kyagata
JF-Expert Member
- Oct 18, 2016
- 6,576
- 12,689
We mgeni wa dar nin,mbona njia ya goba iko poa tu kukufikisha hapo stend ya Magufuli?Ukweli ni kwamba ile stand ipo sehemu mbaya sana!
Hivi unategemea magari yanayotoka huko Kaskazini yanayopita barabara ya Bagamoyo yaje yarudi Mbezi kweli? Yatapitia njia ipi itakayoyarudisha Mbezi Stand kama yatakuwa yamepitia Bagamoyo?
Hakuna gari inayoweza kupitia Bagamoyo ifike mwenge iende Ubungo kisha ianze kuitafuta Mbezi!
Inachotakiwa ni dereva na kondakta amwambie abiria kabla hajapanda gari inapitia Bagamoyo na haitapitia Magufuli stand, hivyo abiria abaki na uamuzi wa kupanda then achague sehemu nyingine safe kwake kushuka au apande gari zinazopita Chalinze!
Tatizo abiria nao ni wabishi, anaambiwa hii gari inapita Bagamoyo na anataka kushuka mbezi anang'ang'ania tu gari ikifika mwisho wa safari anaanza kutukana dereva!
Kingine labda ugeni wa abiria, ambapo wengi wakielezwa wanaelewa!