Mabadiliko ya kimfumo mikopo elimu ya juu

Said mgoha

New Member
Jul 6, 2021
2
2
MAOMBI YENYE KUBAHATISHA

kawaida kila mtu mwenye uhitaji ni lazima ajitutumue kuhakikisha anafanikiwa kwenye malengo yake alojiwekea kwa namna moja ama nyingne katika mazingira aliyopo na kulingana na hali alonayo.

Ni mara nyingi nimesikia, nimejionea na nimejaribu nami pia katika kuhakikisha nami najitahidi katika malengo yangu kuhakikisha yanafanikiwa kwa wakati na kwa muda nilojiwekea mwenyewe ukiachana na utaratibu ambao unakulazimu uufate pale inapobidi kufanya hivyo. Lakini katika kuyafanikisha haya huhitaji uwezeshaji ili kufikia malengo kulingana na jambo unalolifanya maeneo ulipo.

Yawezekana unachokifanya kinahitaji elimu ya juu ili utimize ndoto zako, na elimu hiyo ya juu ni gharama, iwe kwa vyuo binafsi ama vya serikalini, ni lazima utahitajika kupata mafunzo hayo kwa gharama iwe mtoto wa masikini au watajiri na utapaswa kulipa kwa kiwango kilekile kulingana na fani ama course unayosoma katika hicho kitu kiitwacho elimu ya juu.

Na ifahamike kwamba katika makundi haya mawili ya mwenye nacho na asie nacho bali anajikongoja kwa kuungaunga maisha, yeye na familia yake kwa kuungaunga kiubishi ili mambo yaende kwa kujishughulisha na shughuli mbali mbali ilimradi apate msingi utakao muwezesha kuupigania ujuzi anaouhitaji katika elimu hiyo ya juu.

Kwa mwenye kujua katika jitihada iliyofanyika ama iliyochukuliwa na serikali yetu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania katika kumuwezesha mtu huyu anaeipagania ndoto yake na kuhakikisha anaifikia, ni pamoja na kuanzishwa kwa BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU (HESLB). Hiyo yote ni kuhakikisha kwa wale wenye uhitaji basi wanapatiwa mikopo na kuendelea na kupata elimu hiyo inayopatikana kwenye mavyuo mbali mbali nchini.

Katika uhalisia wahitaji wa msaada huo (kukopeshwa kiasi cha fedha wezeshi) ni wengi katika jamii tulonayo. Na kwa bahati mbaya sio kila anaeomba hupata msaada huo kama alivyotarajia katika maombi aliyafanya katika wakati ambao suala hilo liliruhusiwa kufanyika ama pale tu lilipotangazwa.

Ukizingatia watu wanaoomba ni wengi, na kila mmoja hufanya hivyo kipigania ndoto yake ambayo huenda ikakamilika kwa kufika hatua hiyo ya kupata elimu ya juu . Pamoja na kuingia gharama huku na huko, ukizingatia wakati mwingine inakuhitaji wewe unahitaji mkopo huo wa elimu ya juu hata usafiri kunako wezesha ama rahisisha utumaji wa maombi yako. Kwa mfano: muombaji anaweza kuenda internet cafe, kwa wakili kusaini vyeti, Rita kuthitisha vyeti, kutuma nakala, etc. Yote hayo yanafanyika na applicant kwa lengo la kuhakikisha anazingatia matakwa ama vigezo ambavyoanatakiwa kukidhi ama kuzingatia muombaji.

Yawezekana kuwa na waombaji wengi zaidi na wakapatiwa wachache Kati ya wengi hao waloomba mkopo huo wa elimu ya juu. Mfano wanaweza kuomba watu elfu 60000 na kidogo na wakapatiwa watu 30000 na kidogo. Kati ya watu hao kunamtu kakosa ama kanyiwa kama wanayosema waombaji wenyewe kuwa flani kapewa mkopo mie nimenyimwa na lawama zingine nyingi na kuishia kulia tu, huku akidai flani kapata lakini hakuwa na sifa kama ilivyohitajika. Nakumbuka nimewahi kukosa mkopo wa elimu ya juu huku nikiwa nahitaji pesa kweli kweli, na jina langu halikuonekana kwenye majina yalokuwa na dosari kwenye baadhi ya documents zao wala kwenye lists ya walopata mkopo huo. Nilikata tamaa, japo kunahaki ya kukata rufaa, sikuona umuhimu tena zaidi ya kuongeza gharama tu katika uombaji huo wa mkopo muhimu sana katika elimu hiyo ya juu. Nikamua kuachana na habari ya kukata rufaa.

