Mabadiliko ya UKAWA 2015 na ya Rais Magufuli yapi ya kweli?

Mabadiliko ya UKAWA 2015 na ya Rais Magufuli yapi ya kweli?

simon mato

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2015
Posts
926
Reaction score
485
Ndugu wanajamvi;

Dhana ya mabadiliko ni ndefu sanaa naomba watanzania tuilewe hili, katika safari ya mabadiliko kuna watu tunawapoteza ( wanakufa ) safarini kwenye hii vita, kuna watu wanaumia, kuna watu wanapoteza mali zao kupigania mabadiliko ya kweli na kuna wengine ukimbia mabadiliko kutokana na kutofautiana mtazamo au itikadi.

Tuliowapoteza kwenye safari wapo mfano; Mchungaji MTIKILA na Deo Filikunjombe hawa walikuwa mashujaa kweli kweli ila mwisho wa siku lazima mapambano yaishe na mshindi wa vita lazima apitakane na maisha lazima yaendelee.

Nadharia ya mabadiliko waliokuwa wanahubiri UKAWA 2015 ukiangalia kwa mapana yake naona ni bora mabadiliko ya sasa kuliko ya UKAWA 2015. Wanazuoni wengi mtajiuliza ni kwanini niseme hivi ? Lakini naombeni niwajibu hivi!

* Wasiwasi wangu wa mtandao wa Edward lowasa mgombea urais kupitia UKAWA; Ni lazima mda mwingine turudi nyuma tuache itikadi zetu kwa maono mapana, huyu bwana EL ki uhalisia alikuwa na kundi au genge ambalo lilikuwa linamfuata nyuma yake. Na hili kundi hili ilibeba watu wa kada mbalimbali.

Walikuepo wafanyabiashara maarufu, Viongozi wa dini, wanasiasa na wanaharakati mbalimbali. Napatwa na ukakasi mkubwa kuwa endapo huyu El angeshinda urais hawa watu angewalipa nini? Kama ni hela isingewatosha na kama ni Ng' ombe wake wasingetosha na kama ni nyumba zake zisingetosha!

Kwa mantiki hii ni lazima tukae chini tufikirie, na hapa ndipo yatupasa tuwe wakweli Mimi na wewe! Ila kwangu jibu ni rahisi sanaa in short ni " FADHILA" tuuh ndo ingewatosha hawa watu! Lakini ni fadhila ya aina gani? Kwangu Mimi hii fadhila ingetokana na wewe upo kwenye kada ipi.

Na hapa ndipo tunapatwa na wasiwasi kubwa kuwa marafiki wake wale wafanyabiashara wakubwa aliokuwa akiwasema kuwa wanamsaidia je wangelipa kodi? Maana hakuna msaada juu ya hapo

Pia napatwa na ukakasi mkubwa je Balozi Mwapachu angenyimwa uwaziri wa mambo ya nje akapewa mch. MSIGWA? Au je Laurence Masha angenyimwa uwaziri wa mambo ya ndani akapewa Godbless Lema? Jibu ni raisi sanaaa haiwezekani ata kidogo umpe mgeni eneo kubwa la shamba wakati kuna wenyeji ambao mnajuana vizuri.

* Suala la uadilifu* hii pia ni nadharia sahihi hasa ukizingatia hii nchi yetu ilipofikia, kama kiongozi wa familia huwezi kukemea bila kumung'unya maneno juu ya mtoto wako kukoswa uadilifu, ni lazima kwanza kama kiongozi wa familia uwe muadilifu ndipo na wewe unakuwa na Uhuru na ujasiri wa kukemea jambo linaloenda mrama na familia yenu.

Vivyo hivyo kama Kiongozi mkuu wa nchi yakufaaa uwe muadilifu ndipo unapata sauti ya kukemea kwa ujasiri bila kumung'unya maneno. Lakini kwa Bahati mbaya mgombea wa UKAWA ni majeruhi wa tuhuma mbalimbali katika safari yake ya maisha ya kiutawala, Tena tuhuma nzito nzito zilizowahi kukumba Taifa hili.

