Maandamano ya Mtwara yana mengi zaidi ya Gesi

Maandamano ya Mtwara yana mengi zaidi ya Gesi

Gwakukaja85

Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
17
Reaction score
12
Kwa mtu aliyetembelea na kuishi mikoa ya kusini atakubaliana nami kuwa maisha ya mikoa ya Mtwara na Lindi ni karibu na "jehanamu."Nasema hivyo ni kiwa na maana ya kwamba Wananchi karibia 90% hawapati huduma za kijamii,mfano

1:MAJI suala la maji huko Mtwara hasa halmashauri za Newala, Masasi vijijini, Tandahimba wanateseka mno kipindi cha kiangazi. Baadhi ya wananchi wa Newala katika vijiji vya Mikumbi, Mnyambe, Makukwe kwenye mikutano ya hadhara na Mbunge wao walimuuliza suala la maji akawajibu yeye siyo chura hivyo hajui shida ya maji.

2:Umeme ndiyo kabisa vijijini hakuna unawaka mjini tu.

3:Ununuzi wa korosho ni shida tupu. Wananchi wengi wanategemea korosho kama zao kuu la biashara lakini cha ajabu hawafaidiki na zao hilo,wengi wao wanakopesha kwenye vyama vya msingi na malipo hayafanyiki kwa wakati. Wananchi wamekata tamaa na serikali
yao.

Hivyo basi mkombozi pekee hasa kwa vijana ilikuwa ni uzalishaji wa gesi. Kwa mbunge wa kusini kuiacha gesi ipelekwe Dar-Es-Salaam ni kuitelekeza kusini, hakuna haja ya kujenga viwanda Dar-Es-Salaam tu. Hata huku kusini tunahitaji viwanda ili kukuza uchumi wa huku.
Jamaani mikoa ya kusini ina shida nyingi sana na imetelekeza kwa muda mrefu mpaka huwa najiuliza huku keki ya taifa watakula lini? Na ile Mtwara corridor enzi za Rais Mkapa imekwenda wapi? Barabara za Nachingwea-Masasi, Masasi-Newala- Tandahmba, Mtwara vijijini-Luangwa, zitajengwa lini?

Watu wa kusini hawana majibu na wabunge wao nao hawana habari kabisaa. Change ni mimi na wewe hivyo endeleeni kudai watu wa Mtwara.

Bravo Mtwara's peoples.
 
Kwa mtu aliyetembelea na kuishi mikoa ya kusini atakubaliana nami kuwa maisha ya mikoa ya mtwara na lindi ni karibu na "jehanamu."Nasema hivyo ni kiwa na maana ya kwamba Wananchi karibia 90% hawapati huduma za kijamii,mfano 1:MAJI suala la maji huko mtwara hasa halmashauri za newala,masasi vijijini,tandahimba wanateseka mno kipindi cha kiangazi.Baadhi ya wananchi wa newala ktk vijiji vya mikumbi,mnyambe,makukwe kwenye mikutano ya hadhara na Mbunge wao walimuuliza suala la maji akawajibu yeye siyo chura hivyo hajui shida ya maji.
2:Umeme ndiyo kabisa vijijini hakuna unawaka mjini tu.
3:ununuzi wa korosho ni shida tupu.Wananchi wengi wanategemea korosho kama zao kuu la biashara lakini cha ajabu hawafaidiki na zao hilo,wengi wao wanakopesha kwenye vyama vya msingi na malipo hayafanyiki kwa wakati.Wananchi wamekata tamaa na serikali yao.
Hivyo basi mkombozi pekee hasa kwa vijana ilikuwa ni uzalishaji wa Gesi.Kwa mbunge wa kusini kuiacha gesi ipelekwe dar ni kuitelekeza kusini,hakuna haja ya kujenga viwanda dar es salaam tu.Hata huku kusini tunahitaji viwanda ili kukuza uchumi wa huku.
Jamaani mikoa ya kusini ina shida nyingi sana na imetelekeza kwa muda mrefu mpaka huwa najiuliza huku keki ya taifa watakula lini? Na ile mtwara corridor enzi za rais mkapa imekwenda wapi? Barabara za nachingwea-masas,masasi-Newala-tandahmba,mt/vijijini,luangwa zitajengwa lini?
Watu wa kusini hawana majibu na wabunge wao nao hawana habari kabisaa.Change ni mimi na wewe hivyo endeleeni kudai watu wa mtwara.Bravo mtwara's peoples.

