Maandamano ya Kupinga Ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandamano ya Kupinga Ufisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Petu Hapa, Apr 24, 2009.

 1. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Vita dhidi ya Mafisadi inahitaji nguvu ya wananchi sasa. Maana mpaka sasa wananchi wamekuwa wasikilizaji na watazamaji tu. Umefika wakati ambapo tunahitaji kutambua kama hii vita ya mafisadi inawagusa kweli wananchi, na pia serikali itambue inahitaji njia za haraka kudhibiti ufisadi!

  Sidhani kama tunataka viporo kwa uongozi ujao, tunataka ufisadi ushugulikiwe ndani ya awamu ya kwanza ya kikwete, na asiposhughulikia kipindi hichi basi ndio ajue itakuwa swali lake kubwa katika uchaguzi ujao.

  Mawazo yangu, wapiganaji wa ufisadi, waandae maandamano ya amani kuitaka serikali ishugulikie swala la mafisadi kwa haraka zaidi. Tunahitaji kesi hizi zisikilizwe ndani ya miezi 6, na suluhu zake zipatikane kabla ya 2009 haijaisha.

  Maandamano yawe katika mikoa mitatu tofauti, na Zanzibar, katika siku zinazofuatana ndani ya wiki mbili. Kwa mfano maandamano yazinduliwe tarehe 9 may, Dar, tarehe 10 yapelekwe Kilimanjaro, halafu tarehe 16 yaende mwanza na 17 yafungiwe Zanzibar.

  Napendekeza mengi, kupitia ujasiri wake wa kuwataja mafisadi na vyombo vyake vya habari, awe kinara wa maandamano hayo, mzee mwanakijiji ashugulikie agenda za maandamano hayo, NGO’s zihamasishwe kushiriki, hasaFEMACT imekuwa mstari wa mbele kupinga ufisadi. Kitila Mkumbo uhamasishe watu wa vyuoni hasa vyombo vya wanafunzi kushiriki katika maandamano haya. Na watu wengine wenye michango mbalimbali katika harakati, ambao siwafahumu wajitolea kuhamasisha na kupanga maandamano haya.

  Umefika wakati wa kujiondoa katika magazeti na kujipima kupitia wananchi kama kweli ni agenda yetu sote.

  If we talk the talk, lets do the walk.
   
  Last edited: Apr 24, 2009
 2. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Hatimaye ! Brilliant idea. Mwanzo mzuri.
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Naunga mkono wazo ila ngoja wait....
  Kama gazeti la Mwanahalisi lililoandika habari za kuwanufaisha wao (watwana) likaishiwa kufungiwa. je sisi ambao tukiamua kuandamana si itakuwa yale yale ya wanyasa kuitwa wamalawi?

  Hapa tunapigania maslahi na heshima ya nchi kimya kimya ila mawazo yetu ndo yanapiga kelele kukemea uozo na uzandiki wa watawala kupitia forums kama hizi.

  Nadhani kwanza tunapaswa kuwachechemiza wanaozimiliki sheria (polisi) kwa kuwaelimisha ili wabadilike kwanza kisha ndo mtaona mfululizo wa maandamano ya HAKI ukirindima. Nchi hii huchelei kuitwa HAINI kisa tu unadai chako
   
 4. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Haki haijawahi kuja kirahisi rahisi, kwahiyo nauhakika hata haya maandamano hayatakuwa marahisi. Siwezi kusema watakaoamua kushiriki kwa udi na uvumba, jinamizi la ukandamizaji halitawasogelea. Najua lazima litatufuata tu! Lakini hiyo ndio hali halisi ya upambanaji kujitoa muhanga, ila kama waandaaji wa mapambano inabidi kufikiria ni jinsi gani tutapunguza hizo athari.

  Njia moja wapo ni kuhakikisha wanaongoza haya maandamano ni watu wanaojulikana katika jamii na mashirika ya kijamii na vyombo vya wanafunzi, hata kama serikali itakyereka vipi hawezi kuvifunga kirahisi.
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  kuna rafiki yangu mmoja kutoka ng'ambo ya bahari, huwa anawahamasisha sana washkaji zake kuandamana kule ng'ambo ila inapotokea dalili ya majiwasha huwa haonekanagi ktk kilinge hata kushiriki, yeye huchagua aina ya maandamano ya yeye kuandamana nao.
  Sina nia mbaya ila kwanza lazima kuelimishana kuondoa ukungu wa sheria na haki kutoka kwa wabeba bunduki wetu kisha hata wakiamua kututandika shaba iwe wanajua wanafanya nini maana sasa wanajua kuwa wana kazi moja tu kuwalinda watawala hata kama hao watawala wameoza vipi.
  umenipata hapo?
   
 6. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kazi ya JF ni kubwa sana na itaendelea kuwa hivyo, wala maandamano yanayopendekezwa hayana nia ya kudhaifisha forum kama hizi. Kwangu mimi, ni forum kama hizi ambazo zinanipa matumaini kwamba wakereketwa wapo wengi. Lakini pia tutambue, ingawaji maoni yetu yanawafikia viongozi husika, na wao pia wanatambua kabisa haya ni maongezi ya watu wachache tu kupitia mtandao kwahiyo hayawatishi sana. Umefika wakati wa kuwaambia sio sisi watu wachache ambao tunaandika kwenye keyboard ila tuwakilisha hisia za wananchi wengi tu.
   
