kluger
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 2,093
- 1,894
Salaam,
Nimefuatilia tu maandamo yaliyofanyika jijini Dar es salaam, nje ya ubalozi wa Africa kusini kushinikiza au kudai ndege ya Tanzania iliyokamatwa huko nchi Africa kusini ni aibu kubwa kwa Taifa.
Safari hii jeshi la polisi limeonyesha udhaifu wa kintelijensia kwa kushindwa kubaina mpango huu wa maandamano mpka yakafanikiwa, lakini kwa upande mwingine tunawapongeza kwa kutumia fimbo tu kutawanya waandamanaji na si mabomu kama ilivyoada.
Jambo hili lipo kisheria huko mahakamani Africa ya kusini na lilianzia hapa hapa Kwnye mahakama zetu, iweje leo kutumia nguvu ya umma/maandamano kushinikiza maamuzi ya jambo hili?
Je maandamano haya ni kundi gani la jamii?
Polisi tusaidieni kujua waratibu wa maandamano haya ni kina nani hasa?
Ni aibu sana kuona jambo hili limetoka mbali toka serikali ya awamu ya kwanza mpka leo hakuna ufumbuzi uliowahifikiwa.
Hii inaonyesha ni jinsi gani waafrica tulivyo kitabia na namna ambavyo tunapuuza mamlaka tulizoanzisha sisi wenyewe.
Ubabe na kulewa madaraka vinafanya watu na baadhi ya viongozi wetu kukosa utu na kutii sheria, ni kama wapo juu ya sheria za nchi.
Hapa wanatakiwa kufahamu hilo ni ndani tu ya mipaka yetu ya nchi. Huko nje watu wanatii sheria na kupambana kisheria.
Jambo hili limeumbua sana nchi na kuonyesha dunia ni namna gani tunashughulika na mambo ya kisheria.
Kuna baadhi ya watu kwa uelewa mdogo au kwa maksudi wanaunga mkono serikali mapungufu haya yaliyosababisha ndege kukamatwa.
Tuache ushabiki, tuelewe mambo na tuishi katika misingi ya kuheshimiana na kusikiliza wengine, TUACHE UBABE, USHABIKI, UNAFIKI NA TUMUOGOPE MUNGU katika maamuzi na uongozi.
Hili liwe funzo, kwa wote waliokosea katika utendaji.
NB: Kibaya zaidi waliondamana sioni abiria kabisa wa kupanda ndege nauli laki 3.5 kwenda Mwanza tu