Maaskofu Katoliki watoa waraka mwingine 2010 | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maaskofu Katoliki watoa waraka mwingine 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by BAK, Jul 7, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  *WATAKA VIONGOZI WALA RUSHWA WASICHAGULIWE, VYOMBO VYA DOLA KUTOTUMIA NGUVU KUPITA KIASI

  Exuper Kachenje
  Mwananchi

  Wednesday, 07 July 2010

  BARAZA la Maaskofu Katoliki nchini (TEC), limetoa waraka wa Uchaguzi Mkuu huku likiionya serikali na vyombo vyake kuhusu matumizi ya nguvu kupita kiasi na kutaka vitumike kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi.

  TEC imetoa waraka huo ikiwa ni miezi mitatu kabla ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 31 mwaka huu. Mwaka jana, Kanisa hilo lilitoa ilaani ya Uchaguzi kwa waumini wake jambo ambalo lilipingwa vikali na serikali.

  Waraka huo unafuatia mkutano wake mkuu wa 63 uliomalizika jana makao makuu ya TEC Kurasini jijini Dar es Salaam ukiwakutanisha maaskofu wote 33 wa Kanisa hilo nchini.

  Mbali na onyo hilo kwa serikali na vyombo ya dola, waraka huo umevionya vyama na wagombea wa nafasi mbalimbali kuheshimu kanuni za uchaguzi pamoja na kuhimiza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na ile ya Zanzibar (ZEC) kujijengea imani na heshima kwa kusimamia uchaguzi kwa kuheshimu katiba na kanuni ili uwe wazi, huru, haki na usalama.

  "Kwa hiyo sisi kama kadri ya nafasi yetu kama viongozi wa dini na raia wa nchi yetu ya Tanzania tunatambua kuwa tuna wajibu na haki ya kusema yafuatayo juu ya uchaguzi ujao:

  Katika waraka huo, maaskofu hao walisema kuwa vyombo vya dola ni muhimu katika kulinda usalama hasa wakati wa kipindi cha uchaguzi, pamoja na kuwa mara kadhaa imetokea kwamba nguvu kupita kiasi zimetumika na vyombo hivyo kuliko inavyohitajika:

  "Tunaviomba vyombo vya dola vitumie nguvu zake kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi, kwa kuzingatia maadili ya kazi yao pasipo kuegemea upande wowote Ili uchaguzi uwe kweli huru", ilisema sehemu ya waraka huo uliosainiwa na maaskofu wote 33 wa TEC wakiongozwa na Rais wao Askofu Yuda Thadei Ruwa'ichi wa Jimbo Katoliki Dodoma.

  Waraka huo unawaelekeza wapigakura waliojiandikisha kutimiza wajibu na haki yao ya kuchagua viiongozi kwa umakini, kuwahoji na kuwapima wagombea udhati wa nia yao kwa kufuata vigezo vya hadhi ya utu wa mwanadamu na tunu za kimaadili.

  "Kamwe wasimchague mtu kwa shinikizo, kwa msingi ya ukabila, dini, rangi jinsia, wala sababu ya takrima au rushwa", ulionya waraka huo.

  Waraka huo ulibainisha kuwa suala la rushwa limejitokeza karibu katika kila uchaguzi, huku jambo baya zaidi likiwa baadhi ya wananchi kujenga tabia kuendesha maisha yao kwa kutegemea rushwa wanazopewa na wanasiasa.

  Kutokana na hilo, waraka uliainisha kuwa uchaguzi unapofika na hata baada ya uchaguzi jambo linalosababisha baadhi ya wanasiasa kuendelea kubaki madarakani pamoja na kupoteza mvuto na ushawishi wa kiasiasa, uwezo hata sifa za uongozi.

  Baraza la TEC lililaani kujitokeza kwa hali hiyo katika chaguzi zilizopita na baadhi ya watu kudaiwa kuuza vitambulisho vyao vya kupigia kura likieleza kuwa kuuza kura ni kusababisha utawala mbaya, kuuza uhuru na usaliti.

  Kuhusu vurugu kuchafuana kwa baadhi ya wagombea TEC imesema vitendo hivyo vilikuwepo katika chaguzi ndogo zilizopita huku ikiviomba vyama vya siasa na wagombea kunadi sera zao zinazoweza kushawishi wagombea na siyo kushindana kwa maneno ya kashfa na matusi yanayosababisha uvunjifu wa amani.

  Aidha, waraka huo wa TEC umezungumzia pia baadhi ya vyama na wagombea kukosa ukomavu wa kisiasa, unyofu na unyenyekevu wa kukubali matokeo hasa ya kushindwa katika uchaguzi ukiwataka watakaoshindwa kihalali kukubali matokeo na kuungana na wengine katika kujenga nchi.

  "Tunahimiza vyama na wagombea watakaokuwa wameshindwa kihalali kukubali matokeo ya uchaguzi na kuungana na wengine katika kuijenga nchi,"ilieleza sehemu ya waraka huo huku ukiendelea kufafanua kuwa;

  "Tunawaalika wagombea ambao wanadhani hawakushindwa katika uchaguzi kwa njia ya haki, watafute haki zao kwa namna inayokubalika kisheria, kuliko kuhamasisha vurugu na ghasia ambazo matokeo yake ni kusababisha uharibifu wa mali na pengine kupoteza maisha ya watu bila sababu za msingi."

