Maaskofu, wananchi ‘wamchanachana’ Slaa

Maaskofu, wananchi ‘wamchanachana’ Slaa

Aende CCM ambao wamebaki mafisadi kumi katika nile list yake wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM (hayo ni madai yake padre slaa), amechanganyikiwa kukosa nafasi ya urais na hata angepewa asingekuwa na mvuto kama lowassa, akiona vipi aanzishe chama chake kama zitto
 
Hivi Gwajima nae ni askofu au uchwara tu
 
Maaskofu wako kanisa Katoliki tu, wengine ni wachungaji tu
 
Kajimaliza yeye mwenyewe kwa mdomo wake Richmond ya sawa mbona hakusema escrow ambayo ni mbichi kabisa wapi miswaada ya dharura kuhusu gesi iliyosainiwa ghafla ye kang'ang'ana na Richmond tu... Viva ukawa kura yangu itafanya mabadiliko
 
mshenga amepanic mapema sana na alivo #DOMOKAYA lazima ajifanye anajibu jumapili anaweza kukodi hata bendi ya taarabu maana akili zake sijui ni za kuazima maana simuelewi kabisa huyu #MSHENGA WETU
 
Atuambie alivyoacha upadre kanisa lilisimama au lilisonga mbele? C.D.M bado ipo imara na inasonga mbele
 
Duh!kweli chadema zero,yani Gwajima ndie msuluhishi wenu?
 
huyu Dr.ni wa kumpotezea tuwe bize na mapambano adi October
 
Tena huyo Mshenga anatakiwa akae kimya, Hana Buasara wala Hekima, Alimtukana KADINARI PENGO tena akae kimya PUMBAVU.
 
wanaompinga dr slaa kwa matamshi yake ya jana hayana mshiko au hawajamuelewa anasema pingeni yeye ushahidi anao
 
wakati kina magufuli wanachanja mbuga vijijini,mko busy n dr slaa ,nasikia lowasa ameahirisha kampeni na kurudi dar kumjibu slaa,na lowasa hanaga point labda aje humu jf achukue point za kusema kwenye press comf ya kesho.....

anadhani kutokea kwenye luninga ndo kutampa kura.


viijini wenye tv ni wajanja wachache,mtawazengua wanywa viroba,bodaboda na masela wachache,lowasa kuingia ikulu ni ndoto za alinacha asee
 
View attachment 282914




Askofu Josephat Gwajima amejibu tuhuma zilizoelekezwa kwake na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa kuwa alishiriki kama ‘mshenga’ kumshawishi mwanasiasa huyo kumpokea Edward Lowassa katika chama hicho.

Jana, Dk. Slaa alimtaja Askofu Gwajima kama mshenga na kwamba alimshawishi ampokee Lowassa huku akidai kuwa askofu huyo alimtamkia kuwa maaskofu 30 wa Kanisa Katoliki walihongwa na timu ya Lowassa.

Askofu Gwajima amekanusha taarifa zilizotolewa na Dk. Slaa ambaye alikuwa rafiki yake kwa muda mrefu akidai kuwa ni muongo mkubwa. Alisema kuwa Dk. Slaa ameamua kuwashambulia maaskofu hao kwa kuwa anafahamu hawana majukwaa ya kumjibu kama ilivyo kwa wanasiasa.

Gwajima alidai kuwa yeye aliitwa kama msuluhishi ndani ya Chadema na sio mshenga wa kumleta Edward Lowassa.

“Kwa kawaida inashangaza kwamba kama watu wawili wanagombana inatakiwa awepo mtu wa kuwaunganisha, ila anaposema maaskofu 34 haileti maana, haiingii akili, ameingiza Gwajima, Rostam Aziz na maaskfu,” Gwajima ameliambia gazeti la Mtanzania na kuongeza kuwa Dk. Slaa ametumwa na watu anaowafanyia kazi.

Askofu huyo alidai kuwa alichokisema jana Dk. Slaa kilikuwa silaha pekee ya CCM iliyokuwa imebaki na kuwataka waumini wake na watanzania kutoamini alichosema mwanasiasa huyo.

“Nafikiri Slaa ndio risasi ya mwisho ya mwisho iliyokuwa imebaki kwenye bunduki ya CCM,” alisema.

Jana Dk. Slaa alitangaza kustaafu siasa za vyama akieleza kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa siasa nchini hususani Chadema aliyoijenga kwa ajenda ya kupinga ufisadi na badala yake wamemkumbatia Lowassa waliyekuwa wanamtuhumu kuwa fisadi mkubwa.

Gwajima umechemsha kaka tubu mapema wewe ni mtumishi wa Mungu.
 
Back
Top Bottom