Kwa Bahati mbaya hajawahi kukana hadharani kwa ushaidi zaidi ya kusema anaonewa. Nilimsubiri kwa hamu na bashasha 2015 kuwataja majina ya waliohusika kwenye kashfa ya "RICHMOND" iliomng'oa 2008 madarakani kwa sababu alisema alifedheshwa na kuonewa na huu ndio ulikua mda sahihi wa kutoa fedheha na aibu yote lakiniyangekZaidi ya kumsikia propaganda za lisu kwenye majukwa akitetea jambo ambalo lilihatarisha hadi maisha yake.

Wengine wametoka hadi hadharani kusema wana ushaidi juu ya kashfa zake, sasa napatwa na wasiwasi mkubwa mno ebu tuchukulie huu msemo " Fisi kufunguliwa mlango wanapolala Kondoo usiku halafu umuache" athari yake uonekana tena mkubwa mno, kwa mtazamo wangu UKAWA wangeshinda 2015 suala la ufisadi lingekuwa cancer la taifa kutokana na kiongozi wa juu kutokuwa muadilifu.

* shaauku ya kuingia ikulu nayo ilichukua ukurasa mpya* yalisemwa mengi sanaaa kipindi cha kampeni na UKAWA kupitia mgombea wao EL mfano; kusoma bure mpaka chuo kikuu, waliokopeshwa na bodi kusamehewa, sijui ndani ya siku mia moja nini, mara serikali yangu itakuwa na speed ya ajabu.

Lakini ata siku moja mhe. EL hajawahi kusema atafanyajefanyaje watoto wasome bure mpaka chuo kikuu jambo ambalo limewashinda ata Kenya jirani yetu licha ya kuwa na uchumi Mzuri. Kwahyo kizazi cha kuhoji tunapatwa na ukakasi mkubwa mno kutokana na zile kauli tata sawa sawa na " Majibu mepesi kwenye masuala magumu ".

Lakini ukikaa chini ukitafakari kwa kina unakuta mhe.EL alikuwa na tamaa au shauku ya kuingia ikulu kuliko kuwatumikia wananchi na akaenda tena kwenye genge la majeruhi waliokuwa wanaisaka ikulu kama Fisi ambaye hajala siku saba mfululizo yuko radhi amue ata binadamu mchana kweupe ilimradi apate chakula, ndiyo maana zilitumika kila aina ya hujuma kuhakikisha wanaingia ikula ila nyuma ya pazia walikuwa mafisi wanaowatafuta kondoo mtaani.


* Ujenzi wa taasisi na chama* wangeshinda hawa UKAWA 2015 Nina uhakika maisha yangekuwa magumu mno kuliko sasa, kwa sababu ingewabidi wajipange na kujijenga kwanzia kwenye ngazi ya chini hadi juu ki utawala na ki uongozi. Pengine ofisi za chama zingeboreshwa au kujenga upya kwa fedha za umma.

Ingewabidi wabadilishe aina ya watawala kama wakuu wa mikoa, wilaya na kadhalika lakini hao wote najua wengi wao ni mafisi ambao hawajala siku saba halafu wakawekewa kondoo msituni fikiria hatima yake. Ni Mara ngapi tumeskia madiwani wa CHADEMA wanasweka rumande kwa ubadhifu! Na huyo ni diwani tuu je wakuu wa mikoa au wilaya ingekuaje? Ndipo utajua kuwa UKAWA wana uso wa kondoo ili ngozi zao za chui.

:Kwanini nina imani na MAGUFULI kwenye mabadiliko ya kweli Tz;


1. Alikuwa hana mtandao hana wa kumpa fadhila
2. Ni muadilifu na mchapakazi
3. Hana shauku ya Ikulu kama aliyekuwa mgombea wa UKAWA 2015
4. Hana mda wa kupoteza kwenye ujenzi wa chama kwa sababu kaikuta kipo imara.


Safari ya kuelekea uchumi wa kati bado inaendelea;

Ni wako kijana mtiifu, mzalendo na mwanaharakati wa kweli Tanzania.

SIMON MATO:
 
Back
Top Bottom