LazyDog
JF-Expert Member
- Apr 10, 2008
- 2,473
- 193
shalom, are you around? Tarehe saba mwezi huu Shalom aliweka bandiko humu JF: Tuandamane mpaka ikulu
Kuna copy inatembea mtaani nimeona ni vyema kuiweka hapa.
Nimei-type, kwahiyo huenda kuna makosa ya uchapaji.
Tafadhali, pamoja na kutoa maoni yako kuhusu bandiko hili, zingatia kuainisha maboresho ambayo ungependa yafanywe na waandaaji wengine next time.
Amani iwe nanyi!
Lazydog
.
Kuna copy inatembea mtaani nimeona ni vyema kuiweka hapa.
Nimei-type, kwahiyo huenda kuna makosa ya uchapaji.
Maandamano ya Amani
Ndugu, Watanzania wote tunaoitakia maendeleo, amani na utulivu wa kudumu nchi yetu. Tunaombwa kushiriki maandamano ya amani yaliyopangwa kufanyika tarehe 23/08/2008 Saa 4:00 asubuhi yatakayo anzia viwanja vya mnazi mmoja na kumalizikia Ikulu, Mjini Dar es Salaam.
Madhumini ya maandamano haya ni:
- Kuiomba serikali itoe ripoti ya kamati ya EPA na kutangaza hadharani majina ya watuhumiwa waliobainika kuchota fedha za EPA.
- Serikali ifuate sheria kanuni na taratibu tulizojiwekea katika kuwashughulikia watuhumiwa hao.
Ndugu Watanzania hii ni nafasi pekee ya kuonyesha jinsi unavyoipenda na kuithamini nchi yako lakini pia ni njia nzuri ya kuonyesha jinsi unavyo uchukia ufisadi badala ya kuongea tu ndani ya madaladala, vijuweni, ofisini, nk sasa tuunganishe nguvu pamoja na tutashinda.
Tumetoa muda ili kuviwezesha vyombo vya usalama kujipanga kuimarisha ulinzi sehemu zote tutakazo pita ili kufanikisha maandamano hayo.
Kabla ya kuanza kwa maandamano hayo kutakuwepo na sala, dua, maombi, toka dini na madhehebu tofauti.
Muhimu:
- Maandamano hayo hayahusiani na vyama vya siasa na wanasiasa
- Asiwepo mtu yeyote atakayebeba silaha ikiwa ni pamoja na fimbo
- Kubeba vitambaa vyeupe ni muhimu
- Kufanikiwa kwa maandamano haya ni mwanzo wa Tanzania mpya tunayoitarajia, timiza wajibu wako (njooni kwa wingi)
- Kutoshiriki maandamano haya ni kuunga mkono ufisadi
- Maandamano haya yatafanyika nchi nzima kwa awamu
- Kuwa na uchungu na nchi yako kwa kuisaidia kamati ya kueneza taarifa hizi au toa kopi ya tangazo hili na uzisambaze
Kny Kamati ya kutetea maslahi ya taifa
<SAHIHI>
Rafael Mikaya Luvakubusa
Mtendaji Mkuu
Wasiliana na mtendaji mkuu TEL: 0783 679-079
Tafadhali, pamoja na kutoa maoni yako kuhusu bandiko hili, zingatia kuainisha maboresho ambayo ungependa yafanywe na waandaaji wengine next time.
Amani iwe nanyi!
Lazydog
.