Mabadiliko ya thamani ya pesa . . .

Afrika Furaha

JF-Expert Member
Dec 16, 2010
329
9
Wana JF . . . naamini humu kuna wachumi waliobobea. Nataka nifahamu, mfano Tanzanian Shillings ipande thaman mpaka kufikia dola moja ya kimarekani, 1 US $ inabadilishwa kwa Tsh 4. Hivyo mwenye Tsh Million 8 atakuwa ana US$ Million 2 ambazo ni pesa nyingi sana. Hivyo mtu mwenye Million 12 tu za bongo ana uwezo wa kuagiza V8 za US$ 180,000 kila moja hata 10. Na vitu vingi vya thamani vitaonekana kama BURE. Je hali hii itaruhusiwa kweli bila kuweka expire date kwa noti zilizopo ili zisitumike? Na kama itakuwa hivyo, vipi kwa mtu ambaye ana pesa benki, kiwango chake cha pesa kitakatwa au? Sijui nimeeleweka??
 
Kidogo Mkuu, hapa bado hujaeleweka.
Tatizo hapa ni nini? Au shilingi inavyoweza kupanda na kushuka thamani?, ulikuwa na maana gani fedha ndani ya bank ( a/c ) na iliyopo nje ya Bank kithamani?.
 
mimi ninavyojua ni kwamba, nchi nyingi wanachukulia kama US$ ndo reference yao! kuna rafiki yangu anafanya kazi ubalozi hapa bongo. wao wanalipwa kwa $. lets say analipwa $ 5000 kwa mwezi. basi kila akienda kubadili benki anapata mara pesa pungufu ya kitanzania na mara nyingine anapata zaidi :)
 
Thamani ya noti mpya na noti ya zamani ni sawa tu mkuu!! Noti ya zamani kuwa kwenye mzunguko na noti mpya hakubadili thamani ya noti hizo ; thamani ya sarafu ya nchi inategemea sana na nguvu ya uchumi wa nchi husika. Kama tutakuwa na bidhaa nyingi zinazohitajika nchi za nje ,watu watahitaji fedha zetu kwa wingi ili wanunue hizo bidhaa kwahiyo thamani ya fedha zetu[ noti] itapanda ukilinganisha na hao tunaofanya nao biashara. Ili madafu yawe na thamani lazima uchumi wetu UGANGAMALE!!
 
ili shilingi ipande ni lazima ku export zaidi kuliko ku import. Lakini US$ 1 = TZ Sh 4 ni ndoto ya mchana!!
 
nakubaliana na wachumi wenzangu kuwa ili thani ya pesa yako ipande hutegemeana na uhitaji wa pesa yako na nchi nyingine ambapo mara nyingi hutokana na export unazofanya.
 
Back
Top Bottom