Maandamano ya waislamu yaota mbawa...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandamano ya waislamu yaota mbawa...?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Dec 25, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  Waislamu wasitisha maandamano
  Friday, 23 December 2011

  Abdallah Mdangwe na Danieli Rutoryo

  JUMUIYA ya Wahadhiri wa Kiislamu imesitisha maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika jana kutokana na maafa yaliyowapata wakazi wa jiji la Dar es Salaam, yaliyo sababishwa na mvua zilizonyesha hapa jijini na baadhi ya mikoa nchini.

  Maandamano hayo yalikuwa yamedhamiria kupinga maridhiano baina ya serikali na jumuiya za Kikristo na pia, kuishinikiza serikali kulipatia ufumbuzi suala la mahakama ya kadhi kwani limechukua muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi.

  Mwenyekiti wa Jumuia ya Wahadhiri wa Kiislam, Yahaya Juma Yahaya alitoa tamko hilo kupitia TBC1 akisema maandamano makubwa yaliyokuwa yamepangwa kufanyika nchi nzima yameahirishwa kutokana na maafa hayo makubwa yaliyoikumba nchi.

  “Haitakuwa jambo la busara na hekima kuandamana huku ndugu zetu waliokufa kutokana na mafuriko wakiwa wanazikwa. Jumuiya yetu imeona ni vyema kusitisha maandamano haya na kujumuika katika maombolezo na kuwafariji walio fikwa na maafa haya”.

  Aliongeza, “Kwa wenzetu walioko mikoani hususani mikoa 18 iliyohusishwa na maandamano haya taratibu zimeshachukuliwa kuhakikisha viongozi wa Kiislam wanawapa waumini taarifa hii kwani sitisho hili si kwa Dar es Salaam pekee bali ni kwa nchi nzima sababu janga hili ni la kitaifa.”

  Mwananchi ilifika katika ofisi za Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu iliyoko katika Manispaa ya Temeke, Msikiti wa Tungi na kukuta watu wakiendelea na shughuli zao kama kawaida, kwani eneo hilo lilipangwa kuanzia maandamano hayo.

  Katibu wa Baraza hilo la Jumuiya za Waislamu, Sheikh Mubaraka Daluweshi alisema maandamano yameahairishwa kutokana na hali halisi ya wananchi kwani idadi kubwa ya wakazi wa hapa jijini ni Waislamu haitakuwa vyema yakafanyika maandamano wakati maiti zikiwa majumbani kwao.

  “Kutokana na hali halisi ya wananchi asilimia 80 ya wakazi wa jijini hapa ni Waislamu haitakuwa vyema yakafanyika maandamano huku jamii ikiwa kwenye matatizo makubwa kama haya leo tutajumuika na wenzetu katika mazishi,’’ alifafanua shehe Daluweshi.

  Daluweshi hakuweza kutoa taarifa juu ya maandamano haya kama yatapangwa kufanyika tena au la na kudai kuwa yeye si msemaji wa suala hilo, msemaji ni Katibu Mwenezi wa baraza hilo ambae jitihada za kumpata ziligonga mwamba.

  Hata hivyo, tayari Baraza la Kuu la Waislamu (Bakwata) mkoa wa Dar es salaam kupitia shehe wake wa mkoa, Alhad Musa Salim limewapongeza Waislamu wote hapa nchini kwa kukubali kusitisha maandamano na kuwataka kuungana pamoja na Bakwata katika kutetea maslahi ya Waislamu.

  “Tunapaswa kushirikiana kwa pamoja kwani sisi sote tunalengo moja tu kutetea, kulinda na kudai haki za Waislamu mahali popote. Sisi Baraza Kuu la Waislamu tunawaomba Waislamu kuwa na subira kwani tatizo la mahakama ya kadhi lipo katika hatua za mwisho kiutatuzi,’’ alifafanua.

  Salim alisema Bakwata ipo pamoja na wananchi wote walioathiriwa na mafuriko na pia amewataka wananchi walio poteza ndugu zao kutokana na mafuriko haya kuwa na moyo wa subira hususani katika kipindi hiki kigumukwani Baraza hilo litashrikiana nao kwa hali na mali.
   
