Mabadiliko yatamwongezea madaraka DPP

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
WABUNGE kadhaa wameonyesha wasiwasi wao kuhusu utaratibu wa kutenganisha shughuli za uendeshaji mashitaka na kazi ya upelelezi wa kesi. Wamebainisha kuwa ingawa utaratibu huo ni mzuri, lakini unamwongezea madaraka Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).

Walieleza wasiwasi huo jana wakati wakichangia katika muswada wa sheria ya Mfumo wa Mashitaka nchini wa mwaka 2007, uliowasilishwa kwa mara ya pili bungeni jana na Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Mary Nagu.
Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM), alisema ana hofu na madaraka makubwa anayopewa DPP kupitia sheria hiyo mpya kwa vile DPP "naye pia ni binadamu na anaweza kutumia vibaya madaraka hayo."

Katika mchango wake, Dk. Mwakyembe alieleza wazi kuwa haipongezi serikali kwa kuleta muswada huo kwa sababu umechelewa mno.

Alisema mapendekezo ya kutenganisha shughuli za upelelezi na uendeshaji mashitaka lilitolewa kwa mara ya kwanza miaka 31 iliyopita na iliyokuwa Tume ya Msekwa.

"Mapendekezo ya awali ya kufanya marekebisho haya yalitolewa na Tume ya Msekwa. Yanapotokea mabadiliko miaka 31 baadaye sina sababu ya kupongeza," alisema Dk. Mwakyembe.

Akitetea uamuzi wake wa kutoipongeza serikali, Dk. Mwakyembe alisema madhara ya polisi kuachiwa kufanya kazi zote zinazohusiana na makosa limewaumiza watu wengi kwa muda mrefu na halikupaswa kuachwa liendelee.

Alisema inaweza kulikuwa na wataalamu wachache kuijenga idara ya uendeshaji mashitaka kuwa inayojitegemea na suala hilo liangaliwe, kwani hata sasa bado wataalamu ni wachache.

Alipendekeza kuwa maofisa wa Jeshi la Polisi waliokuwa wakifanya kazi ya kuendesha mashitaka wana uzoefu unaotakiwa, kwa hiyo washawishiwe kujiunga na ofisi ya DPP ili kuiimaisha zaidi.

Alisema mabadiliko yanayofanywa kupitia muswada huo yanaweza yasiwe na maana kama hayatafanyika marekebisho yatakayolenga kuboresha maslahi ya maofisa wanaoshughulika katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hasa mawakili wa serikali.

Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Charles Keenja (CCM), alisema mfumo uliopo hivi sasa unamwonea mnyonge na ushahidi wa hilo unaonekana katika hali halisi pale watu wenye fedha kutokukaa mahabusu.

Alisema pamoja na kuanzisha utaratibu wa kutenganisha shughuli za upelelezi na uendeshaji mashitaka hivi sasa, lakini baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo, DPP aangalie pia kesi nyingine zote zilizopo, kwani kuna watu 'waliosota' mahabusu kwa miaka mingi wakishitakiwa kwa makosa wasiyotenda.

Akichangia muswada huo, Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP), alisema tatizo la mrundikano wa mahabusu litaendelea kwa sababu wakati DPP atakuwa anadhamiria kupunguza idadi ya kesi zisizo za msingi, polisi nao watakuwa wanaendelea kuwakamata watu na kuwaweka rumande hata kama hawana makosa yanayostahili kuwekwa rumande.

"Watu wa BoT hawajakamatwa, tunasema tusubiri upelelezi kwanza, sawa, lakini kama inawezekana kwa hawa wa juu, kwa nini iwezekane pia kwa watu wanyonge?" alihoji.

Awali, akiwasilisha muswada huo, Dk. Nagu alibainisha kuwa pamoja na mambo mengine, sheria inalenga kutenganisha upelelezi na uendeshaji mashitaka.

"Polisi na taasisi nyingine kama PCCB, TRA na kadhalika watashughulika na upelelezi huku Mkurugenzi wa Mashitaka akishughulikia uendeshaji wa mashitaka. Huu utakuwa ni utekelezaji thabiti wa utawala bora," alisema.

Alisema kutakuwa na utaratibu mpya wa kisheria wa kuendesha mashitaka kwa lengo la kuharakisha upatikanaji wa haki wakati mashitaka ya jinai - isipokuwa machache yaliyo mepesi - yatafunguliwa na DPP ili kuondoa dhana ya ubambikizaji wa kesi.

Muswada huo ulipitishwa jana jioni na utaanza kutumika kwa majiribio katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Tanga, Mwanza, Ruvuma na Shinyanga.
 
Aliyoyasema Mh. Cheyo ni makubwa haya,tuyaangalie kwa undani,siyo mzaha,kwani ni moja kati ya vitu vinavyotutia Watz hasira sana
 
Ndiyo maana tangia jana nasema kwa mwendo huu issue ya BOT imesha kufa maana hadi wamalize upelelezi la sivyo hakuna wa kukamatwa . Wamepeleka miezi 6 makusudi wakijua hii sheria itakuwa in place na wanapeta .
 
Tatizo sio kubadilishwa kwa sheria,tatizo ni Je tatizo la kuingiza siasa katika Haki litawezekana?
 
Back
Top Bottom