  Hata hivyo, waraka huo ulieleza kuwa mara nyingi vurugu zinazofanywa na vyama na wagombea mbalimbali au kukataa matokeo kusababishwa na hisia kwamba kanuni mbalimbali za uchaguzi kutoheshimiwa au kukosa uwazi katika uchaguzi.

  TEC imetumia waraka huo wenye kurasa tano kuwataka viongozi wenzao wa dini mbalimbali kutoegemea upande wowote wala kushika uelekeo wa kundi lolote, badala yake kuwa sauti ya wasio na sauti wenye kupima mambo kwa ukomavu, upeo haki na ukweli bila kuathiri uadilifu wao huku likiwataka wananchi kuombea Uchaguzi Mkuu ili wapatikane viongozi wenye kujali maslahi ya wote na kujenga jamii yenye upendo, umoja, haki, amani na maendeleo ya kweli.

  Hii si mara ya kwanza kwa Kanisa Katoliki nchini kutoa ujumbe kuelekea Uchaguzi Mkuu. Mwaka 2005 na miaka ya nyuma limekiuwa likifanya hivyo ambapo kwa mwaka huu waraka huo umebeba wazo lisemalo "Kanisa katika Tanzania na Huduma ya upatanisho, Haki na Amani.

  Mwaka uliopita kanisa hilo kupitia chama chake cha wanataaluma Wakatoliki lilitoa ilani ya uchaguzi ambao ulivuta hisia za wengi na kuzua mjadala mzito kwa watu wa kada mbalimbali ikiwemo wabunge.

  Wakati huo huo Festo Polea na Tumsifu Sanga wanaripoti kuwa Umoja wa Wakristo Tanzania (CCT) kwa kushirikisha masheikh na wanaharakati mbalimbali wa kutetea sekta ya madini nchini wanatarajia kutoa waraka elekezi kwa wananchi utakaoelekeza jinsi wawekezaji wa madini wanavyoinyonya serikali na kusababisha wananchi wake kutonufaika na migodi hiyo.

  Waraka huo unatarajiwa kutolewa kabla ya uchaguzi ili wananchi waweze kutambua uwazi jinsi madini yao yanavyoibiwa na wahisani na kutoweza kuinufaisha serikali.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana Mwenyekiti wa Umoja huo, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Diyosisi ya Kaskazini Mashariki Dk Stephen Munga alisema waraka huo utaeleza taarifa zilizowazi kuhusu kiasi kinachochukuliwa na wawekezaji na kukipeleka nchini kwao huku serikali yetu ikikosa kunufaika.

  Alisema waraka huo utaweka wazi mambo yote ya madini kuanzia mwaka 2002 hadi 2010, huku akidai kuwa katika waraka huo wataeleza jinsi kila kampuni inatoa kiasi gani katika kodi na inapokea kiasi gani kwa kuwa nyingi zinadanganya.

  Habari zaidi soma=>Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010
   
 2. m

  mliberali JF-Expert Member

  #21
  Dec 30, 2017
  Joined: Jul 13, 2012
  Messages: 3,577
  Likes Received: 2,156
  Trophy Points: 280
  anacopy Rwanda kanchi ka watu mil5 wote wanajuana
   
 3. kayaman

  kayaman JF-Expert Member

  #22
  Dec 30, 2017
  Joined: Aug 3, 2013
  Messages: 3,017
  Likes Received: 4,683
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Awamu hii ni kusifia tu ukosoaji unatuvunjia amani yetu.
   
 4. mjingamimi

  mjingamimi JF-Expert Member

  #23
  Dec 30, 2017
  Joined: Aug 3, 2015
  Messages: 13,124
  Likes Received: 10,908
  Trophy Points: 280
  Bado ngoma Ngumu.
  Kakobe 3-0 ccm.
  Endeleeni kujaribu uenda mkachomoa hata goli moja.
   
 5. s8plus

  s8plus Member

  #24
  Dec 30, 2017
  Joined: Aug 14, 2017
  Messages: 24
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Wapo kimya sio kwa kumlipizia kisasi ila ni kuhofia their fate kama wakichagua upande
   
 6. m

  mliberali JF-Expert Member

  #25
  Dec 30, 2017
  Joined: Jul 13, 2012
  Messages: 3,577
  Likes Received: 2,156
  Trophy Points: 280
  Labda tuseme hivi kakobe mwanzo alikosea sasa amepatia, na pengo mwanzo alipatia sasa amekosea
   
 7. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #26
  Dec 30, 2017
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,408
  Likes Received: 1,084
  Trophy Points: 280
  Kanisa Katoliki halijawahi kuogopa superpower na ndilo lililoangusha Roma Empire, haliwezi kuogopa nchi changa.
   
