Maaskofu Wakataa Uchaguzi Jumapili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maaskofu Wakataa Uchaguzi Jumapili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nyikanavome, May 26, 2010.

 1. Nyikanavome

  Nyikanavome JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Maaskofu wakataa uchaguzi Jumapili
  Wednesday, 26 May 2010 04:31

  *Ni wa madehebu yote ya kikristo
  *Waunda Jukwaa kupata sauti moja

  Na Job Ndomba

  MAASKOFU wa Madhehebu ya Kikristu nchini wamezindua jukwaa lao na kulitumia kuitaka serikali kupanga siku yoyote ya kazi kwa ajili ya uchaguzi mkuu badala ya kutumia Jumapili kama ilivyozoeleka.

  Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana aliyekuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Wakristu Tanzania, Askofu Severine Niwemugizi wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Rulenge-Ngala mkoani Kagera.  Askofu Niwemugizi alisema pamoja kwamba serikali imeshapanga tarehe ya uchaguzi, Jukwaa hilo linaiomba kuangalia upya na kuitafuta siku nyingine mbadala na kuiacha siku ya Jumapili kuwa ya watu kuabudu.

  "Japokuwa maamuzi yanaweza kuwa magumu kutokana na gharama, lakini tunaiomba serikali kuangalia upya siku ya kufanya uchaguzi badala ya Jumapili kwani siku hiyo ni ya watu wa Jumuiya za kikristu kuabudu," alisema.

  Alisema kuwa hilo linawezekana hata kwa kuigwa kutoka nchi ya jirani ya Burundi, ambao waliamua kufanya uchaguzi Jumatatu.

  Askofu huyo liwatoa hofu baadhi ya watu waliodhani kuwa kuundwa kwa jukwaa hilo kuna lengo la kuvunja makanisa kuwa na kanisa moja, chini ya uongozi wa jukwaa hilo, bali watambue kuwa lengo lake ni kuwa na umoja wenye sauti ya pamoja.

  "Lengo letu ni kuwa na umoja wenye sauti moja na hivyo kila taasisi ya dini itaendelea kuwa na imani yake lakini linapotokea jambo kutakuwa na sauti moja," alisema.

  Aliongeza kuwa malengo yake ni kulinda na kutetea uhuru wa kuabudu, kuhamasisha maombi katika mambo makubwa nchini, na kuwa na sauti moja ya kuimarisha imani ikiwa ni pmaoja na kuvumiliana na kuheshimiana.

  Alisema kiu ya kuwa na umoja huo ilianza muda mrefu na lengo kuu ni kuwa na umoja ambao ni kielelezo cha imani na upendo na hii ni chumvi ya amani nchini.

  Naye Mwakilishi wa Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. William Lukuvi alisema umoja huo utaisaidia serikali kutekeleza wajibu wake vizuri kwani ni ukombozi wa kihistoria katika ukristu nchini.

  Bw. Lukuvi alisema jukwaa hilo ni mwavuli wa taasisi zingine ndogo ndogo za kikristu na litasaidia serikali kutoa vibali vya shughuli mbalimbali kirahisi na kudhibiti vizuri vikundi vinavyotumia vibaya miavuli yao ya imani.

  Alilitaka jukwaa hilo kufunga milango yake vizuri ili kudhibiti wahuni wanaoweza kulivamia na kulitumia vibaya kinyume na mwongozo wake.

  Awali akitoa chimbuko lake, Mratibu wa Jukwaa hilo, Katibu Mkuu wa CCT, Dkt. Leonard Mtaita alisema lilianza mchakato wake mwaka 2007 na kufikia maamuzi ya kuzinduliwa jana.

  Jukwaa hilo kwa sasa litaongozwa chini ya wenyeviti wenza wa Jumuiya ya Kikristu Tanzania (CCT) na wenyeviti wake ni Maskofu Gerald Mpango, Peter Kitula na Owdenburg Mdegela (KKKT-Iringa), lakini kila taasisi itakuwa na wenyeviti wake.

  Baraza la Maskofu Tanzania (TEC) litakuwa na wenyeviti wenza, Askofu Bruno Ngonyani (Lindi), Askofu Pascal Kikoti na Askofu Mkuu Paul Ruzoka (Tabora).

  Na kwa upande Makanisa ya Pentekoste (PCT), kutakuwa na Askofu Sylivester Gamanywa, Danie Awet na Eliud Isakya.

  Uzinduzi huo ulihudhuriwa pia na maelfu ya waumini wa jumiya hiyo na ulianza na kufungwa kwa sala na kupambwa na nyimbo mbalimbali za kwaya.

  Maaskofu wakataa uchaguzi Jumapili
   
 2. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2010
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  TUNGOJE KESHO NA WAISLAMU WASEME KUWA WANATAKA IJUMAA ISIWE SIKU YA KAZI BALI IWE MAPUMZIKO ILI WAUMINI WAKE WAENDE KUABUDU.


  Kazi kweli kweli
   
 3. d

  damn JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Haina shida yote yanawezekana. lililo muhimu ni watu na jamii kukubaliana, kwamba ijumaa ni off, tukikubaliana tutasema SAWA. Ikiwa uchaguzi usiwe siku ya idaba kwa dini yoyote tukikubaliana itakuwa SAWA. Hatuhitaji hata kuumiza vichwa. mifumo yote ya maisha ni majadiliano na makubaliano.
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kumekucha! haya, tuone basi kama kweli nchi hii inandeshwa kwa nguvu ya Kanisa au la -- kama wanavyodai Waisilamu! Kazi kwako Muungwana!
   
 5. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Hapa sababu ya msingi ni kuwa uchaguzi ni muhimu na uchukua muda kidogo; hawa maaskofu wameomba hili kiutu uzima ili wakristo washiriki kupiga kura kikamilifu kama waraka zao zinavyosema! Pia hii ni siku moja tu. Sasa waislamu wakitaka Ijumaa iwe weekend maanake kwa mwaka siku 52, i.e. pia wao watatoa sababu zao za msingi.
   
 6. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Maaskofu hawa wameiomba serikali na sio kwamba wameagiza. Wangekuwa wameagiza na ikitekelezwa basi nchi itakuwa inaendeshwa kwa nguvu ya kanisa bali lao ni ombi na serikali inaweza kukubali au kukataa na hapo hakuna nguvu ya kanisa.
   
Loading...