Maandamano yaibuka upya Beirut

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,362
Reaction score
4,817
Ghasia zimeibuka tena katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut, ambapo vikosi vya usalama vimetumia gesi ya kutoa machozi na mizinga ya maji dhidi ya waandamanaji ambao walikuwa wakirusha chupa na mabomu ya kienyeji karibu na jengo la bunge.

Idadi kubwa wa watu walijeruhiwa katika kadhia hiyo ya Jumapili. Hali hii ya maandamano ya kulipinga kundi la wanasiasa walio katika hatamu ya uongozi imekuwa ikiendelea tangu katikati mwa mwezi Oktoba.

Safari hii waandamanaji wanapinga waziri mkuu aliyejizulu Saad Hariri akirejea tena katika serikali itakayoundwa. Wanataka kiongozi huru kabisa ambaye hana muingiliano na vyama vya kisiasa nchini humo.



Chanzo: DW Swahili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…