 8. a

  ankai JF-Expert Member

  #27
  Dec 30, 2017
  Joined: Nov 25, 2017
  Messages: 703
  Likes Received: 633
  Trophy Points: 180
  Aaaah ivi aya yote yanatoka wapi Kwan kutubu ni sh ngapi jamani?
   
 9. A

  Augustino Fanuel Massongo JF-Expert Member

  #28
  Dec 30, 2017
  Joined: Dec 23, 2016
  Messages: 1,283
  Likes Received: 640
  Trophy Points: 280
  "Huwezi kulinganisha mlima Kilimanjaro na kichuguu" Bishop Kilaini.
   
 10. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #29
  Dec 30, 2017
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,345
  Likes Received: 2,224
  Trophy Points: 280
  kama kweli alikosea, kumbe maaskofu wetu wanalipiziana kisasi hata kama wanaona mambo yanaenda mrama!!!!
  ni wakati wa kushikamana...umoja wetu ndio nguvu yetu. Tukilala sasa tutalaliwa daima.
   
 11. lost id

  lost id JF-Expert Member

  #30
  Dec 30, 2017
  Joined: Aug 12, 2014
  Messages: 2,088
  Likes Received: 4,420
  Trophy Points: 280
  Pengo na baadhi ya wakatoliki wanajulikana kabisa ni wanafiki.

  Pengo alishapoteza moral authority ya kukemea jambo lolote. Kilaini ni fisadi wa escrow. Kati ya watu wanaotakiwa kuaa jela na kina Ruge Kilaini na baadhi ya maaskofu wa katoliki wanatakiwa kua jela.

  Pengo alikua mkali kwa sababu aliekua rais hakuna mtu wao, hakua mpokea ekaristi takatifu. Baadae pengo la kilaini wakapoozwa mlungula wa escrow wakanyamaza kimia.

  Pengo akaja kuibukia kwenye katiba mpya, akaharisha aliyoyaharisha kila mtu anajua.
   
 12. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #31
  Dec 30, 2017
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,408
  Likes Received: 1,084
  Trophy Points: 280
  Yeye anashambulia usalama wa TAIFA wakati ni kikundi badala ya kushambulia hoja. Sasa toka lini dini zikaogopa usalama wa taifa lolote.
   
 13. Copenhagen DN

  Copenhagen DN JF-Expert Member

  #32
  Dec 30, 2017
  Joined: Oct 5, 2014
  Messages: 5,967
  Likes Received: 8,158
  Trophy Points: 280
  LAZIMA LITUBU TUUU HAMNA NAMNA
   
 14. Chiwaso

  Chiwaso JF-Expert Member

  #33
  Dec 30, 2017
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 4,738
  Likes Received: 2,554
  Trophy Points: 280
  Ukipita kwenye ZEBRA usisahau kuwasha ''Hazard'' na kusimama kwa dk 4.
   
 15. P

  Pohamba JF-Expert Member

  #34
  Dec 30, 2017
  Joined: Jun 2, 2015
  Messages: 16,573
  Likes Received: 25,721
  Trophy Points: 280
  Polycarp anaanzaje kumkemea Joni?

  Sasa hivi tunasikia Kinafiki Kelele za Askof Mmoja Mmoja Kwanini hawatoi nyaraka rasmi za Kanisani Kama wakati ule wa 'Mdini na dhaifu wa Bagamoyo'?
   
 16. Copenhagen DN

  Copenhagen DN JF-Expert Member

  #35
  Dec 30, 2017
  Joined: Oct 5, 2014
  Messages: 5,967
  Likes Received: 8,158
  Trophy Points: 280
  Vyovyote vile LAZIMA LITUBU TUUU
   
 17. Copenhagen DN

  Copenhagen DN JF-Expert Member

  #36
  Dec 30, 2017
  Joined: Oct 5, 2014
  Messages: 5,967
  Likes Received: 8,158
  Trophy Points: 280
  vyovyote vile LAZIMA ATUBU TUUUU hamna namna
   
 18. nimbagonza

  nimbagonza JF-Expert Member

  #37
  Dec 30, 2017
  Joined: Jun 15, 2015
  Messages: 953
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 180
  Mwacheni baba wa watu aseme atakacho coz ni mtz na ana moyo anaguswa
   
 19. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #38
  Dec 30, 2017
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,408
  Likes Received: 1,084
  Trophy Points: 280
  Mkuu MODS, hii thread ya KAKOBE inapoletwa huku inakuwa shida ku-connect na mambo ya juzi. Watadhani ni mambo ya mwaka 2010.
   
 20. Gangongine

  Gangongine JF-Expert Member

  #39
  Dec 30, 2017
  Joined: Dec 31, 2015
  Messages: 3,866
  Likes Received: 1,756
  Trophy Points: 280
  Tunachunguza uraia wa Kakobe. Hana Dalili za Uraia
   
 21. Gangongine

  Gangongine JF-Expert Member

  #40
  Jan 1, 2018
  Joined: Dec 31, 2015
  Messages: 3,866
  Likes Received: 1,756
  Trophy Points: 280
  Wewe Kumbe fala!!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...