Mabadiliko Ya Ulinzi kwenye Mitandao jamii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabadiliko Ya Ulinzi kwenye Mitandao jamii

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Oct 6, 2010.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Oct 6, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kwa wale wapenzi wa Mitandao Kama Facebook na Hi5 kwa siku za karibuni
  watakuwa wameona mabadiliko Fulani kwenye hatua za kuingia kwenye
  account zao haswa wakiwa maeneo mapya .

  Mfano mimi nilipokuwa safari nilipata wakati mgumu sana kuweza kuingia
  kwenye mtandao wangu wa facebook kwa ajili ya kujadili taarifa Fulani
  kwa sababu mtandao huo uligundua ninataka kufungua account toka eneo
  ambalo sijazoeleka nikatakiwa kujibu maswali kama 5 hivi ili
  kudhibitisha anuani yangu hiyo

  Ilikuwa bahati mbaya sana nilitakiwa kuchagua picha za marafiki zangu
  4 tatizo ni kwamba rafiki zangu hao walitumia picha ambazo sio zao
  lakini majina ni halisi nikapata wakati mgumu kuweza kupata maswali
  hayo kutokana na mvurugano wa picha ambazo sio za kweli .

  Hili ni tukio moja kati ya mengi ambayo kwa siku za karibuni
  yanabadilisha kabisa mtindao wa wizi na aina nyingi za kuhalifu ambazo
  wahalafu wengi haswa wale wa nchi maskini walizoea kuiba au kujaribu
  kuingilia account za watu kwa kutumia njia za kuotea password au hata
  kujibu maswali mengine kwa usahihi .

  Hiyo ni hatua kubwa sana kwa mtandao wa facebook , ukija kwenye
  mitandao kama google nayo imebadilisha kidogo sheria zake na taratibu
  zake zinazohusu masuala binafsi ya watu nayo inaelekea huko kama
  facebook lakini google wanaenda mbali zaidi wanataka wateja wao walio
  sehemu mbalimbali duniani waweze kutumia simu zao za mikono kuweza
  kutumia bidhaa Fulani kwa bei nafuu kwa njia ya mtandao hata kununua
  na kufanya aina nyingine za burudani .

  Mfano unapotumia mtandao wa google unaweza kujiunganisha na mitandao
  mingine kutumia huduma zao kadhaa kama zile za blogu , wana zile simu
  zao , wana huduma kama google earth , huduma za kutafuta vitu na
  kufanya vitu kwa njia ya mtandao na vyote hivi vinaweza kufanyika
  ukiwa na simu ya mkononi tu .

  Ndio maana ukienda baadhi ya maeneo jijini dare s salaam kuna vijana
  wengi wenye simu hizi nyingi zinaibiwa afrika kusini na kuja kuuzwa
  hapa nchini na wahalifu , mafundi na wadau wengine wanawasaidia kufuta
  baadhi ya vitu ili waweze kupata access kuweza kutumia huduma kadhaa
  za simu hizo lakini wengi huwa wanajisau kwamba simu hizo zinaweza
  kufuatiliwa zinaweza kujulikana pale zilipo na kuonekana zinafanya
  nini kutokana na hizo huduma zake zingine hata kama kukifanyika
  majaribio ya kufuta .

  Simu hizo zimekamatisha wengi mjini hapa na wengi wamejuta kwanini
  waliamua kununua simu hizo kwa njia za magendo na kuamua kufuta baadhi
  ya vitu kwenye simu ili ziweze kufanya kazi hata wewe kama una simu
  ambayo una mashaka nayo tafadhali toa taarifa ili maafa yasije
  kukukuta wewe kwa sababu njia ni rahisi sana .
  Lakini aina za technologia hizo sio za kujivunia sana sometimes kwa
  sababu niliona moja ina email address moja , kijana Yule akajaribu
  kubadilisha password ya email ili aweze kutumia simu hiyo sijui
  aliishia wapi ina maana kama alikuwa na uwezo wa kubadilisha pwd ya
  email angeweza kuingia kwenye huduma zingine za simu hizo na hata
  kuhamisha taarifa muhimu za mwenye simu .

  Hili ni funzo kwa wale wanaopenda kutegemea simu zao kuhifadhi kila
  kitu na haswa kutumia anuani pepe zao kama alama zao kuu katikaulinzi
  wa vifaa vyao hivyo
  Naomba niishie hapa
   
 2. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Asante kwa maelezo mazuri
   
Loading...