Maandamano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandamano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by John Mnyika, Oct 21, 2009.

 1. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #1
  Oct 21, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Kwa muda nimekuwa mbali na ulingo huu, nashukuru kwamba mijadala ya fikra mbadala inaendelea kwa kasi. Oktoba 14, niliongoza maandamano ya kumbukumbu ya Nyerere. Wapo waliunga mkono, wapo waliokosoa. Kwa wakosoaji, hoja mbili kubwa ziliibuliwa; mosi, kwa viongozi wa CHADEMA kumuenzi Mwalimu, na kwamba kumuenzi huko ni utamaduni ule ule wa kusifu na kuabudu viongozi. Ulikuwepo pia mtazamo kwamba kumuenzi kwa maandamano badala ya kufanya shughuli nyingine ni kupoteza muda. Katika kundi hilo, wapo waliopendekeza kwamba tulipaswa kumuenzi kwa njia nyingine mathalani kusafisha mazingira nk!.

  Tuliamua kufanya 'maandamano'(sio matembezi) kufikisha ujumbe mahususi wa mabadiliko. Kati ya mambo ambayo tulikuwa na ubishani na polisi ni kuomba kibali cha maandamano badala ya matembezi. Nashukuru kwamba polisi walitupa kibali, hata hivyo, nilieleza masikitiko yangu kuwa baada ya kutoa kibali na taarifa kuanza kusambaa; polisi hao hao wakaaandika barua nyingine ya kufuta kibali. Maelezo ya kikao nao ni kwamba maandamano yangepunguza 'attention' kwa hotuba ya rais Butiama, na pia ya kwamba siku ya Nyerere ni ya maombolezo ya kifo; hivyo si vyema kufanya maandamano. Tulikuwa na mjadala wa zaidi ya masaa kadhaa mpaka usiku. Nampongeza kamanda wa polisi mkoa, kwa kuwa hatimaye baadaye aliacha kutupatia barua ya kufuta maandamano. Nashukuru kwamba alitambua kwamba uamuzi wa kufuta maandamano yale ulikuwa kinyume cha katiba, na hakukuwa na sheria yoyote ambayo ilimpa mamlaka hayo(sheria inazungumza sababu za kiusalama).

  Tulifanya maandamano kwa lengo la kufikisha ujumbe, kwamba Nyerere anaenziwa kinafiki na watawala, na chama chao. Njia za kupitia maandamano hayo tulizipanga kwa sababu maalumu; maandamano hayo yalianzia Uwanja wa Tanganyika packers; pembeni ya magofu ya kiwanda ambao kilibeba maadhui ya sera za mwalimu za kuweka kipaumbele uzalishaji wa ndani. Magofu ya kiwanda kile, ni ishara ya sera mbovu za CCM ya sasa, za kutanguliza ubinafsi kwa kisingizio cha ubinafsishaji kuuza viwanda kwa bei chee. Na kugeuza nchi kuwa soko holela!.

  Tulipotoka hapo, tulipita Msasani/Mikocheni kwa Mwalimu, pale tulisimama kwa dakika moja kumkumbuka; pembeni yetu kikiwepo kiwanja cha wazi ambacho bila nguvu ya umma, tayari kilishatekwa kinyemela karibu kabisa na macho ya Nyerere!

  Tukaelekea mpaka Kinondoni; tukipita katika maeneo yanayowakilisha kuongezeka kwa pengo baina ya matajiri na masikini katika nchi yetu. Tukapita makao makuu ya chama, ilikuwa Dr Slaa atusalimu, lakini baada ya kuwa ameshasikia hotuba ya Kikwete na namna ambavyo aligeuza maadhimisho ya Nyerere ya kitaifa kuwa ya CCM, Dr Slaa akaamua kujiunga nasi kuendelea na maandamano ili kutoa ujumbe maalum.

  Tukafika ofisi ya Mkoa wa kichama wa Kinondoni ya CHADEMA, pale Dr Slaa akahutubia(Mwenye audio ya Hotuba yake atuwekee maana alisema maneno mazito sana kuhusu polisi, Kikwete na mwelekeo wa taifa)

  Kwa sababu mbalimbali, tulikatishia maandamano hapo; lakini itakumbukwa kwamba kwa mujibu wa ratiba niliyoisambaza awali; maandamano yalikuwa yaendelee kupitia Magomeni, Mburahati, Makurumla, Manzese mpaka Ubungo.

