Mabaraza ya Mawaziri

Ghost Worker

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
1,229
2,000
Juzi kwenye maadhimisho ya siku ya sheria, Mh. Rais pamoja na mambo mengine alizungumzia matatizo ya Mabaraza ya Ardhi na Nyumba (ya Wilaya) na baadaye akatoa rai kwa Jaji Mkuu kutazama namna ambayo Mahakama inaweza kusimamia Mabaraza haya ili kukabiliana na malalamiko ya migogoro ya ardhi.

Kwanza hata kabla hatujanyoosheana vidole vya lawama, hatua ya Mh. Rais japo kuzungumza jambo kuzihusu mahakama hizi za ardhi na kukiri sehemu ya matatizo yake ni jambo la kupongezwa kiukweli, maana licha ya maudhui ya mwaka huu wa sheria kujikita kwenye dhima ya Mahakama na wadau katika kuweka mazingira wezeshi kwa biashara na uwekezaji, hakuna hata hotuba moja iliyojaribu kuyamulika japo kidogo mabaraza/mahakama hizi kwa upekee. ARDHI ni miongoni mwa rasilimali muhimu na miongoni mwa misingi muhimu kabisa ya uchumi, hivyo ni nyenzo muhimu kabisa ya biashara na huo uwekezaji unaoguswa na maudhui ya mwaka huu wa sheria.

Ukiacha matatizo mengine kama tuhuma za rushwa (ambayo kimsingi ni tatizo la kila sekta) ni kweli kuwa pana MATATIZO MAKUBWA kwa mabaraza ya ardhi ambayo yanahitaji suluhu ya HARAKA na ya kipekee kwa maslahi mapana ya haki na usawa.

MABARAZA YA WILAYA

Licha ya kwamba hayana rasilimali watu ya kutosha mabaraza haya yapo kwenye wilaya CHACHE SANA hali inayosababisha yasifikiwe kwa urahisi na wananchi walio wengi. Katika maeneo mengi kunakuwa na mwamuzi (Mwenyekiti) mmoja ambaye anahudumia wilaya kadhaa na wakati mwingine Mwenyekiti mmoja anahudumia hadi mkoa mzima! Hapa hatuwezi kutegemea ufanisi katika hali kama hii, hasa ukizingatia ardhi ni miongoni mwa maeneo yanayozalisha migogoro mingi sana inayohitaji utatuzi wa kisheria wa haraka.

Urasimu katika masuala ya rasilimali watu kwa Mabaraza haya ambayo yapo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ni sababu nyingine inayopelekea kulegalega kwa ufanisi wa mabaraza haya. Kwa mfano inapotokea mtumishi (hasa wenyeviti) kutokuwepo kazini kwa sababu kama za kuachishwa, kusimamishwa, kuhama n.k mchakato wa kumpata mwingine huweza kuchukua hata miaka miwili! Yapo maeneo kuna kesi hadi za mwaka 2017 bado hazijatolewa maamuzi kutokana na sababu kama hizi.

Yapo pia mabaraza ambayo yana waamuzi lakini hayawezi kutekeleza majukumu yake kutokana na kukosekana kwa washauri (Assessors) na hali hiyo inaweza kuchukua miezi kadhaa. Hii inatokea pale washauri hawa wanapomaliza mikataba yao. Ni takwa la kisheria kwa mabaraza ya Wilaya kuwa ni lazima yawe na washauri, lakini ni jambo lenye kuleta ukakasi kwamba kukosekana tu kwa wshauri iwe sababu za kuchelewesha haki za watu kwa miezi mingi tu ilhali upatikanaji wa washauri hawa una mchakato rahisi kabisa!

MABARAZA YA KATA
Haya ni kirusi cha CORONA katika suala zima la haki-ardhi na chanzo kikuu cha maumivu kwa wengi ambao wamebaki hawana namna ya kufanya. Mabaraza haya nayo pamoja na mambo mengine hushughulika na masuala ya ardhi. Kuna wakati Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaama aliwahi kutamka kuyafutilia mbali mabaraza haya ndani ya Mkoa huo kutokana na madudu yanayoendelea huko. Japo amri yake ilizua sintofahamu na kuibua maswali kadhaa (sikumbuki liliishia wapi) lakini ile ilipaswa kuwa chachu ya kujitafakari na kurekebisha kasoro zilizopo.

Kinachoshuhudiwa kwenye mabaraza ya kata ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni na taratibu na maamuzi ya ajabu kabisa yanayoishia kuziweka rehani haki za wadaawa kanuni kuu huko ikiwa ni MWENYE NGUVU MPISHE. Kutokana na uchache/umbali pamoja na mapungufu mengine ya mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya ambayo ndio yana mamlaka ya rufaa juu ya mabaraza ya kata, wengi wa wadaawa wanaonyimwa haki zao na mabaraza ya kata wamekuwa wakishindwa kuyakatia rufaa maamuzi ya mabaraza ya kata na kuhiyari kuzipoteza haki zao au kujichukulia sheria mikononi.

Kwa baadhi ya maeneo madiwani wamekuwa wakiamini kabisa kuwa mabaraza hayo yanaanguka chini ya mamlaka yao (Kutokana na kuitwa mabaraza ya KATA) na hivyo kujipa mamlaka makubwa katika kuingilia mienendo na maamuzi ya mabaraza ya kata kwa maslahi yao binafsi na ya kisiasa. Hili likijumlishwa na uduni wa elimu ya wajumbe wa mabaraza haya linasababisha hali ya mabaraza haya kuwa mbaya zaidi.

MAPENDEKEZO
Mamlaka zinazohusika zione kuwa sasa ni wakati wa mabaraza ya ardhi ya wilaya kufutwa na mamlaka yake kurejeshwa kwenye mahakama za wilaya kwa ajili ya kuhakikisha ufanisi wake hasa ikizingatiwa huduma ya mahakama za wilaya angalau zimesogea jirani zaidi na wananchi ambapo kuna mahakama karibu kila wilaya nchini.

Mabaraza ya kata yaondolewe kabisa mamlaka ya kushughulikia mashauri ya ardhi na mamlaka hiyo ipelekwe kwa mahakama za mwanzo na ikionekana kuwa na lazima mabaraza hayo yaendelee na jukumu hilo basi yatekeleze jukumu hilo kwa uangalizi wa mahakama za mwanzo kama ambavyo zinasimamia mashauri ya aina zingine katika mabaraza hayo.
 
Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
4,749
2,000
Yani hawa jamaa ni mbadala wa mahakama katika mashauri ya ardhi lakini namna wanavyofanya kazi wanajua wenyewe.

Yani miongoni mwa kero kubwa ni ucheleweshaji wa maamuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
permanides

JF-Expert Member
May 18, 2013
3,994

Hariri kichwa cha habari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom