Mabadiliko ya tabia na shule za kisasa/kidini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabadiliko ya tabia na shule za kisasa/kidini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by anti-fisadi, Oct 22, 2011.

 1. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Imekuwa ni tabia ya wazazi wengi kupima viwango vya shule kwa kuangalia matokeo ya mitihani ya mwisho au wengine kuangalia mtoto mmoja mmoja wanaokutana nao na basi kufikia uamuzi wa kuwahamishia au kuwaanzishia elimu yao kama ni vidudu au msingi huko.

  Ni wachache sana wanaofanya utafiti wa kina,kuangalia njia zinazotumiwa kuwafanya watoto wafikie hapo au pia kufuatilia na kujua tabia mbalimbali zinazojitokeza shuleni hapo kutoka kwa wazazi kadhaa. Unakuta wazazi wakijibidiisha kuwatafutia watoto wao shule wanazodhani ni bora bila kujua undani wa hizo shule,kiasi kwamba hata wazazi wengine hudiriki mpaka kulia watoto wao wakikosa!

  Nilipata mshtuko pale niliposikia shule kadhaa za kidini zikiripotiwa na matukio ya kudhalilisha watoto na baadhi ya wazazi na walimu wakijua hilo na kuliacha liendelee bila kuchukua hatua sahihi. Moja ya shule hio ipo mbezi beach karibu na st.Gaspers church. Inaripotiwa kuwa watoto kadhaa wameshadhalilishwa kijinsia wakike kwa wakiume lakini bado siri inaendelea na wakati huohuo watoto wakiendelea kuharibika.

  Hivi tutakuwa na taifa la kesho la aina gani,kama upuuzi kama huu ukiendelea kukua na kufichwa? Tukiangalia upande mwingine,chanzo cha tatizo sio watoto bali wazazi wanaopuuzia malezi bora ya watoto wao,wengine wakizani malezi ni kazi ya dada wa nyumbani. Mtoto kuchomekwa vijiti,penseli,vidole na vitu kama hivo na wenzake sehemu za siri. Hivi wanatoa wapi fikra kama hizi za kishetani au wazazi wao wanafanya hazarani au wanakuwa wakifanyiwa na madada wa nyumbani??

  Matukio haya ni mengi,kuna familia imevunjika kutokana na haya;mzazi mmoja kujua mtoto wao alifanyiwa kiasi cha kuanza kujinyea hovyo na kumficha mwenzake, badae mwenzake alipojua tatizo na kwamba alifichwa ikawa ndio mwisho wa ndoa yao,inasikitisha sana!

  Kumbe tatizo ni kubwa zaidi,kiasi cha kuharibu ndoa na sio mtoto pekee! Je polisi,wananchi,mamlaka za ustawi wa jamii, wizara zipo kuchunguza haya mambo mashuleni!? Au mwisho wao ni kwenye kutoa vibali na kupokea malipo!

  Nitaendelea kutoa taarifa zaidi punde zikiitajika. Unaweza kunitumia meseji binafsi nitakujibu. Jamani,wazazi tuwe makini hizo ada mnazolipa ni kubwa sana watoto wenu kupuuzwa.

  Kama uandishi ni mbovu,tusameheane! Ila nina uhakika nimeeleweka.
   
 2. l

  lasix JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  inasikitisha sana kwa kweli,watoto tunajitahidi kuwapa malezi bora nyumbani ila wakifika shuleni wanaharibiwa na wachache ambao wamelelewa malezi ya kutopewa uangalizi wa karibu matokeo yake kila kitu wanataka wajaribu..hebu fikiria mwanao anafanyiwa vitendo ivo na wenzake tena ktk mazingira ya shuleni ambayo tunayaona ni salama zaidi..
   
 3. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Habari kama hizi zinahatarisha sana amani hasa kwenye nchi zenye waumini wengi wa kiislam kama hapa kwetu. Unajua kwenye swala kuu ya ijumaa mfuga ndevu mmoja anaweza kutoa fatwa na umma ukaishukia hiyo shuleTakbir allahu akbar!! . Juzi juzi tu huko misri mtu kwenye TV bila woga alizusha uongo kuwa wakiristo wa nchi hiyo walikuwa wanapiga askari jeshi na kuomba umma uende kuwasaidia askari jeshi tena wenye bunduki (AK47) na matokeo yake kukawa na genocide ya wakiristo. Ndo wanavyoanza hivyo kutafuta visa na visingizio vya kumwaga damu nadhani huyo mungu wao ni vampire
   
 4. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mrdash1, humu sikuongelea dini ama kitu kama hicho! ningeomba usipotoshe maana ya hii thread. Mada inahusiana na watoto kudhalilishwa wakiwa kwenye shule tunazoziamini kuwapa misingi bora ya elimu na maisha, na wazazi wawe na muda kufanya uchunguzi wa hizo shule na sio kuachia watu wengine wawafanyie.
   
Loading...