Mabasi ya Mwendokasi kuanza kutumia gesi asilia

Donatila

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Messages
3,092
Likes
4,079
Points
280
Age
28
Donatila

Donatila

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2014
3,092 4,079 280
Msimamizi wa Usambazaji Gesi katika Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Ismail Naleja, amesema awamu ya pili ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam yatatumia nishati ya gesi asilia badala ya mafuta jambo litakalosaidia kupunguza gharama. Katika awamu ya pili, mabasi mapya 200 ya mradi huo yanatarajiwa kuingizwa nchini.

Akizungumza katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, kuhusu usambazwaji wa gesi katika magari, Naleja alisema hatua hiyo itaongeza idadi ya magari yanayotumia gesi nchini ambapo hivi sasa kuna mabasi 60 yanayotumia gesi na kuwashauri wenye magari kutumia mfumo huo ili kupunguza gharama za uendeshaji.

“Uendeshaji wa gesi utakuwa nafuu jambo linaloweza kufanya hata nauli zake kupungua kwani kilo moja ya gesi inatumika katika umbali unaotumiwa na mafuta ya dizeli lita moja na nusu,” alieleza Naleja.

Alisema kilo moja ya gesi ni Sh 1,500 wakati lita moja na nusu ni Sh 3,000, pia gesi haiharibu mazingira kwa sababu haina kaboni ikilinganishwa na petroli.

Aliongeza kuwa, gharama ya ufungaji wa mfumo wa gesi kwenye gari ni Sh milioni mbili, fedha ambayo inarudi baada ya kupunguza gharama katika matumizi kwa miezi mitano tu.

Mtaalamu huyo alisema matumizi ya gesi katika magari si hatari, kwani gesi inayotumika ni nyepesi kuliko inayotumika majumbani, hivyo ikivuja inasambaa hewani na tatizo likitokea mtungi wa gesi unajifunga.

Naye Msemaji wa Kampuni inayoendesha mabasi ya haraka ya UDART, Sabri Mabrouk alisema ni kweli kuwa awamu ya kwanza ya magari yaendayo haraka hayakuweza kutumia gesi kutokana na shirika hilo kuchelewa kupeleka wazo hilo. Hata hivyo sasa wameshafanya mazungumzo ili mradi wa awamu ya pili utumie gesi ili kupunguza gharama.

Alisema wanatarajia awamu ya pili ya mradi utakuwa na mabasi 200.

Chanzo: HabariLeo
 
kisepi

kisepi

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2015
Messages
1,784
Likes
468
Points
180
kisepi

kisepi

JF-Expert Member
Joined Jun 9, 2015
1,784 468 180
ok sawaaaa
 
Copenhagen DN

Copenhagen DN

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2014
Messages
6,071
Likes
8,351
Points
280
Age
29
Copenhagen DN

Copenhagen DN

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2014
6,071 8,351 280
Blah blah nyingii. Billion 600 eti imetumika kwenye mradi huu. Watu wanalaana sana. Endeleen kuiba tutawalipia hayo maden. Iyo gesi wiz mkubwa watu wameshajichukulia chao hamna shida tutawalipia tu maden
 
Bilionea Asigwa

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Messages
16,007
Likes
22,625
Points
280
Bilionea Asigwa

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2011
16,007 22,625 280
Ubunifu mzuri sana huu.

Wakiweza pia waanzishe kwenye magari ya kawaida ya abiria lakini pia kwenye treni na kwenye vivuko vyetu .

Wazo zuri sana hili likifanyiwa utafiti mzuri wa kutosha.
 
mgt software

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
11,166
Likes
2,011
Points
280
mgt software

mgt software

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
11,166 2,011 280
mitambo inauzwa wapi niwahi, kwani kwa sasa sitaki kwenda kituo cha mafuta kuna harufu huwa sizipendi.
 
sblandes

sblandes

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2010
Messages
3,150
Likes
1,314
Points
280
sblandes

sblandes

JF-Expert Member
Joined Apr 25, 2010
3,150 1,314 280
Mbona majibu hayajitosherezi?au ndio kikomo cha ujuzi wa wataalamu wetu wa mabasi mwendo poa,na
Wataalamu wa gesi wa TPDC.Shame on you.
 
kabila01

kabila01

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2009
Messages
3,568
Likes
2,972
Points
280
kabila01

kabila01

JF-Expert Member
Joined Apr 21, 2009
3,568 2,972 280
Wafikirie kwenye treni pia
 
kisepi

kisepi

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2015
Messages
1,784
Likes
468
Points
180
kisepi

kisepi

JF-Expert Member
Joined Jun 9, 2015
1,784 468 180
hapa kazi tu
 
O

ochuado

New Member
Joined
Jul 29, 2015
Messages
2
Likes
0
Points
3
O

ochuado

New Member
Joined Jul 29, 2015
2 0 3
DIT walikuwa na mradi wa kubadili injini za petroli kutumia gesi miaka kadhaa iliyopita.....ulifia wapi? Wadau wa DIT mtujuze.
 