 7. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nitakuwepo

  Kwanini unadhani polisi watatushambulia? Ndio nafahamu ubabe wa polisi hasa katika maandamano ya vyuo vikuu, lakini sijapata ufahamu wa mtu wa bunduki katika maandamano ya uraiani! Nielimishe! si kwamba nasema hayajotokea ama watu wa vyuoni wanafaa kududwa na polisi, la hasha, ila ningependa kama unamifano hata ya miaka ya nyumba tuelimishana ili tujiandae na hao polisi! Nacho jua mimi, watakachoweza kufanya iwapo maandamano yatakuwa makubwa na kuwaogopesha ni kurusha mabomu na kupiga na kusweka watu rumande! Iwapo watafyatua risasi, huo ndio utakuwa mwisho wao.
   
 8. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Idea bomba sana Petu?

  BWT....!Je, unafikiri serikali itashtuka kwa maandamano hayo, kwani kina Dr. Slaa si walishaandamana na kutaja a list of shame...what happened thereafter? Je, serikali yetu inajua implications za wananchi kuandamana? kwani inawauma kusikia wananchi wanaandamana? mimi siamini kabisa kama eti kuandamana kwa siku moja tu kutawakosesha serikali usingizi...!

  Labda sema tujipange mitaani hadi ikulu, tukiimba nyimbo za ukombozi na taifa......non stop mpaka watoe tamko rasmi la hatua madhubuti za kuwachukulia hatua mafisadi au mpaka waresign! Hili lisiwe zoezi la siku moja ...no, iwe ni non stop...hapo nafikiri hawa watastuka!

  Alternatively, labda tuandae ushahidi wa kutosha kuwashtaki mafisadi wote then petition iandaliwe na isainiwe na wananchi wote wanaokereketwa na ufisadi, then tutafute Advocates watusaidie kuwafungulia kesi mahakamani tukishirikiana na wanaharakati mbalimbali! Mimi nipo tayari kuisupport hii morally and materially tukishajipanga vizuri!
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Wazo zuri Petu Hapa.
  Wanajamvi tunaweza kuandaa maadamano nchi nzima kuishinikiza serekali ichukue hatua za kisheria dhidi ya mafisadi.
   
 10. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wasiwasi wako unamsingi kabisa, na unaouliza maswali ya msingi ni vipi tujipange ili kuhakikisha mchango wa wananchi unaleta mabadiliko katika ufisadi.

  Labda nianze na swala la list of shame! Juhudi alizozifanya Slaa na kutaja mafisadi ilikuwa nzuri na ilikuwa ni mchango mkubwa, lakini ilikupata ushiriki mpana tunahitaji kujitoa katika mambo ya siasa. Vyama vya siasa katika maandamao yajayo vitakuwa washiriki na sio waongozaji wa maandamano haya.

  Maandamano ya kugawanyika hawayaogopi, lakini maandamano ya pamoja bila kujali itikadi wanayaogapa ila wanauhakika hayawezi kutokea. Amini nakwambia, serikali ikiona zaidi ya watu elfu 6000 barabara moyo utaenda mbio tu. Tatizo maandamano mengi yanayoendelea ni tumejigawa sana, ngo's kivyao, waislamu kivyao, vyuo vikuu kivyaoo, kafuu kivyao, sekondari kivyao. Sasa tukivuja hiyo kivyao vyao, na kuwa sisi! Serikali itacheza dede!


  Nachosema mimi chochote kile ambacho wananchi wataona kinafaa ndicho kitumike. Ni kweli watanzania wanapenda nyimbo kwiyo hilo nalo ni jambo la msingi! Tuziimbe wee mpaka machozi yatoke. Kuelekea Ikulu nalo ni wazo zuri ila tunatakiwa kuhakiki huyu mkuu asiwe majuu maana anasafiri sana. Wasiwasi wangu kwenda ikulu watatupa kibali?

  Lakini swali la msingi pia, ambalo wataalamu wa maswala ya siasa na serikali watuambie - haya maandamano lengo lake liwe nini na tumshinikize nani, halafu tutajua wapi tutaelekea na tujipange vipi

  This is not an alternative it should be a second stage of citizens action toward mafisadi. Maandamano yaanze, stage two petition.
   
 11. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  unadhani unaweza kushiriki vipi? ama unamapendekezo gani juu ya kuishinikiza serikali
   
 12. Poetik Justice

  Poetik Justice Member

  #12
  Apr 24, 2009
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Swala la maandamano si baya lakini wananchi lazima wahamasike zaidi ili waweze kushiriki. On the other hand, Mengi au independent media houses zingine zingeweza kuandaa documentaries kuhusu ufisadi. Yaani, definition ya ufisadi, jinsi unavyoathiri nchi, maendeleo na hata wananchi. Documentary ijumuishe testimonies au stories za watu kuhusu madhara ya ufisadi ili watu wahamasike zaidi. Mfano.. vifo vya maalbino imekua ni rahisi ku-raise awareness na hisia za watu maana zile picha na testimonies zimetugusa, tukasikitika, tukasirika etc etc. Tukaandamaana na kulaani hivyo vitendo, kwa hiyo hata kwenye ufisadi, the same can happen.
   
