Mimi ni Roman Catholic lakini hawa maaskofu wamenifanya niufikirie mara mbili mbili huu ukatoliki wangu.
Kwanini hawa maaskofu watudharau kwa kiasi hiki? Yani wametuona sisi ni ma-Robot tusioelewa chochote hadi tuelekezwe cha kufanya?
Wewe ni muumini wamashaka na kwa kua ni mambo ya imani nitasema tuu Mungu akusaidie
Hawa maaskofu kwa akili zao wanadhani Mungu alishindwa kutufanya ma-Robot tufanye anayoyataka yeye tuepukane na haya mateso ya hii Dunia?
Wamenikera sana hao maaskofu.
Tatizo Lako Mkuu Bado Hujamuelewa Vizur MUSAMI Kwa Ufupi ilitakiwa Maaskofu Wakae Pamoja Na Mashekhe Wajadil Msimamo Wao Ndo Wautoe Hadharani. Lakin Kusema Maadhimio Ya Maaskofu Tz Ni ... Juu Ya Katiba. Swali, Je Masheikh Nao Wakija Na Msimamo Wao Kinyume Na Maaskofu Huoni Kama Itatokea Balaa Kubwa?.
Mimi hapo sioni ushindani wowote. Mbona serikali hiyo hiyo inahimiza viongozi wa dini kuwalea watu wake katika maadili na kupelekea nchi kupata viongozi wazuri? Huwezi kutenganisha dini na serikali. Utasali wapi kama hakuna amani? Hapa Maaskofu walimaanisha kuikubali katiba hii ni sawa sawa na kutenda dhambi kwa maana wanajua hii katiba itaathiri vizazi miaka mingi mbele na hii dhambi itatokana na maamuzi ya leo. Tukubaliane hivi, serikali ikiipigia kampeni hii katiba ili ipite acha na wengine waipinge. Kwanini serikali inalazimisha watu kuipigia kura ya NDIYO hii katiba? Nijibu hilo swali langu ndo nitaendelea kuchangia hii thread.
Kwa hiyo wewe unakubali serikali inavyoipigia debe katiba? Serikali yenyewe ina ajenda gani inapowaambia watu wapige kura ya NDIYO? Kwa nini serikali wasitoe tu uhamasishaji wa kusoma katiba wakawaacha watu kuamua wenyewe? Mifano halisi ninayo. Waziri Mh Mary Nagu juzi kati alikuwa na wamasai akawaambia hii katiba ni nzuri wapige kura ya NDIYO (Hiyo ni kampeni ya serikali) Makamu wa pili wa rais kule Zanzibar naye hivi majuzi kule Zanzibar aliwaambia wananchi kuwa wapige kura ya NDIYO. (Pia hiyo ni kampeni ya serikali) Sasa inakuwaje vibaya Maaskofu kuwaambia waumini wao wapige kura ya HAPANA wanapoona inatakiwa kuwa hivyo? Jamii forum ni ya watu wenye akili wanaoweza kuchambua mambo lakini nasikitika kuona watu wengi wanashindwa kuielewa vizuri hii nchi yetu. Tukubaline hapa kama Maaskofu wamekosea basi na serikali ishakosea zamani na hakuna wa kumlaumu mwenzie...
Mimi katika katiba hii pendekezwa wala kurayangu sio ya siri niwazi tu kwamba nitapiga kura ya H.
Lakini siwaungi mkono maaskofu kwa kauliyao ya kutuelekeza aina ya kura tutakayo piga, wana siasa wanaweza kuwaelekeza wanachama na wana nchi wote aina ya katiba wanayoona kwamba ina faa, na kuwaelekeza wana nchi wapige kura ya namna gani.
Viongozi wa dini wasijiingize kwa undani sana katika maswala ya kisiasa.
maandiko hayana maana km unavyofikiria wewe,hivi Maaskofu wakitulia pasipo kusema chochote huku mambo yanaharibika,kesho na kesho kutwa nchi isipokalika huo Ufalme wa Mungu watauhubirije?,Na je watu wakianza kukimbia machafuko huo Ufalme wa Mungu watamhubiria nani??? KAA FIKIRI KWA KINA.
Tokea Kardinali Pengo atoe kauli ya kupinga mapendekezo ya Maaskofu juu kura ya hapana kwa katiba inayopendekezwa,amekuwa akiitwa msaliti hata kufikia kutukanwa na akina Gwajima,lakini nionavyo mimi wasaliti ni maaskofu.
1.Wameusaliti wito wao wa kuutangaza Ufalme wa Mungu badala yake wamekaa wakipoteza muda kuujadili ufalme wa duniani Luka 9:2 Yohana 18:36 labda watuambie wameongozwa na andiko gani
2.Wamesaliti umoja wa Taifa la Tanzania maana unapotoa tamko la wakristo kupiga kura ya hapana unawaambia nini watu wa imani nyingine?je na wao wakikutana kupiga kura ya ndio,mustakabari wa Taifa utakuwaje?
3.Je huu sio mwanzo wa kutumia umoja huu kufanya kampeni za viongozi wanaoona wao wanafaa kuongoza kipindi cha uchaguzi?
4.Makanisa yanahusisha watu kutoka makundi mbalimbali,wapo wanaoipinga katiba inayopendekezwa na wapo wanaoikubali,je huu sio mwanzo wa kukaribisha migogoro ya kiitikadi ndani ya makanisa.
Mungu atusaidie