Maandamano ya CHADEMA: Aqulina Akwilini Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza NIT apigwa risasi na kufariki; Polisi wakiri kuhusika

Hicho ndicho alichokita mbowe kitokee Ile wakitumie kama duru ya kupata huruma. Nawapa pole wazazi wa marehemu na nawashauri wamfungulie kesi mbowe kwa ushawishi wa kuvunja sheria na kilichompeekea mwanawao kupoteza maisha

Punguza ujinga ndugu
 
Ni pole tu tunaweza kusema hakuna cha ziada. Hata tulie, hata tulalamike, hatuwezi tena kumrudisha
 
Huu uzi umenionesha namna tuna waTz wapumbavu humu nchini, chuma cha moto kupenya kwenye nyama za mtu asiye na hatia maumivu yake si ya mchezo, uoga, hofu na mshangao wa kuvuja damu na taharuki ya waliomzunguka si kidogo, fikra zake zinawaza kifo kimekaribia lakini kwanini kwa hali hii nyie acheni kabisa hili jambo.
 
Maandamano huwa yana mengi, mf maandamano ya CDM Moro yalipelekea kifo cha muuza magazeti n no one alijua risasi iliyomuua ni ya polisi au mtu mwingine.

Binafsi pamoja na ushabiki wangu, nimejizuia kushiriki maandamano yoyote ya siasa!!!
 
Mnashindwa kupambana na majambazi mnapambana na raia asiye na siraa, nisawa kupigana na mtu aliyefungwa mikono na miguu, alafu unajisifu kuwa umempiga. Polis mjitafakari.
 
Saa 11 jioni maeneo ya Mabibo jijini Dar es Salaam, msichana mrembo na anayejiamini anaingia kwenye basi la daladala huku simu yake ikiwa sikioni akizungumza na mtu mwingine.

Daladala hilo linaonekana limejaa, hakuna siti yoyote, lakini msichana huyo hakujali, aliingia kwenye basi hilo na kusimama, safari ikaanza.
Alikuwa anakwenda Kijitonyama ili awahi mabasi ya kwenda Bagamoyo, lakini safari yake ikaishia njiani.

Safari yake ikaishia njiani mara mbili; hakufika Kijitonyama alikokuwa anakwenda, lakini pia safari yake ya duniani ikawa imeishia hapo.

Hiyo ni safari ya mwanafunzi wa shahada ya kwanza wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline aliyeuawa juzi kwa kupigwa risasi na polisi, ambaye simulizi yake imewekwa kwenye gazeti la Mwananchi la Jumapili. Usikose kupata nakala yako.

SWALI LILILOPO:

Aliyefyatua hiyo risasi anajulikana? Na je atafanywaje?

Time will tell.
 
Watu wanaua wenzao utadhani wao hawatakufa, utadhani wataishi milele. Huyo polisi alomuua huyo binti, hivi ingekuwa mdogo wake ndo ameuwa kwa sababu ya kijinga namna hiyo angejisikiaje. Mungu awape uvumilivu wazazi, ndugu na jamaa na watanzania kwa ujumla katika kifo cha huyo mwanafunzi na wengineo wanaouwawa hovyo hovyo kwa namna moja ama nyingine
 
Back
Top Bottom