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Messages
44,928
Likes
12,897
Points
280
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined Jun 14, 2011
44,928 12,897 280
Kwanza lile limtungi ni lizito, litaharibu shock up ya gari.

Pili nikiwa nasafiri natakiwa niwe nimebeba gesi ya kutosha ambayo itazidi uzito kwenye gari.

Tatu, huo mradi haujasambaa sehemu kubwa.

Ndo yale ya kupanga foleni kuweka gesi.
 
Lupyeee

Lupyeee

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Messages
2,689
Likes
2,794
Points
280
Age
48
Lupyeee

Lupyeee

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2016
2,689 2,794 280
Hapa kazi tu.

Piga kazi Magufuli mpaka Nyumbu wanyooke
 
NDESSA

NDESSA

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2013
Messages
1,889
Likes
1,568
Points
280
NDESSA

NDESSA

JF-Expert Member
Joined May 2, 2013
1,889 1,568 280
Bongo maneno mengi sana vitendo zero.
 
babu M

babu M

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2010
Messages
4,146
Likes
1,149
Points
280
babu M

babu M

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2010
4,146 1,149 280
Msimamizi wa Usambazaji Gesi katika Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Ismail Naleja, amesema awamu ya pili ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam yatatumia nishati ya gesi asilia badala ya mafuta jambo litakalosaidia kupunguza gharama. Katika awamu ya pili, mabasi mapya 200 ya mradi huo yanatarajiwa kuingizwa nchini.

Akizungumza katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, kuhusu usambazwaji wa gesi katika magari, Naleja alisema hatua hiyo itaongeza idadi ya magari yanayotumia gesi nchini ambapo hivi sasa kuna mabasi 60 yanayotumia gesi na kuwashauri wenye magari kutumia mfumo huo ili kupunguza gharama za uendeshaji.

“Uendeshaji wa gesi utakuwa nafuu jambo linaloweza kufanya hata nauli zake kupungua kwani kilo moja ya gesi inatumika katika umbali unaotumiwa na mafuta ya dizeli lita moja na nusu,” alieleza Naleja.

Alisema kilo moja ya gesi ni Sh 1,500 wakati lita moja na nusu ni Sh 3,000, pia gesi haiharibu mazingira kwa sababu haina kaboni ikilinganishwa na petroli.

Aliongeza kuwa, gharama ya ufungaji wa mfumo wa gesi kwenye gari ni Sh milioni mbili, fedha ambayo inarudi baada ya kupunguza gharama katika matumizi kwa miezi mitano tu.

Mtaalamu huyo alisema matumizi ya gesi katika magari si hatari, kwani gesi inayotumika ni nyepesi kuliko inayotumika majumbani, hivyo ikivuja inasambaa hewani na tatizo likitokea mtungi wa gesi unajifunga.

Naye Msemaji wa Kampuni inayoendesha mabasi ya haraka ya UDART, Sabri Mabrouk alisema ni kweli kuwa awamu ya kwanza ya magari yaendayo haraka hayakuweza kutumia gesi kutokana na shirika hilo kuchelewa kupeleka wazo hilo. Hata hivyo sasa wameshafanya mazungumzo ili mradi wa awamu ya pili utumie gesi ili kupunguza gharama.

Alisema wanatarajia awamu ya pili ya mradi utakuwa na mabasi 200.

Chanzo: HabariLeo
Inaenda umbali gani:
-Lita moja ya petroli?
-Kilo moja ya gasi?
 
Kinyozi wetu

Kinyozi wetu

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Messages
326
Likes
52
Points
45
Kinyozi wetu

Kinyozi wetu

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2014
326 52 45
Blah blah nyingii. Billion 600 eti imetumika kwenye mradi huu. Watu wanalaana sana. Endeleen kuiba tutawalipia hayo maden. Iyo gesi wiz mkubwa watu wameshajichukulia chao hamna shida tutawalipia tu maden
kila kitu ni mwendokasi mpaka fikra zao.
 
K

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Messages
1,056
Likes
1,064
Points
280
K

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined May 27, 2016
1,056 1,064 280
MSIMAMIZI wa Usambazaji Gesi katika Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Ismail Naleja, amesema awamu ya pili ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam yatatumia nishati ya gesi asilia badala ya mafuta jambo litakalosaidia kupunguza gharama. Katika awamu ya pili, mabasi mapya 200 ya mradi huo yanatarajiwa kuingizwa nchini.

