Mabadiliko ya kitabia

Explainer

JF-Expert Member
Dec 16, 2015
516
504
Msishangae wakuu, ikiwa mtu akaanza mada bila hata kutoa salamu.

Habari zenu wakuu,

Unajua ugumu wa maisha umetufanya tubuni mbinu mpya ya kujipatia ridhiki. Jamani jamani naomba niweke wazi kitu hiki kinachonipa wasiwasi ndani ya Taifa letu.

Kumekuwa na ongezeko kubwa la ndugu zetu omba omba wasiokuwa na vigezo vya kuomba omba barabarani. Hawa nao tuseme wamefoji taaluma hii? Au ndio ugumu wa maisha? Kuna jamaa mmoja mitaa ya Upanga pale yaani yeye ni mzima kabisa lakini maisha yake amewekeza katika kuombaomba pesa vitoto vidogo vya shule ya msingi Diamond.

Ukipita na mitaa ya mjini kati utakutana na ombaomba wanaotumia hadi smartphone, yaani leo nimechoka kabisa wengine wanawatumia watoto wadogo na kila mtoto jioni anatakiwa akabidhi hesabu yake ya mapato ya siku nzima.

Tulitazame tatizo hili kwa jicho pevu jamani, ikiwezekana wale wote wasio walemavu wala matatizo yoyote wakamatwe na kisha watafutiwe kazi za kufanya, maana hii ni aibu kwa Taifa na ni mfano halisi wa jamii yenye watu wavivu kabisa.

Ila kama wameachwa ili kuwa vivutio kwa watalii hapo sawa, maana kupitia wao watautangaza ujinga wetu, uvivu na upungufu wa maarifa na pia tutapata fedha nyingi za kigeni toka kwa watalii wanaokuja kushangaa omba omba wazima kabisa wasiokuwa hata ulemavu wowote.

Asanteni.
 
Hahhhaha umenichekesha sana mkuu...Eti ombaomba ana smartphone kabisa na ni mzima...Hao ndio wale ukiwapa pesa nzuri wanapiga selfie na wewe!!
 
Mkuu kiukweli umewaza mbali Ila umeshajiuliza kuna wasomi wangapi mpaka Leo Hawana kazi za kufanya, Je hao omba omba tutawapatia kazi gani ilihali wengi wao hawana elimu na hawana ujuzi wowote?

Waacheni tu waombe kwani hata wao wanahaki ya kumilki hizo smartphones Au mkuu hautaki na wao waifufahie JF?
 
Omba omba hawajaongezeka ni mtizamo wako tu,Jiji hili la Dar limekuwa na ombaomba miaka nenda miaka rudi.

Na kutokana na ongezeko la idadi ya wakazi kwa sasa wa Dar na Inahitaji ya kila mmoja yameongezeka sana na ukilinganisha na gharama ya kuishi.

Na kuna njia nyingi za utapeli kwa sasa ndiyo zimeibuka kwa hapa Dar mithili ya msaada kumbe ndiyo unaibiwa taratibu bila kujua ukifikiri unasaidia.

Na wengi tu wanaibiwa kimya kimya wakifikiri wanatoa msaada kumbe ni utapeli mpya hapa Dar
 
Back
Top Bottom