Maandamano ya wasanii ruksa, vyama vya siasa hapana..!

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,685
1,111
Kwa nini tuna andamana,tunadai haki yetu na kuonyesha hisia zetu kwa kufikisha ujumbe wa hisia zetu kwa jamii husika kwa njia ya maandamano tukiwa na lengo la kudai haki yetu.

Iweje maandamano ya wasanii kudai haki zao za kazi ya mikono yao yawe halali lakini maandamano na mikusanyiko ya kisiasa ionekane si halali!?

Kuna shida ndani ya taifa letu,haiwezekani haki ile ile iwe halali kwa kundi fulani kwa sheria ile ile iliyoruhusu mkusanyiko lakini kwa mantiki hiyo hiyo kundi lingine lionekane halina haki ya kukusanyika wala kuandamana.

Tumefikia hapa kwa kuwa tumekuwa mbumbumbu wa kuisoma katiba na kama tunaisoma hatujui tafsiri ya katiba ndiyo maana tuna gawanywa kwa matabaka ya wenye haki na wasio na haki.

Mikutano ya kisiasa na maandamano yapo kisheria,unaposimama na kukataza shughuli hizo sikuwa unaivunja sheria tu bali unaikanyaga katiba na kuitawala nchi kwa utashi wako binafsi.

Tumeambiwa tuheshimu mamlaka ya watawala,watawala ili wapate dhamana ya kutuongoza lazima waheshimu katiba,iweje leo tuheshimu mamlaka ya watawala ikiwa watawala hawataki kuheshimu katiba!?

Kwa mantiki hiyo wote tunaoshindwa kuheshimu mamlaka za watawala na watawala wanaoshindwa kuheshimu mamlaka ya kikatiba ni vilaza. Na kutokana na ukilaza wetu leo tumekubali mikopo yetu ya elimu ya juu kukatwa kwenye mishahara yetu kwa 15% ilihali mikataba yetu ilikuwa 8%. Tumekubali kutekeleza utashi wa mtu mmoja bila kuzingatia mkataba wa kisheria,kama tumeshindwa kuisimamia sheria tumekuwa wahanga wa matumbo yetu kwa kutekeleza wajibu bila haki.

Vyama vya siasa vipo kisheria kwa mujibu wa katiba yetu, vikiongozwa na kanuni ya vyama vya siasa ya mwaka 1992,ajabu vyama hivi vimezuiliwa kufanya kàzi zake zilizokubaliwa kisheria kwa hofu ya utashi wa mtu mmoja,lakini wasanii wamesimamia haki hiyo hiyo ya kikatiba wameandamana na kukusanyika kisha tunasema haki sawa,usawa unatoka wapi?

Mbomoa nchi ni mwananchi na mjenga nchi ni mwananchi pia, tukiendelea kuikumbatia batili kwa kuiogopa haki kwa matakwa ya utashi wa mtu tutaliangamiza taifa kwa uvivu wa kufikiri na uoga wa kutenda,kila mmoja atekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria katika kutekeleza majukumu yetu ya kila siku,tukiacha utashi kuwa sheria iko siku tutaulizwa mmeitendea nini Tanzania.
 
Diamond.jpg


 
Habari wakuu!
Kwa kawaida maandamano yoyote Yale lazima yawe na kibari maalumu kutoka polisi. Je bashit.e na Wasanii Wa bongo movie walikuwa na kibari cha kufanya maandamano? Tunaomba nakala ipigwe picha na kutupiwa humu
 
Makonda alitoa kibali ili wakamuunge mkono kupiga marufuku movies za nje, na ndiyo maana walianzia ofisini kwake
 
Habari wakuu!
Kwa kawaida maandamano yoyote Yale lazima yawe na kibari maalumu kutoka polisi. Je bashit.e na Wasanii Wa bongo movie walikuwa na kibari cha kufanya maandamano? Tunaomba nakala ipigwe picha na kutupiwa humu
Hata mtoto wangu yule wa KG 1 anakushinda kuandika...(KIBARI) ndio nini...!!??
 
Mkuu nilimuona siro pale kwenye mkutano
Lazima itakuwa linabaraka zake
 
Maandamano dhidi ya machinga? Au dhidi ya nani? Nani anatakiwa kupokea ujumbe wa maandamano na kuufanyia Kazi? Tukisema Zero is empty wanachachamaa lakini kweli hili linaweza kufanywa na kiongozi timamu?
 
Yote hii analazimisha kuandikwa na magazeti kesho. Mwendo mdundo, apuuzwe, hakuna kumwandika. Asubiri uhuru gazeti
 
Maandamano lazima yawe ya kuunga mkono basi. Hoja tofauti na wafalme hazikubaliwi maana wanafanya kazi kwa manufaa ya "wanyonge"
 
Kitu chochote anachofanya Bashite ni halali..Hata kutumia hela na mali za watu binafsi kukarabati ofisi za Serikali ni halali kwake..Ila fanya wewe ndugu uone
 
Maandamano dhidi ya machinga? Au dhidi ya nani? Nani anatakiwa kupokea ujumbe wa maandamano na kuufanyia Kazi? Tukisema Zero is empty wanachachamaa lakini kweli hili linaweza kufanywa na kiongozi timamu?
Bashite aliandamana akajipokea mwenyewe.
FB_IMG_1492680554934.jpg
 
Back
Top Bottom