Akizungumza katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, kuhusu usambazwaji wa gesi katika magari, Naleja alisema hatua hiyo itaongeza idadi ya magari yanayotumia gesi nchini ambapo hivi sasa kuna mabasi 60 yanayotumia gesi na kuwashauri wenye magari kutumia mfumo huo ili kupunguza gharama za uendeshaji.

“Uendeshaji wa gesi utakuwa nafuu jambo linaloweza kufanya hata nauli zake kupungua kwani kilo moja ya gesi inatumika katika umbali unaotumiwa na mafuta ya dizeli lita moja na nusu,” alieleza Naleja.

Alisema kilo moja ya gesi ni Sh 1,500 wakati lita moja na nusu ni Sh 3,000, pia gesi haiharibu mazingira kwa sababu haina kaboni ikilinganishwa na petroli.

Aliongeza kuwa, gharama ya ufungaji wa mfumo wa gesi kwenye gari ni Sh milioni mbili, fedha ambayo inarudi baada ya kupunguza gharama katika matumizi kwa miezi mitano tu.

Mtaalamu huyo alisema matumizi ya gesi katika magari si hatari, kwani gesi inayotumika ni nyepesi kuliko inayotumika majumbani, hivyo ikivuja inasambaa hewani na tatizo likitokea mtungi wa gesi unajifunga.

Naye Msemaji wa Kampuni inayoendesha mabasi ya haraka ya UDART, Sabri Mabrouk alisema ni kweli kuwa awamu ya kwanza ya magari yaendayo haraka hayakuweza kutumia gesi kutokana na shirika hilo kuchelewa kupeleka wazo hilo. Hata hivyo sasa wameshafanya mazungumzo ili mradi wa awamu ya pili utumie gesi ili kupunguza gharama.

Alisema wanatarajia awamu ya pili ya mradi utakuwa na mabasi 200.
 
Kinyozi wetu

Kinyozi wetu

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Messages
326
Likes
52
Points
45
Kinyozi wetu

Kinyozi wetu

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2014
326 52 45
MSIMAMIZI wa Usambazaji Gesi katika Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Ismail Naleja, amesema awamu ya pili ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam yatatumia nishati ya gesi asilia badala ya mafuta jambo litakalosaidia kupunguza gharama. Katika awamu ya pili, mabasi mapya 200 ya mradi huo yanatarajiwa kuingizwa nchini.

Akizungumza katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, kuhusu usambazwaji wa gesi katika magari, Naleja alisema hatua hiyo itaongeza idadi ya magari yanayotumia gesi nchini ambapo hivi sasa kuna mabasi 60 yanayotumia gesi na kuwashauri wenye magari kutumia mfumo huo ili kupunguza gharama za uendeshaji.

“Uendeshaji wa gesi utakuwa nafuu jambo linaloweza kufanya hata nauli zake kupungua kwani kilo moja ya gesi inatumika katika umbali unaotumiwa na mafuta ya dizeli lita moja na nusu,” alieleza Naleja.

Alisema kilo moja ya gesi ni Sh 1,500 wakati lita moja na nusu ni Sh 3,000, pia gesi haiharibu mazingira kwa sababu haina kaboni ikilinganishwa na petroli.

Aliongeza kuwa, gharama ya ufungaji wa mfumo wa gesi kwenye gari ni Sh milioni mbili, fedha ambayo inarudi baada ya kupunguza gharama katika matumizi kwa miezi mitano tu.

Mtaalamu huyo alisema matumizi ya gesi katika magari si hatari, kwani gesi inayotumika ni nyepesi kuliko inayotumika majumbani, hivyo ikivuja inasambaa hewani na tatizo likitokea mtungi wa gesi unajifunga.

Naye Msemaji wa Kampuni inayoendesha mabasi ya haraka ya UDART, Sabri Mabrouk alisema ni kweli kuwa awamu ya kwanza ya magari yaendayo haraka hayakuweza kutumia gesi kutokana na shirika hilo kuchelewa kupeleka wazo hilo. Hata hivyo sasa wameshafanya mazungumzo ili mradi wa awamu ya pili utumie gesi ili kupunguza gharama.

Alisema wanatarajia awamu ya pili ya mradi utakuwa na mabasi 200.
Hekaya za abunuasi.. tushasikia vingi na tunazid kuona vingi.
 
Forum statistics

Threads 1,238,662
Members 476,083
Posts 29,325,912