JT2014
JF-Expert Member
- Jan 18, 2014
- 1,863
- 1,367
Niwapongeze wanajf wote kwa kuingia mwaka mpya 2018. Pia niwape pole/hongera na kazi za kulijenga taifa.
Niende moja kwa moja kwenye hoja yangu iliyonisukuma kuanzisha uzi huu. Katika safari zangu za mapumziko ya sikukuu za Christmas na mwaka mpya,nilisafiri katika mojawapo ya mabasi ya kwenda mikoani(kanda ya ziwa)
Nilishangazwa sana na wahudumu wa mabasi hayo. kumwaga takataka wanazozikusanya kwenye mabasi kutoka kwa wateja wao wanaosafiri mfano,mabox ya biscuit chupa za soda/maji n.k. wakisimama porini kwa lengo la watu kuchimba dawa wanamwaga taka taka hizo kwenye mapori na hivyo kupoteza maana ya kuweka vikapu hivyo kwenye mabasi ambapo lengo lilikuwa kuzuia abiria kutupa taka ovyo njiani.
Rai yangu kwa mamalaka husika ni kuweka udhibiti wa tabia hii, ili kuhakikisha mabasi yana mifuko ya kutunzia taka taka kwenye buti za magari yao mpaka mwisho wa safari au mpaka sehemu sahii yenye kuhusika na takataka hizo ili kuepuka uharibifu wa mazingira kwa kiasi kikubwa.
Karibu kama una wazo mbadala au la ziada ili kuhakikisha hali ya mazingira inatunzwa.