Waambueni waendelee kuwapigia kura CCM, wajinga ndio waliwao na CCM
 
Kikwete na wenzake wala hawahitaji gesi kufika Dar kama big deal, wanachohitaji wao ni ule MRADI wa 1.2Bn dollars utekelezwe ili wachukuae cha juu chao cha 50% then hela hiyo itawarudisha CCM madarakani 2015 na wengi wao watabakia matajiri hadi mwisho wa dunia...

Baada ya mradi wa bomba la gesi kukamilika na wao wamechukua chao mapema, hawatajali kama gesi imesafiria au haijasafiri, kuna umeme au hakuna. By the way kama issue ni umeme kwa 1.2Bn Dollar unazalisha 1200MW pale Stiggler's Gauge na kupata umeme wa maji wa bei nafuu lakini wao wamekomaa kwenye mradi wa bomba la kusafirisha gesi kwa kuwa ndio nafasi pekee ya kufanya ufisadi mkubwa zaidi katika historia ya nchi hii na kuwafanya matajiri wa kutupwa
 
Kinachosikitisha zaidi wabunge wao wengi wapo kwenye vyombo vya maamuzi(mawazir) lakini hawana jipya kwa wananchi wao.Mbaya zaidi Madiwan wengi darasa la nne au nane, wenyewe n ndiyo CCM wamesahau wajibu wao kwa wapiga kula wao.Wananchi wanatia huruma na kofia na tshirt za CCM zilizotoboka toboka kwa kuvaliwa kla siku
 
Wana-kusini, msijione wachache, hayo ambayo Gwakukaja85 ameyataja ndio yaliyowakimbiza wengi kuja Dar na kaskazini ... Hv upande wote wa 'kusini' mna hata 'Univesity' moja kweli au ndo bado mnajivunia OU? Huu ndo muda wenu wa kupata kile mlichoibiwa na kunyimwa toka Uhuru! Wenzenu wa kaskazn tunawaunga mkono, imagine, mi upande wa baba n Machame na mama ni Masasi, Machame wenzenu Lami, Umeme, Hospitali toka Mkoloni but huko hadi leo mnakula vumbi na sound ... msikubali, kama huku kuna Mt.K'njaro then huko nw mmepata gesi!
 
Mkapa sialikua wakule? Mawaziri kibao wanatoka Kule sasa iweje msiweze hata kupata maji ya kunywa? Na wananch wakule wanabadilishana ndno moja ya mahind kwa ndoo moja ya maji.kweli sisi tunashida lakiny nyie huko imewapenda zaidi. Ombeni mungu m4c iendelee kuzunguka huko
 
Kikwete na wenzake wala hawahitaji gesi kufika Dar kama big deal, wanachohitaji wao ni ule MRADI wa 1.2Bn dollars utekelezwe ili wachukuae cha juu chao cha 50% then hela hiyo itawarudisha CCM madarakani 2015 na wengi wao watabakia matajiri hadi mwisho wa dunia...

Baada ya mradi wa bomba la gesi kukamilika na wao wamechukua chao mapema, hawatajali kama gesi imesafiria au haijasafiri, kuna umeme au hakuna. By the way kama issue ni umeme kwa 1.2Bn Dollar unazalisha 1200MW pale Stiggler's Gauge na kupata umeme wa maji wa bei nafuu lakini wao wamekomaa kwenye mradi wa bomba la kusafirisha gesi kwa kuwa ndio nafasi pekee ya kufanya ufisadi mkubwa zaidi katika historia ya nchi hii na kuwafanya matajiri wa kutupwa

this is it!! miradi mingi ya ujenzi inayoendelea sasa hivi ni EPA za kufa mtu! komaeni wana kusini!
 