 13. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #13
  Apr 24, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Poetik,

  You are very right! The media houses have been quite proactive to present the public with facts about corruption, then i think it should turn the wheels around to show the government how the public is tired with corruption.
   
 14. m

  mnozya JF-Expert Member

  #14
  Apr 24, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Ni wazo zuri sana. Daima nguvu ya umma hushinda. Kwa kuwa JF si jukwaa la kisiasa ni vema wanaharakati wakashirikishwa. Mie nadhani iwe kama ifuatavyo
  Kulaani ufisadi.
  1. kuishinikiza serikali ichukue hatua za ziada na za makusudi. Tunaposema serikali tunamaanisha Rais na baraza lake la mawaziri
  Kulaani serikali kung'ang'ania kuficha nyaraka ambazo zimejaa hujuma kwa taifa, hapo tulaani tamko la waziri Ghasia bungeni kuwazodoa watu wanalinda na kutetea rasilimali za Tanzania huku akijua wazi kuwa HILO NI JUKUMU LA KIKATIBA LA KILA MTANZANIA.

  Kama ilivyo kwa mkataba wowote unaovunja sheria huwa ni mkataba haramu, HIVYO WARAKA WOWOTE UNAOHUJUMU TAIFA NI WARAKA HARAMU OTHERWISE IMEKUWA PROVED VINGINEVYO.
   
 15. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #15
  Apr 24, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  wanaharakati gani washirikishwe? Tafadhali kama unamajina kamili na mawasiliano yao nitumi PM. Pie kama unawazo la NGO nipatie tafadhari.
   
 16. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Apr 24, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Watamwaga FFU, polisi na hata jeshi ili kuhakikisha maandamano hayo hayafanyaki. Si mnajua CCM ni chama cha mafisadi!? Kwanini waruhusu maandamano ya Watanzania waliochoka na ufisadi na hali chama hicho si wawakilishi tena wa wakulima na wafanyakazi?
   
 18. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #18
  Apr 24, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
   
 19. H

  Herbert Member

  #19
  Apr 24, 2009
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Ni kweli chama kimokosa hatamu na hakieleweki kinamwakilisha nani katika hili taifa letu.

  Ila swala la kuogopa bunduki na mabomu ya machozi hapa halipo. Mi nadhani kama wachangiaji wengine walivyotangulia kusema kwamba tukiwa kama raia walioguswa na swala la ufisadi na ni swala ambalo si geni hata kwenye medani za kimataifa, Tukiandamana kwa amani hawa jamaa watakuwa hawana ujanja.

  Tatizo kubwa ni tunaanzaje kuingia barabarani???

  Nadhani tukipata documentary chache ya maisha halisi ya watanzania na kusikia kutoka kwa watu waliochoka kama Mengi alivyofanya then swala la kuingia barabarani litakua automatic.

  Tuwe wazalendo na tupige vita kwa dhati ufisadi.

  Nimesikia kuna tetesi kwamba ufisadi sasa umeingia NSSF na kuna hatari ya baadae raia wema wanaochangia mfuko huu kuja kushindwa kulipwa fedha zao. Sasa tusipokua makini tutazama kwenye dead lock.
   
 20. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #20
  Apr 24, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nilishatoa wazo awali kwamba waandishi wa habari waanze kuandika mtazamo wa wananchi juu ya ufisadi sasa! Imefika wakati tuchoke kuwasikia huyu kafikishwa mahakamani na yule kamtaja yule. Inabidi tuanze kusikia sauti za wananchi wa kawaida, mtizamo wao ni nini kuhusu ufisadi! Na sio kwenye swala la Kipima joto, tunahitaji vipindi maalumu.

  Mengi, tupe vipindi vya bure tuweke program za kusikia wananchi mitizamo yao na debate juu ya ufisadi! Kipindi kinaweza kufanyika kama talk show hivi! Utupe lisaa moja na nusu - kwenye television na radio! Jina la kipindi litakuwa "Maamuzi ya Mwananchi" kiwe mara mbili kwa wiki na marudi mara mbili kwahiyo tunakiona mara nne kwa masa 12 kwa wiki ndani ya miezi mitatu kuanzia Mid May or June, 2009. Kunavipindi ambayo vitafanyika dar, na kunavipindi ambavyo vitafanyika mikooni kutokana na mada husika. Washiriki katika vipindi watakuwa wananchi wa kawaida waliothirika moja kwa moja na ufisadi, wataalamu wanaolewa sheria na hatu a za kuchukua dhidi ya ufisadi, na wakereketwa. Dhumuni la kipindi hicho na kuelimisha na kujenga msimamo wa wananchi dhidi ya ufisadi! Lengo la kila kipindi ni kuhakikisha jamii inajadili ufisadi kwa upana wake na hatua zinazoweza kuchukuliwa.
   
Loading...