 2. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Eti 80% ya wakazi wa DSM ni Waislamu? Hiyo sensa ilifanyika lini?
   
 3. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Halafu umeona walivyo wabaguzi! Ingekuwa (kama ni kweli) 30% ni waislamu wangeandamana.

  Hawa watu wanachefua na wanaharibia majority ya waislamu wastaarabh!

  Najivunia sana kuwa Mkristu wa kikatoliki!
   
 4. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #4
  Dec 25, 2011
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  hawana jipya zaidi kufuga mandevu na kupandisha suruali
   
 5. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Hawa ni mazuzu,wameshapewa go ahead ya kuanzisha hiyo mahakama ya kadhi,na serikali imesema watumie pesa zao ktk kila kitu juu ya unzishwaji na kuiendesha hiyo mahakama sasa cjui wanataka kumwagiwa maji na vijana wa Kova? Haya sie yetu macho
   
 6. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #6
  Dec 25, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,277
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Wanabeep tu hawawezi kitu, walisema wangeandamana Zanzibar wakatishwa kidogo wakaogopa, juzi tena wameogopa...

  Hawawezi kuandamana hawa
   
 7. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #7
  Dec 25, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  Upuuzi huu kama usingedhibitiwa ungewadhalilisha waislam wote!
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Dec 25, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  wangewacha waandamane tu, they had a message to deliver
   
 9. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #9
  Dec 25, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Amepitiwa nadhani alitaka kusema 80% ya wakazi wa Temeke. Which may be very possible, lakini jiji lote, labda anatumia sensa ya 1930.
   
 10. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #10
  Dec 25, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mimi ni Muislam ila Maandamano haya ya Kipuuzi siyaungi Mkono kabisa. Niliwaambia hata wenzangu Ijumaa tulipokuwa Msikitini lakini wakaanza kuniponda mara Ooh kwa vile Mke wangu ni Mkristo, Ooh kwa vile nimepanga nyumba ya Mkristo, nk. Nikaawaaambia kama ni hivyo mbona bado sijasilimu?
   
 11. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #11
  Dec 25, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hiyo ni sensa ya msikitini sio ya jiji!
   
 12. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #12
  Dec 25, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mahakama ya kadhi, mkulu ameshatoa ruhusa, shida nini bandugu???
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Dec 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  sijui hizo takwimu nawe umezipata wapi.................ingawaje hata kama..........TZ is 4 all of us too........
   
 14. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #14
  Dec 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  shida ni hela za wafadhili.............................kuelekezwa kwingineko........................ingawaje wafadhili hao ni walipa kodi wa nchi za Kikristu.....
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Dec 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  Tubarikiwe sote.......................
   
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  Dec 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  tukishayasahau mafuriko watarudia khoja yao..................................itasikilizwa lakii kwa vile iko nje ya uwezo wetu basi itawekwa kapuni........
   
 17. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #17
  Dec 25, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  They normally pick any number that sounds good to them, claiming it is the actual and correct figure.
  Sasa utaona, baada ya hapa, kila watakapoongelea DSM muslims, watakuwa wanadai hivyo hivyo, na wengine hata watasema ni zaidi ya asilimia 80.
   
 18. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #18
  Dec 25, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wanaweza sana kuandamana hadi kuchoma bendera, hivi sasa wako kwenye dilemma maana aliyoko madarakani ni ustaadh, sasa wakiandamana wataonekana wanampinga ustaadh na mikakati yake ya kuwaimarisha. Kama unataka kusikia Takbir, subiri siku kafir atakapo kabidhiwa funguo za magogoni.
   
 19. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #19
  Dec 25, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,603
  Likes Received: 6,770
  Trophy Points: 280
  kuandamana ni haki ya msingi ya kila raia ili mradi hazivunjwi sheria za nchi, na ili mradi sheria zenyewe ziwe halali na si za kibaguzi
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Dec 25, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  HAO, HAWA, THEY, THEM, WALE, - Muslim..
  SISI - Wakristu.....

  Kaazi kweli kweli.....
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...