Mababu na mabibi zetu hawatuambii! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mababu na mabibi zetu hawatuambii!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by VUTA-NKUVUTE, Mar 14, 2012.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,870
  Likes Received: 6,609
  Trophy Points: 280
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekuwa na kawaida ya kuongea na 'Wazee wa Dar es Salaam' hasa anapoongelea masuala yashikayo chati nchini.Kwa mfano,aliongea na wazee hao pale alipochimba biti kwa Mgaya wa TUCTA juu ya Mgomo wa Wafanyakazi wa Taifa zima.Pia ni hivi majuzi tu,Rais ameongea na wazee hao wa Dar kuelezea hasa mgomo wa Mdaktari nchini.

  Pamoja na utaratibu huu kuonekana na Ikulu kuwa wamfaa Rais wetu,tatizo kubwa ni moja.Wazee wetu(Mababu na Mabibi zetu) hawajawahi kutuambia wanachoongea na Rais Karimjee na kwingineko.Wanabaki kusifia msosi wa kujisevia na vijisenti wanavyopewa kutokana na usikivu wao 'makini'.

  Rais wetu Kikwete na aongee nasi vijana Karimjee....
   
 2. k

  kuzou JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  anaongea nasi kupitia wazee,ni kama ambavyo waziri mkuu anaongea na wahariri lkn walegwa ni sisi.
   
 3. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,289
  Likes Received: 1,436
  Trophy Points: 280
  anapohutubia Taifa kila mwisho wa mwezi huwa anamwita nani kusikiliza?

  Kusema anaongea na wazee wa Dar ni ka platform tu lakini sio kusema kuwa anawaambia kitu wazee ili waje kutujuza aliyoongea nao. Ni moja kati ya outreach programmes.
   
Loading...