  Pale Magomeni, ilikuwa tusimame kwenye nyumba ya kwanza kabisa aliyoishi Mwalimu ambayo alipangishiwa na wazee wa Dar es es salaam wakati wa harakati za kudai uhuru. Ilikuwa tuwe na ujumbe maalumu pale, kuhusu mchango wa wazee wa Magomeni, Kinondoni na DSM kwa ujumla katika harakati za kudai uhuru. Na wajibu wao wakati huu katika kuleta mabadiliko baada ya misingi ya taifa hili kutikiswa na maadili kutekelezwa. Hata nyumba hii ambayo imebeba kumbukumbu ya historia kwa bahati mbaya nayo imeshavunjwa. Pale Urafiki, ilikuwa tusimame tena katika kukumbuka mchango wa Mwalimu; katika kujenga viwanda vyenye muunganiko wa mbele na nyuma(foward and backward) na sekta zetu za kiuchumi. Kiwanda cha nguo cha urafiki, sasa uzalishaji umepungua, mitambo mingine imeuzwa kama vyuma chakavu, nyumba za wafanyakazi zimeuzwa kinyemela; wafanyakazi wanateseka kwa maslahi duni; maghorofa yale yanakodishwa kwa watu tofauti kibiashara badala ya makusudio ya awali.

  Ilikuwa tusimame kituo cha mabasi Ubungo, pale ilikuwa tuweke bayana ufisadi wa pale na ukikukwaji wa sheria katika zabuni. CAG tayari alishakamilisha ripoti ya ukaguzi mpaka leo Waziri Mkuu Pinda ameikalia. Lakini nilidokeza nikiwa pale Kinondoni, UBT ni mfano wa namna ambavyo makada wa CCM wanaojigamba kumuenzi Mwalimu walivyomsaliti; mradi ule uko chini ya familia ya Kingunge Ngombare Mwiru; mwenye kujiita mjamaa, kumbe ni kiwakilishi cha tamaa za viongozi hao. Matokeo ya Maamuzi ya Zanzibar yaliyofukia miiko ya uongozi.

  Ilikuwa tutoke pale, tusonge mbele tukipita makao makuu ya msururu wa Majenereta ya umeme kuanzia Songas, Dowans nk; jirani kabisa na Makao Makuu ya TANESCO. Kiwakilishi cha CCM ya leo, wakati wa mwalimu aliona mbali na kuwekeza katika miradi ya muda mrefu ya nishati; CCM ya leo, inaendesha nchi kwa dharura; lakini pia njia ile ni ishara ya namna wananchi wanavyonywa katika sekta ya nishati ya umeme kupitia mikataba ya kifisadi kwa barakoa ya capacity charges nk. Pale ilkuwa turudie tena mwito wetu wa miaka kadhaa nyuma, wa kutaka mitambo ile ya Dowans itaifishwe; wakati huo huo taifa lichague uongozi na sera mbadala zitakazosimamia uwekezaji wa muda mrefu katika sekta ya nishati wa taifa letu.

  Naandika ujumbe huu leo; kwa sababu bado naamani, maandamano yale yanapaswa kuendelea; kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere haipaswi kuwa ya siku moja, ni suala endelevu kwa vitendo. Naandika ujumbe huu kuuliza kama kuna ambao wako tayari kuunga mkono maandamano haya ya safari ya pili kufikisha ujumbe huu.

