Maarifa ni dhahabu masomo ni tiba

Maarifa ni dhahabu masomo ni tiba

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,780
Reaction score
8,155
.
IMG-20250528-WA0045(1).jpg
Hebu angalieni hii picha, lakini msiishie kuiangalia, itazameni na mnapoitazama, itazameni kwa makini.

Kisha tafakari ujumbe ufuatao👇👇👇
Hivi unajua kwamba kila mmoja wetu hapa duniani amefanikiwa?

Yaani hakuna mtu duni, maskini, fukara, boya, lofa wala kenge.

Uduni, umaskini na ufukara tulio nao, huu uboya na ulofa mpaka tunaonekana kenge machoni pa watu, ni matokeo ya KUKOSA MAARIFA!

Maarifa ni nini?

Ni elimu sahihi, iliyodhibitika kuwa ni sahihi.

Hii elimu ikiingizwa kwenye matendo inakuwa maarifa na haya maarifa yakiendelezwa yanatupatia ufahamu na ufahamu ukiendelezwa unageuka uzoefu.

Mtu mwenye uzoefu katika kazi, taaluma, fani au jambo lolote, uwa anatumia nguvu kidogo sana kufanikiwa.

Mtu asiye na maarifa, hana ufahamu na bila ufahamu hakuna uzoefu na bila uzoefu basi katika kila jambo utatumia nguvu kubwa sana bila mafanikio au kwa mafanikio kidogo sana.

Ndio maana msingi wa mafanikio yoyote ni maarifa.

Jipatie maarifa ufanikiwe.

Pasipo maarifa hakuna mafanikio.

Darasa hili ni mahususi kwa ajili ya kupeana maarifa ya kiroho ambayo yakiendelezwa kwa kuyafanyia kazi yatainua kizazi cha watu waliofanikiwa kwenye nyanja mbalimbali za maisha.

"Knowledge is power" 👊🏻💪🏻👍👍👍
 
Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu ndipo mengine yoote mtazidishiwa.
Hapa Ina maanisha tafuteni maarifa ukiwa nayo utapata kila kitu ukitakacho duniani.
Kwa maana maarifa ni tiba ya matatizo yote.
Ukiweza badili mtazamo wako ndipo utaweza badili maisha yako.
 
Ufalme wa Mungu ni upi ? Naomba uthibitisho wa hili
Umo ndani yako kwa maana umeumbwa kwa mfano wa Mungu kwa maana una chembechembe za uungu ndani mwako thus umepewa uwezo wa kuumba chochote utakacho kupitia nguvu yako ya ndani inaitwa Uungu au sumaku uhitaji nguvu ya nje yaani booster kuwa wewe
 
Maandiko yanasema "Pesa ndio jawabu la mambo yote"
Tumia maarifa kupata pesa, nakubaliana na ww mkuu.
 
Back
Top Bottom