Maandamano ya Kupinga Ufisadi

Jamani jamani! maandamano ya kuweza kuwastua mafisadi huwa hayapangwi ulizeni kote walikoweza kufanya hiyo kitu. Maandamano huwa yanakuja ghafla kutokana na khali itakayowachukiza wananchi na kuamua kusema basi. kama tunavyojua sisi huwa hatuchukii kabisa hata tufanywaje. Mimi nilidhani walipotukatia umeme tukashindwa kuona champion league dar yote moto ungewaka du majitu kimyaaaa hata kulalamika tu hakukuwepo. Kupanga maandamano ni sawa na kumpa mwanafunzi mtihani kabla unategemea apate zero!
 
Jamani jamani! maandamano ya kuweza kuwastua mafisadi huwa hayapangwi ulizeni kote walikoweza kufanya hiyo kitu. Maandamano huwa yanakuja ghafla kutokana na khali itakayowachukiza wananchi na kuamua kusema basi.

Kwa misingi ya nguvu ya umma na kubaliana na wewe! But organization should start somewhere!
 
maandamano ya kulindwa na Polisi hayana RAHA...haytatokuwa na tofauti na maandamano ya UWT au Umoja wa Vijana wa CCM.....raha ya Maandamano mpambane na POLISI....na hapo ndipo Ulimwengu utalipuka na kelele zenu...from there we can write a new history...otherwise tuache idea ya Maandamano.

Unapenda hatari wewe! Na sidhani kama kufikiria hatari ndio suluhu, zaidi watu wakienda na mtizamo wa vurugu, hata kabla polisi hawajaanza kurusha mabomu wananchi tutawavamia. halafu hapo sijui tutakuwa tunatatua tatizo gani. Hao polisi, ni wananchi pia, ni wamoja sisi! sasa tukijisahau tukawaona na wao ni adui wa maendeleo hatutafika popote. Tunatakiwa tuangalie polisi au wanajeshi hao watawezaje kushirika katika maandamano! kama wafungwa waliweza kugoma chini ya ulinzi wa polisi, sisi tulio huru tunashidwa nini?

for what i know from JK..Mkiandamana hamtopigwa..mtaachwa ila mtazuiwa tu msifike IKULU au kuleta fujo za kuvunja biashara. JK his heart is soft in nature...Hawezi ona damu ya Mtanzania inamwagwa kwa Maandamano ambayo kesho yake tu watu watasahau....
the way yanavyoratibiwa hapa tayari yashafeli....!!!

Kwanini tusiende ikulu! kama swala ni kuongea na raisi na baraza la mawaziri kwanini tusiwafuate walipo? Lakini kabla ya kufika huko kwa kufikirika, je nia tunayo? Sababu je! Uhalali wa maandamano je? Haki ya kuandamana! kama majibu ni ndio, basi umma utaamua.
 
Mbona hujabuy idea ya petition mkuu?

Petition ni wazo zuri lakini linakona sana - kwanza kuelewa kwa kina ufisadi, pili kuwa na muhutasiri mzima wa hatua zilizochukuliwa, tatu ufafanuzi wa athari zilizopo kwa hatua zinazochukuliwa, nne mapendekezo ya nini kifanyike, na mwisho msimama! kama unauwezo, weka hoja chini na msimamo utakao wakilisha wananchi. Itume hapa gulioni kwanza wenye information waifanyie kazi!
 
Moja ya options- ni kurudi kwenye vyama vya siasa- hivi vina haki ya kuwepo na kufanya siasa. Kama kun chama kinachwoeza kuratibu na kuongoza katika hili ingekuwa vyema. La msingi kila mtu afanye homework yake. Mfano kila mwan JF achague watu wake kumi/au hata ishirini kama anaweza. Awaelimishe waelewe tatizo na nini pendekezo la kufanya. Watu wakielewa, na maandamano hayo yakapangwa yawe ya muda mrefu-sustainable, Watawala wataelewa. Lakini kama tunafikiria jambo la kupita- a day or two Hamna kitu hapo
 
organization is still a challenge! Watu wamekuwa wagumu kuchukua front role! HOFU.
 