  Naandika ujumbe huu mgao wa umeme ukiwa unaendelea; naandika ujumbe huu ikiwa Zitto na viongozi wengine wamerudia tena mwito wa kutaka mitambo ile itaifishwe. Naandika ujumbe huu nikijua kwamba tunahitaji masuluhisho ya muda mfupi ya dharura, lakini pia tunahitaji kufikiria masuluhisho ya muda mrefu. Kuna ambaye yupo tayari kuandamana? Iwe kwa yeye mwenyewe au kuwezesha watanzania wengine kuandamana? Tafadhali tuwasiliane kupitia 0784222222 au mnyika@yahoo.com. Tunaweza tukatoa matamko kwenye vyombo vya habari, tunaweza tukajenga hoja bungeni, tunaweza tujadili kwenye makongamano. lakini tukumbuke pia, tunawajibu wa kuunganisha nguvu ya umma. Maandamano ni njia mojawapo ya kufikia azma hiyo. Iwe ni maandamano ya kulaani ama kutoa ujumbe mbadala. Iwe ni kuonyesha hasira ya kutopata tunachostahili kupata ama ni kushinikiza kupata tunachopaswa kupata. Tukubali kuwa mawakala wa mabadiliko tunayotarajia kuyaona. Pamoja tunaweza!

  JJ
   
 2. K

  Koba JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  Mnyika ni kweli utagombea ubunge wa Ubungo?
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mie nafikiri mnadai mengi sana hadi mtu unachanganyikiwa mnadai kipi.

  Kwa sasa mngeelekeza nguvu zenu kwanza kwenye UMEME na mchukue point kadhaa. Haya ya UDA, KAMATA, Kingunge nk yanakuwa mengi sana.

  Ushauri wangu ni kuwa muwe kama SIMBA kwenye kundi la nyumbu/Pundamilia. Akishagundua mnyama fulani ni selule (goigoi) basi huweka atention yake yote kwa huyo mmoja. Pundamilia huwa wanakimbia Zigzag ili kumchanganya simba apoteze shabaha. Ila mie hapa naona nyie wenyewe mnajikimbiza Zigzag na mwisho mtawapa watu kizunguzungu.

  Tafuteni kitu kimoja mnashambulia hadi kinaeleweka. Na kwa sababu watu wanaipata habari ya Mgawo, nafikiri hili hata mseme kila siku basi watu watalisikiliza. Kazi kwenu na kazi njema.
   
 4. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Polisi walikosea kudhani Siku ya Nyerere ni siku ya maombolezo. Hatuombolezi kifo miaka kumi. Sasa tunashangilia mchango wa Mwalimu kwa Taifa. Kwani JK alipokwenda Butiama alikwenda kwenye matanga? Hapana, alikwenda kwenye sherehe ya kumkumbuka Mwalimu.

  Kwa wenye imani ni hivi: On the day that he died, Mwalimu was born into heaven. That is why we celebrate his life on that day rather than on the day he was born into "this vale of tears".

  Ilikuwa ni sahihi sana kwa CHADEMA kukumbushia mchango wa Mwalimu kwa maandamano. Polisi wanaogopa mno CCM!
   
 5. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mkuu huwa nakukubali kabisa kwa mawazo yako na nini imani Mungu atakusimamia katika mapigano tuko pamoja daima.Usikate tamaa tuko pamoja.
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  John,

  Nakupongeza sana kwa kuwasiliana nasi na kutupa angalau kwa ufupi mawazo yako. Ni jambo jema sana.

  Kama alivyosema ndugu yetu hapo chini, naomba mjaribu kujipanga ili kuwa na ujumbe wenye mwelekeo, usiopwaya. Kwa sababu akili ya watu wengi haiwezi kumeza mambo mengi kwa wakati mmoja. Tumia nafasi hii kushikilia suala la umeme ambalo kwa sasa lina mshiko kwa kila mtu na tayari JK ndiye amewekwa katika ya hicho kizungumkuti. Just hit the bull!

  Mwisho naomba sana jitahidi kuonesha kuwa wewe na wenzako ni viongozi. Sidhani kama ni busara kuwauliza watu unaowaongoza na hasa katika mazingira yetu kama wako tayari kuandamana. Kwa sirika ya Watanzania wengi watakukatisha tamaa. Nashauri uje na mpango kamili wa kitu gani unapendekeza kifanyike, mfano maandamano ya kupinga mgawo wa umeme na uzembe wa JK na mimi naamini watu watajitokeza tu.

