Mabadiliko ya bei za Nishati ya Mafuta

Mabadiliko ya bei za Nishati ya Mafuta

Display Name

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2014
Posts
423
Reaction score
451
MABADILIKO YA BEI ZA NISHATI YA MAFUTA

Beiza mafuta yanayopitia bandari ya Dar es Salaam zimepungua kwa mwezi wa pili mfululizo na kufikia shilingi 2,120 kwa lita moja ya petroli, 2,080 kwa dizeli na 2,046 kwa mafuta yataa.

Kwa kila lita kumekuwa na punguzo la shilingi 175 kwa petroli, shilingi 144 kwa dizeli na shilingi 156 kwa mafuta yataa, kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Udhibitiwa Huduma za Nistahi na Maji (EWURA) Dodoma. Bei hizo zitaanza kutumika kesho tarehe 6 Februari, 2019.

Hii ina maana pia kwamba kwa mwezi Januari na Februari 2019, bei za rejareja za Petroli, Dizelina Mafuta ya Taa zimepungua kwa jumla ya Shilingi 316, Shilingi 356 na Shilingi 323, mtawalia.

Taarifa hiyo imeeleza pia kwamba bei za mafuta yaliyopitia bandari ya Tanga zitaendelea kuwa zile za mwezi uliopita kwasababu hakukuwa na shehena mpya.

Hali kadhalika, beiza mafuta yaliyopitia bandari ya Mtwara zitaendelea kuwa zilezile zilizotangazwa Januari 25 2019, ambapo petroli ilipungua kwa shilingi 271 na dizeli shilingi 221 kwa lita.



Sent using Jamii Forums mobile app
 

Attachments

Ina takiwa yauzwe buku kwa ltr moja
 
Nishangaa kukuta ati bei ya Diesel imepanda kuwa juu ya Petrol. Tena kwa shs 40 zaidi. Je mnaonunua haya mafuta mliiona hii??
 
Angalau sasa 10,000 itakuwa na thamani kwenye wese!!!
 
Back
Top Bottom