YAP PETU HAPA,

Wazo zuri la uzalendo.

O.K lets go ahead. Tusichelewe tuanze kuongea na kupanda kabla hili vuguvugu halijapoa.

tatizo ni kuwa kila mtu yuko bize kutatua shida zake za kimasikini kila siku, hivyo tukiacha ikipoa basi tena.

Kama kuna mchango sema
 
Nilichosema mwanzo, ni watu wajitolee kuorganize maandamano na wengine wajitolee kuweka agenda za maandamano. Nimeongea na vikundi sita vya kijamii na vijana lakini hawajafikia hitimisho! Wanaangalia ni jinsi gani maandamano yataendana na agenda za mashirika yao! Pesa za NGO's na kazi zao ziko limited kikatiba! SUBIRA!
 
Kina Zitto na kina Slaa na kina mama Kilango na kina Selelii.. ndio walitakiwa kuonekana mitaani na mabango wakiongoza maandamano dhidi ya ufisadi na wakiwa na ajenga zilizo wazi:

a. Rostam ajiuzulu
b. Mashtaka ya EPA yawe ya kuhujumu uchumi
c. Chenge ajiuzulu
d. Mramba ajiuzulu
e. Kiwira irudishwe kwa wananchi
f. Benki Kuu ichunguziwe na chombo huru
g. Peter Noni aunganishwe na wenzake kwenye kesi
h. DPP afanye kazi aliyoapishwa kuifanya vinginevyo ajiuzulu
i. Mapendekezo yote ya Kamati Teule yafanyiwe kazi!

Ni maandamamano hayo ambayo yana malengo yaliyokuwa wazi, politically provocative ndiyo yanaweza kugusa watu.... ila sijui kama Lipumba atakuwa tayari kuungana nao!
 
Jakaya Mrisho Kikwete , Rais wa nne wa Tanzania -AJIUZULU.

Hao hawatajiuzulu kama wanajua mkulu wao ni mchafu! never, DPP hata akijiuzulu if he has no go ahead ya mkubwa ,tukubali hicho cheo kila atakayekuja atajiuzulu!

Mapendekezo ya Kmati teule yaendane na Mwakyembe, Kilango, n.k kujiuzulu kwa kutoridhishwa na utendaji wa serikali!
 
I support maandamano kumpinga Mr. President, that ameshindwa kuongoza nchi hivyo akae pembeni. Current country leadership is the source and the big problem.
 
Kina Zitto na kina Slaa na kina mama Kilango na kina Selelii.. ndio walitakiwa kuonekana mitaani na mabango wakiongoza maandamano dhidi ya ufisadi na wakiwa na ajenga zilizo wazi:
a. Rostam ajiuzulu
c. Chenge ajiuzulu

Nguvu ya kuwalazimisha wabunge kujiuzulu ipo kwa umma wote wa tanzania, ama ni wananchi wa jimbo husika? Taratibu zake zikoje?

Ni maandamamano hayo ambayo yana malengo yaliyokuwa wazi, politically provocative ndiyo yanaweza kugusa watu.... ila sijui kama Lipumba atakuwa tayari kuungana nao!

Sina wasiwasi na lipumba! I will be worried more with Mama Kilango na Seleli - kwa sababu kwa njia moja ama nyingine watakuwa wanasema serikali iwajibike. I am sure of their political stand on Ufisadi, but i am not sure in their of their activism out of parliament!
 
Nguvu ya kuwalazimisha wabunge kujiuzulu ipo kwa umma wote wa tanzania, ama ni wananchi wa jimbo husika? Taratibu zake zikoje?

Hawa wanaitwa "Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania".. kwani wanachofanya/wasichofanya Bungeni kinatuhusu sisi sote..

Sina wasiwasi na lipumba! I will be worried more with Mama Kilango na Seleli - kwa sababu kwa njia moja ama nyingine watakuwa wanasema serikali iwajibike. I am sure of their political stand on Ufisadi, but i am not sure in their stand activism politics out of parliament!

ndiyo tutajua ni yapi maneeno na yapi matendo..
 
Back
Top Bottom