Kutokana na hali hii ya uhitaji nikajiwazia zangu mwenyewe Kwani kukiwa na vigezo huwa kunazaidi ya kigezo kingine?, na kama hakuna kwanini nilikosa mkopo huo wa elimu ya juu? Ama sikuwa na sifa za ziada ambazo hazikuwa zimeanishwa ama nilisahau kusoma document moja yenye maelezo nini cha kufanya wakati unapofanya zoezi la uombaji?, na kama hapakuwa na tatizo basi yawezekana walioomba ni wengi kuliko idadi ya ambao wangepatiwa mkopo huo, hivyo ililazimika wengine wakose watake wasitake wangekosa tu.

Huku nyuma baada ya kumaliza kutuma maombi ungeweza kuamini umemaliza kazi kwa kuwa maombi yako yameenda ulipotaka yafike, kwa bahati mbaya majina ya vyuo yametoka na umefanikiwa kupangiwa chuo zaidi ya kimoja. Lakini majina ya mikopo nayo yanatoka ukosa kuonekana kwenye batch zote ya kwanza mpaka ya nne. Unaanza kuhangaika na kukata rufaa mara mungu yupo nawe unatoka kwenye list ijayo. Wengine Hata haki ya rufaa wakiitumia hukwama pia.

Lakini nikajiwazia ingekuwa kunautaratibu ambao (system)umeratibiwa kwa lengo la kupokea majina na sifa zake pamoja na muda ambao ingeweza kujifunga ama kujizima pale idadi inayohitajika ili kupatiwa mkopo huo inapokuwa imeenea. Aka kufanya hivyo itasaidia kumuhakikishia yule mwenye uhitaji kupata uhakika wa kupata mkopo huo, hali hiyo pia ingeweza kupunguza usumbufu hata katika wahitaji na ofisi kupitia idadi ya applicant elfu 60000 na kidogo ambayo sio wote ambao wangepatiwa mkopo huo.

Vile vile pia, nadhani ingeweza kusaidia kwa mtu ama muombaji atakae kuwa amechelewa kufanya utaratibu mwingine mapema ili kuhakikisha anaendelea kwenda kukamilisha malengo yake kwa kujipanga mapema zaidi maana atakuwa amejionea mapema kuwa mkopo amekosa kwa kuwa system amepokea idadi iliyohitajika na imekamilika hivyo haipokei tena. Na taarifa itatolewa mapema baada ya system kujizima ili waombaji wengine kusitisha zoezi hilo la uombaji. Na kama ingehitajika zoezi hilo la ukopeshaji liendelee kwa wanafunzi wa elimu ya juu basi system ingesetiwa upya na kupokea idadi elekezi kuliko kuhangaika na ukataji wa rufaa na mambo mengine kama hayo yangekuwa hayapo tena katika kubahatisha upatikanaji wa mkopo huo. TEHAMA ni watu wetu, tuwatumie kwa faida ya taifa letu, ili kazi iendelee kwa kasi. Wizara zinazohusika (ya fedha na elimu) zinaweza fanya jambo ili kurahisisha na kuboresha mazingira haya ya utoaji mikopo elimu ya juu.

Nimeamua kuandika kwa kuwa muda si mrefu zoezi hilo litafanyika na changamoto zile zile za mwaka 2017 na kuendelea tunakwenda kuzipata tena. Unajikuta mkopo hujapata, hukujiandaa kwa namna nyingine yoyote, zaidi ya kusubiri muda wa kukata rufaa ujaribu haki hiyo.

Naomba kuwasilisha kwako mwanakuijenga jamii yetu mwanajamii, mwenzangu hapo ofisini kwako na kama muhusika mwenye kuamiwa na kubeba dhamana juu yetu sie wahitaji wa huduma hiyo.

By Sas M.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom