FisadiKuu
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 8,164
- 13,437
Kuna mlipuko mkubwa sana umetokea Lebanon muda si mrefu, inasemekana silaha na milipuko ya Hezbolah ndio imeharibiwa na intelijensia ya Israel..
Picha linaendelea..
====
Mlipuko mkubwa umepiga mji mkuu wa Lebanon, Beirut, huku kukiwa hakuna uthibitisho kuhusu mlipuko wa pili
Mlipuko mkubwa umetokea mjini Beirut wakati kukitarajiwa uamuzi kuhusu kesi ya mauaji ya Waziri Mkuu wa zamani Rafik Hariri mwaka 2005.
Ripoti zinasema kuwa mlipuko mkubwa umetokea kwenye eneo la bandari la mji huo, huku kukiwa hakuna ripoti za kutokea kwa mlipuko wa pili. Mamlaka zinahofu kutokea kwa madhara makubwa.
Video iliyowekwa mtandaoni imeonesha uharibifu mkubwa uliotokana na mlipuko huo.
Mahakama ya Umoja wa Mataifa inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu kesi ya washukiwa wanne wanaoshukiwa kuhusika na mauaji ya bwana Hariri.
Wafuasi wote wanne wa kundi la Hezbollah, wamekuwa wakikana kuhusika na kifo cha Hariri. Uamuzi wa mahakama utatolewa siku ya Ijumaa
Ripoti kuhusu uwezekano wa kutokea mlipuko wa pili katika makazi ya bwana Hariri imetolewa.
Waziri wa afya wa Lebanon Hamad Hasan amezungumzia kuhusu majeruhi wengi na uharibifu mkubwa uliojitokeza.
Shirika la habari la Reuters limenukuu vyanzo vya habari vikisema miili kumi imetolewa kutoka kweny kifusi.
Vyombo vya habari nchini humo vieonesha watu wakiwa wamenasa kwenye vifusi. Shuhuda akieleza jinsi mlipuko huo wa kwanza ulivyokuwa wa kishindo na sauti kubwa.
Sababu ya mlipuko huo bado haijafahamika.
Ripoti hii imekuja wakati kukiwa na mvutano wa kisiasa nchiniLebanon, huku maandamano yakitokea mitaani dhidi ya serikali kuhusu namna wanavyoshughulikia changamoto za kiuchumi tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 1975-1990.
UPDATES
WATU ZAIDI YA 25 WAFARIKI DUNIA KATIKA MLIPUKO WA BEIRUT, LEBANON
Takriban watu 25 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 2,500 wamejeruhiwa katika mlipuko huo ambao chanzo hakijafahamika
Mlipuko huo umetokea katika eneo la bandari la Beirut
UPDATES
Waziri wa Afya, Hamad Hassan amesema Watu zaidi ya 50 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 2,750 wamejeruhiwa kufuatia mlipuko uliotokea eneo la bandari ya mji huo
Mlipuko huo pia umetuma mawimbi yaliyosababisha majengo mengi mbali na eneo la mlipuko, kutikisika, kuvunjika madirisha na milango
UPDATE
WATU 78 WAMEFARIKI KATIKA MLIPUKO WA BEIRUT, LEBANON
Kwa mujibu wa taarifa za Mamlaka nchini humo Watu 78 wamefariki dunia na wengine 4,000 wamejeruhiwa katika mlipuko uliotokea eneo la bandari ya mji huo
Huku shughuli za uokoaji zikiendelea, Waziri wa Afya, Hamad Hassan amesema kuna watu wengi hawajulikani walipo na ni vigimu kuwatafuta usiku kwa kuwa hakuna umeme
Mlipuko huo ulituma mawimbi yaliyoathiri majengo umbali wa Kilometa 10 kutoka eneo la mlipuko, milango na madirisha yalivunjika. Mji umejaa vioo vilivyovunjika kwenye majengo
Waziri Mkuu wa Lebanon, Hassan Doab amesema takriban tani 2,750 za Ammonium Nitrate (inayoweza kulipuka) zilizokuwa zimehifadhiwa katika ghala moja kwa miaka 6. Amesema uhifadhi huo haukubaliki na ametaka uchunguzi ufanyike kujua chanzo cha mlipuko na majibu yatoke ndani ya siku 5
Ammonium nitrate ni muhimu katika utengenezaji wa mbolea na vifaa vya milipuko. Imewahi pia kutumika katika mashambulio ya kigaidi likiwemo shambulio la ‘Alfred P. Murrah Federal Building’ katika mji wa Oklahoma mwaka 1995
Katika hatua nyingine, Maafisa wa Lebanon wameonesha kushtushwa baada ya Wanadiplomasia wa Marekani kuuita mlipuko huo ‘shambulio’ kufuatia Rais Trump kuuita hivyo katika mkutano wake na Waandishi wa habari
UPDATE
WALIOFARIKI KWENYE MLIPUKO WA BEIRUT WAFIKIA 135
Baraza la Mawaziri la Lebanon limetangaza wiki 2 za hali ya dharura katika mji wa #Beirut na kulipa Jeshi udhibiti wa usalama kufuatia mlipuko ulioua Watu 135 na kujeruhi wengine 5,000
Mamlaka zinasema zinatarajia idadi ya vifo kuongezeka wakati huu ambao Waokoaji wanaendelea kufukua vifusi vya majengo kutafuta walionusurika vifo katika tukio hilo
Gavana wa Beirut, Marwan Abboud amesema Watu 300,000 wamepoteza makazi na Mamlaka zinafanya kazi ili kuwapatia watu hao chakula, maji na malazi
Chanzo cha mlipuko huo bado hakifahamika. Maafisa wanahusisha mlipuko huo na tani 2,750 za Ammonium Nitrate iliyokuwa imehifadhiwa kwa miaka 6 katika ghala moja katika eneo la bandari palipotokea mlipuko
UPDATE
SERIKALI ILITAHADHARISHWA KUHUSU MLIPUKO ULIOUA WATU ZAIDI YA 100
Serikali ya Lebanon inalaumiwa kwa kupuuza maonyo yaliyopelekea mlipuko kuua watu 135 huku wengine zaidi ya 5,000 wakijeruhiwa na takribani watu 300,000 wameharibiwa makazi yao
Maafisa wa Beirut, bandari ambayo mlipuko umetokea waliliona janga hilo na kutoa onyo mara kwa mara. Miezi sita iliyopita maafisa waliichunguza bohari yenye ammonium nitrate na kuonya kuwa isipoondolewa itailipua Bairuti yote
Waziri Mkuu wa Lebanon, Saad Hariri amelaumiwa kwa tukio hilo. Serikali hiyo imeshatangaza wiki mbili za hali ya tahadhari na kuwapa ngovu jeshi kufanya kazi kiufanisi kwa muda huo
Idadi ya waliofariki na majeruhi inaweza kuendelea kuongezeka kwa kuwa bado kuna watu hawajulikani walipo. Linapoendelea suala la kufukua kujua madhara zaidi linaweza kuibua vifo au majeruhi zaidi wa mlipuko huo
UPDATES
RAIS WA LEBANON ASEMA UZEMBE AU KOMBORA YAWEZA KUWA CHANZO CHA MLIPUKO
Rais wa Lebanon, Michel Aoun amesema mlipuko uliosababisha vifo vya watu 157 na kufanya uharibifu mkubwa mjini #Beirut huenda ulisababishwa na uzembe au shambulio la roketi kutoka nje
Aoun ameahidi kufanyika kwa uchunguzi kamili juu ya tukio hilo huku tayari Maafisa 20 wa bandari wakikamatwa kama sehemu ya uchunguzi huo
Aidha, Benki Kuu nchini humo imesema imezizuia akaunti za washukiwa 7, akiwemo Wakuu wa bandari na forodha
Mlipuko huo unahusishwa na Ammonium Nitrate iliyokuwa imehifadhiwa katika ghala kwa miaka 6 huku Serikali ikionywa kuhusu hilo miezi 6 nyuma
UPDATES
LEBANON: MLIPUKO WA BEIRUT WAPELEKEA MAWAZIRI, WABUNGE KUJIUZULU
Waziri wa Habari, Manal Abdel Samad na Waziri wa Mazingira, Damianos Kattar wamejiuzulu kufuatia mlipuko wa Agosti 04 uliosababisha vifo 157 na majeruhi 6,000
Kufuatia mlipuko huo uliotokea eneo la bandari ya mji wa Beirut, maelfu ya wananchi waliandamana mwishoni mwa wiki iliyopita kushinikiza viongozi kujiuzulu
Katika taarifa yake, Manal amesema anajiuzulu kwa heshima ya waliopoteza maisha, waliojeruhiwa na ambao hawajulikani walipo. Pia, ameongeza kuwa amefanya hivyo kuitikia wito wa wananchi kutaka mabadiliko
Mbali na Mawaziri hao, Wabunge wapatao 9 nchini humo wamejiuzulu tangu kutokea kwa mlipuko huo ambao umepelekea watu wapatao 300,000 kukosa makazi
Wataalamu wanakadiriwa kuwa mlipuko huo umesababisha hasara ya takriban Dola Bilioni 15