  Kila la heri na endelea na kazi nzuri.
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Watu wengine bana si uPM akujibu huko huko
   
 8. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Nyie mnatakiwa kufanya maandamano kutaka mabadiliko ya kikatiba na kutaka umeme wa uhakika, siyo kumuenzi Nyerere ambaye alianzisha matatizo yetu yote.

  Siasa za upinzani Tanzania haziwezi kukomaa mpaka wapinzani watakapopata guts za kum repudiate Nyerere na kusema mabaya yake.
   
 9. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tueleweshwe msimamo wa CHADEMA kuhusu dowans kwani tokea mapema mlikaa kimya!

  Maandamano ngoma mtakayopiga sisi tutacheza.
   
 10. K

  Koba JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ..hivi wewe unataka kutukanwa tuu au?
   
 11. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,375
  Likes Received: 3,139
  Trophy Points: 280
  viongozi waliandamana ili kutimiza neno ```tumuenzi mwalimu`` lakini ni watu waliomsaliti nyerere kwa kiasi cha ajabu...............
   
 12. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,503
  Trophy Points: 280
  Bwana Mnyika, kwa hali halisi ya umeme ilivyo, mi naamini kabisa viongozi wa CHADEMA mkiamua kuhamasiah umma..japo hata wa DSM tu, you will make a big difference...hamasisheni watu waandamane kwamba kwa nini hawana umeme...hilo tu kwanza. Mkifanikiwa hilo, mtaona mambo yatakavokuwa mteremko..

  Hizo helikopta alizonunua Mh Ndesamburo hazitasaidia sana kama wananchi hawatakuwa wamepata hamasa na kuwaamini wala kwa muda mrefu wa kutosha!

  hebu someno mbinu za Obama..mwenzenu ameanza kampeni tangu akiwa kwen 20s. nadhani umesoma master peace yake 'Dreams from My Father'...mngeweza kuazima mawazo mawili matatu kuhusu 'community organizations and the organization process'
   
 13. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  watu wengi wanalalamika kuhusu utendaji wa kazi katika CCM na enzi za nyerere na kufikiria kuwa Chedema wata-make change....viongozi wenyewe wa chedema wametoka CCM what are youe xpecting kila mtu in Tanzania anafikiria kujinufaisha mwenyewe na wala siyo nchi yake....Watu wanapiga kelele sana na siku wakija kupewa uongozi you will tell me Kaizer....kutakuwa hakuna mabadiliko kabisa......Kila mtu Tanzania ni Fisadi si CCM si chadema si NCCR -Mgaeuzi.....
   
 14. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2009
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Marehemu Mwl Nyerere katuachia katiba mbaya,nashukuru mungu hata yeye binafsi aliwahi kunukuliwa akisema kama angetaka kuwa dictator kwa katiba ya Tanzania angeweza kuwa bila matatizo.

  Namshangaa sana Mnyika na CHADEMA yake wasivyokuwa na akili kumshabikia mtu aliyetengeneza katiba ya kumfanya rais wa Tanzania Mungu mtu???????????.

  Wapinzani wote kwa pamoja tupiganie katiba mpya.

   
 15. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #15
  Oct 22, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  You really have a dark view of Tanzanians. Wako viongozi chungu nzima Bongo ambao sio fisadi. Unadhani Dr. Slaa ni fisadi? Yeye ni sumu ya mafisadi. Na hayuko mwenyewe. Watanzania wengi wenye uwezo wa uongozi sio fisaidi. Hata wewe nadhani sio fisadi.

  Tuna uhakika wa kuangamia zaidi kama tutaichagua tena CCM. Ila tukiichagua Chadema, kuna uwezekano mkubwa wa kubadilika kabisa. Huoni ni bora kuongozwa na watu kama Slaa badala ya hawa wa sasa?
   
 16. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #16
  Oct 22, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  A war consist of many battles. Si kosa kwa chama kinachopigania katiba mpya kuongoza maandamano ya kumkumbuka Nyerere.


  Kuna makosa alifanya Mwalimu, lakini yako mengi mazuri ambayo aliyafanya vile vile. Alijenga taifa lenye umoja. For that, he is The Father of the Nation. You cannot take that away from him.
   
Loading...