Waislamu wasitisha maandamano
Friday, 23 December 2011
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wahadhiri wa Kiislam, Yahaya Juma Yahaya alitoa tamko hilo kupitia TBC1 akisema maandamano makubwa yaliyokuwa yamepangwa kufanyika nchi nzima yameahirishwa kutokana na maafa hayo makubwa yaliyoikumba nchi.
Haitakuwa jambo la busara na hekima kuandamana huku ndugu zetu waliokufa kutokana na mafuriko wakiwa wanazikwa. Jumuiya yetu imeona ni vyema kusitisha maandamano haya na kujumuika katika maombolezo na kuwafariji walio fikwa na maafa haya.
.