Nilifanya kazi mkoa wa Mtwara mwaka 1978-1980. Katika kipindi hicho, ukipelekwa kufanya kazi Mtwara ilikuwa ni kama adhabu na watumishi wengi wa serikali walikuwa hawapendi kwenda huko kutokana na kutokuwepo na huduma nyingi za kawaida. Katika watumishi wa serikali waende huko, serikali ilikuwa inatoa incentives mbali mbali kwa waliokubali kwenda huko. Mojawapo ya incentive mojawapo ni kupatiwa usafiri wa ndege kila wakati wa likizo kwenda mikoa ya mbali au hata safari za ki serikali. Hata hivyo ni ajabu kusikia kuwa baada ya miaka yote hii, sehemu hizo bado ziko nyuma sana.

Kila patakapotokea fursa ya kuleta maendeleo katika shemu hizo, serikali inapaswa iipe kiupaumbele.

Kwa taarifa, mimi sitokei Mtwara, bali natokea kati ya mikoa 'iliyoendelea' Tanzania. Napenda maendeleo hayo yaende pia kwa Watanzania wa Mtwara na sehemu zingine ambazo bado zimeachwa nyuma.
 
Mimi siwaonei huruma wacha waliwe na ma CCM hadi wakome.Wakitaka kuwa nami basi serikali za Mitaa wekeni Chadema tu ndiyo tuanzie hapo .
 
Kinachosikitisha zaidi wabunge wao wengi wapo kwenye vyombo vya maamuzi(mawazir) lakini hawana jipya kwa wananchi wao.Mbaya zaidi Madiwan wengi darasa la nne au nane, wenyewe n ndiyo CCM wamesahau wajibu wao kwa wapiga kula wao.Wananchi wanatia huruma na kofia na tshirt za CCM zilizotoboka toboka kwa kuvaliwa kla siku

Umegonga mule mule mkubwa.......Ndugu zetu pande zile wanaishi maisha duni sana
 
Kwa mtu aliyetembelea na kuishi mikoa ya kusini atakubaliana nami kuwa maisha ya mikoa ya Mtwara na Lindi ni karibu na "jehanamu."Nasema hivyo ni kiwa na maana ya kwamba Wananchi karibia 90% hawapati huduma za kijamii,mfano

1:MAJI suala la maji huko Mtwara hasa halmashauri za Newala, Masasi vijijini, Tandahimba wanateseka mno kipindi cha kiangazi. Baadhi ya wananchi wa Newala katika vijiji vya Mikumbi, Mnyambe, Makukwe kwenye mikutano ya hadhara na Mbunge wao walimuuliza suala la maji akawajibu yeye siyo chura hivyo hajui shida ya maji.

2:Umeme ndiyo kabisa vijijini hakuna unawaka mjini tu.

3:Ununuzi wa korosho ni shida tupu. Wananchi wengi wanategemea korosho kama zao kuu la biashara lakini cha ajabu hawafaidiki na zao hilo,wengi wao wanakopesha kwenye vyama vya msingi na malipo hayafanyiki kwa wakati. Wananchi wamekata tamaa na serikali
yao.

Hivyo basi mkombozi pekee hasa kwa vijana ilikuwa ni uzalishaji wa gesi. Kwa mbunge wa kusini kuiacha gesi ipelekwe Dar-Es-Salaam ni kuitelekeza kusini, hakuna haja ya kujenga viwanda Dar-Es-Salaam tu. Hata huku kusini tunahitaji viwanda ili kukuza uchumi wa huku.
Jamaani mikoa ya kusini ina shida nyingi sana na imetelekeza kwa muda mrefu mpaka huwa najiuliza huku keki ya taifa watakula lini? Na ile Mtwara corridor enzi za Rais Mkapa imekwenda wapi? Barabara za Nachingwea-Masasi, Masasi-Newala- Tandahmba, Mtwara vijijini-Luangwa, zitajengwa lini?

Watu wa kusini hawana majibu na wabunge wao nao hawana habari kabisaa. Change ni mimi na wewe hivyo endeleeni kudai watu wa Mtwara.

Bravo Mtwara's peoples.
Twa isala isi malafyale? Kangi une nalondile kujobha whuwhuwho,,,,,,
 
Back
Top Bottom