina mihuri na kuziita kiboko au simba dumu.
Ukitaka bati origina za kiboko nenda duka kubwa la FMJ maarufu kama mama wahenga,Kamaka kwa warusi au kiwandani MM steel Mwenge.
Pia ukitaka bati original za simba dumu,nenda kiwandani Alaf tazara au kwa agent wao mkubwa Willy enterpices Tazara.
 
Ukitegemea taasisi za serikali kufanya huo ukaguzi imekula kwako.
 
Hayo mabati kama ulinunua kwa viduka vidogo buguruni au mapambano(Veternary) umeliwa.
Aidha buguruni maeneo ya mwembeni na black six ndio kiwanda cha kugonga bati za kichina mihuri na kuziita kiboko au simba dumu.
Ukitaka bati origina za kiboko nenda duka kubwa la FMJ maarufu kama mama wahenga,Kamaka kwa warusi au kiwandani MM steel Mwenge.
Pia ukitaka bati original za simba dumu,nenda kiwandani Alaf tazara au kwa agent wao mkubwa Willy enterpices Tazara.
Nimejifunza kitu hapa
 
Kuna jamaa yangu amepaua nyumba cha kushangaza umande tu unavuja anajiuliza masika yakija itakuwaje? Hivi ni viwanda vichache atakavyojenga magufuli kila kona siyatakuwa majanga.

Kwa nini unasema Magufuli atajenga viwanda kama hivyo?
 
Back
Top Bottom