Mabasi ya Mwendokasi kuanza kutumia gesi asilia

Gazeti la Habari Leo limeripoti kuwa` msimamizi wa usambazaji gesi katika shirika la maendeleo ya petrol Tanzania (TPDC), Ismail Naleja, amesema awamu ya pili ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam yatatumia nishati ya gesi asilia badala ya mafuta jambo litakalosaidia kupunguza gharama.

Kupitia gazeti hilo Naleja amesema matumizi ya nishati hiyo yataanza katika awamu ya pili ambapo mabasi mapya 200 ya mradi huo yanatarajiwa kuingizwa nchini.

Akizungumza katika maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea kwenye viwanja vya mwalimu Nyerere, kuhusu usambazwaji wa gesi katika magari, Naleja alisema hatua hiyo itaongezeka idadi ya magari yanayotumia gesi nchini ambapo hivi sasa kuna mabasi 60 yanayotumia gesi na kuwashauri wenye magari kutumia mfumo huo ili kupunguza gharama za uendeshaji.

>>>’‘Uendeshaji wa gesi utakua nafuu jambo linaloweza kufanya hata nauli zake kupungua kwani kilo moja ya gesi itatumika katika umbali unaotumiwa na mafuta ya dizeli lita moja na nusu”

Unaweza kuzipitia hapa chini habari nyingine kubwa kwenye magazeti ya July 04 2016
 
Safi sana, uzuri wa JPM mambo yake ni ya uhakika yaani hamna chembe ya ubabaishaji.
 
Tufanye calculation diesel lita1 ni 1600 kwa sasa so 1.5 itakua ni 2400/= je kilo moja ya gesi ni chini ya 2400??? Wataalamu wa gesi asili naombeni muongozo?? Na je usalama wa kati ya gesi na diesel upoje?? Engneers nisaidien.. Naomba kuwasilisha
 
Kabla ya kuhamishia huo unafuu wa gesi kwenye DART, si wangeanza na kupunguza bei ya gesi ya kupikia. Mama zetu wanaumia na moshi wa kuni wajameni. Shusha bei ya gas mpaka ifike 1000/kg nadhani hapo familia nyingi wataswitch kwa gas ambayo kwa mujibu wa viwango, ni more cleaner.
 
Back
Top Bottom