Maandamano makubwa ya CHADEMA kumng'oa Meya wa Ilemela - Agosti 19, 2013

Makala Jr

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,395
1,110
Ndugu wana JF, bila shaka mtakumbuka kuwa hakuna Meya Tanzania asiyekuwa na chama lakini Meya Henry Matata alitimuliwa uanachama na CHADEMA kwa makosa ya kukihujumu chama kwa maslahi ya CCM na kufuja mali za chama alipokuwa Diwani kupitia CHADEMA lakini halmashauri ya jiji la Mwanza ilipogawanywa; alichaguliwa kwa hila na CCM kupitia madiwani wake katika kikao haramu ambacho siyo tu kwamba akidi haikutimia kutokana na madiwani wa CHADEMA kutokuwepo, bali pia hawakupewa taarifa sahihi kuhusu uchaguzi.

Maandalizi yote ya maandamano kushinikiza Henry Matata yamekamilika, muda huu gari za matangazo zinapita kuwakumbusha wana Ilemela waliokuwa na shauku ya muda mrefu kumtaka achaguliwe Meya halali nje ya kibaraka wa CCM asiyekuwa na malengo na wananchi zaidi ya kulinda ufisadi wa CCM.Maandamano hayo yataongozwa na Mbunge wa Ilemela, Mhe. Highness Kiwia, Mbunge wa Nyamagana Mhe.Ezekiel Wenje, viongozi wa kitaifa wa CHADEMA na madiwani wote wa chama hiki tegemeo la kuleta demokrasia.

=============
Tanzania Daima said:
na Sitta Tumma, Mwanza | Tanzania Daima

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), manispaa ya Ilemela, mkoani Mwanza, kimeitisha maandamano makubwa ya amani kesho kwa ajili ya kushinikiza kung'olewa kwa meya wa manispaa hiyo, Henry Matata, anayedaiwa kuchaguliwa kinyume cha sheria.

Akitangaza maandamano hayo mbele ya waandishi wa habari jijini hapa jana, Ofisa Operesheni wa CHADEMA Kanda ya Ziwa Magharibi, Tungaraza Njugu, alisema yataungwa mkono na maelfu ya wananchi wa Nyamagana.

Alisema maandamano hayo yataanzia Buzuruga saa 4:00 asubuhi kisha kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo, katika uwanja wa Furahisha, na kwamba unahitajika kufanyika upya uchaguzi wa meya na naibu wake.

Tungaraza aliyeongozana na ofisa wa chama kanda hiyo, Meshack Mikael, pamoja na katibu wa mbunge wa Ilemela, Laban Agrey, alisema maandamano hayo yanahusisha pia kupinga kufukuzwa kinyemela madiwani watatu wa chama hicho.

Madiwani waliofukuzwa na meya wa manispaa hiyo kinyume cha sheria ni Abubakar Kapera (Nyamanoro), Malietha Chenyenge (Ilemela) na Dany Kahungu wa kata ya Kirumba.

"CHADEMA tumeitisha maandamano makubwa hapo kwa lengo la kumkataa meya wa Ilemela na kushinikiza uchaguzi ufanyike upya.

"Matata amechaguliwa bila kukidhi akidi ya madiwani wa manispaa hiyo ambayo ni theluthi mbili ya madiwani wote 14, hivyo siyo meya.

"Lakini maandamano haya yatalenga pia kupinga Matata kuwafukuza madiwani wetu kinyemela. Sheria zinasema diwani atakosa sifa baada ya kutohudhuria mfululizo vikao vitatu vya Baraza la Madiwani, lakini Matata aliyechaguliwa kinyume cha sheria aliwafukuza ndani ya wiki moja baada ya kuchaguliwa," alisema.

Alisema CHADEMA pamoja na wananchi wa Ilemela wanahitaji kufanyika upya kwa uchaguzi wa meya na naibu wake na kwamba kama kweli madiwani hao wamefukuzwa kihalali wapewe barua za kufukuzwa kwao na tume ya uchaguzi itangaze kata hizo kuwa wazi.

"Kuna taarifa zinaeleza kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alishaandika barua ya kutengua uamuzi wa kufukuzwa madiwani hao na barua hiyo ‘imekaliwa' na mkuu wa mkoa,"alisema.

Naye katibu wa Highness Kiwia, Laban Aggrey, kwa niaba ya mbunge huyo alisema kuwa maandamano hayo yataanzia Buzuruga kisha kupita barabara ya Nyerere, Mlango mmoja, Uhuru, Nkrumah, Balewa na kuishia uwanja wa Furahisha.

"Polisi wameshabariki kufanyika maandamano yetu, hivyo ofisi ya mbunge wa Ilemela inawasihi sana wananchi wajitokeze kwa wingi kuja kudai haki yao iliyoporwa kinyume cha sheria," alisema.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu, alisema maandamano hayo ya CHADEMA yameruhusiwa na jeshi lake.

"Haya maandamano tumeyaruhusu kabisa yafanyike, maana kama watu wanasema wanadai haki yao kwa nini tuwazuie? Tumewapangia maeneo ya kupita maandamano haya hadi huko Furahisha," alisema Mangu.

Uchaguzi wa meya wa Ilemela uliofanyika Desemba mwaka jana, ulikiuka kanuni na sheria za halmashauri, ambapo akidi ya wajumbe iliyokuwa ikihitajika kwa ajili ya meya kupigiwa kura ni madiwani tisa, lakini ni madiwani sita tu ndiyo waliopiga kura.

Katika uchaguzi huo uliohudhuriwa na mkuu wa wilaya hiyo, Amina Masenza (DC), pamoja na mwanasheria wa jiji la Mwanza, Savela Manzi, aliyesimamia uchaguzi huo kwa upande wa mambo ya sheria, Matata alitangazwa kuwa meya baada ya kuchaguliwa na madiwani wasiokidhi theluthi mbili.

Madiwani waliopiga kura kumchagua Matata na naibu wake (Dede Swila wa CCM), walikuwa wanne wa CCM, mmoja wa CUF ambaye ni mbunge wa viti maalumu, Mkiwa Kimwanga, na Matata mwenyewe aliyefukuzwa uanachama wa CHADEMA.

Matata alichaguliwa wakati suala lake la kufukuzwa uanachama ndani ya CHADEMA likiwa bado linangojea uamuzi wa mahakama.
 
Ango,olewe tu matata nchi haiwezi kuchezewa namna hiijangiri lenzake Mkurugenzi kabwe anabwia vumbi la Dar pepo ya Mwanza kaisahau kabisa
 
Jee haiwezekani kungolewa kwa kura mpaka maandamano. Hii culture ya maandamano sasa inaleta matatizo mengi, Arusha imetuharibia maisha, biashara zimekufa, watalii wamekimbilia kenya na moshi, Wamachinga wanaharibiwa mitaji yao. Hivyo kweli kama CDM ina numbers hapo ilemela kwanini msitumia nguvu ya kura na kumuondoa. Ikiwa mnashirikisha maandamano inamaanisha ya kuwa ccm ndio wenye numbers , ila CDM inafanya uchochezi.

hatuwezi kukubali mahayawani wachache wabake demokrasia na kuchezea sheria halali,lazma ang'olewe huyo meya wa kuchonga
 
Jee haiwezekani kungolewa kwa kura mpaka maandamano. Hii culture ya maandamano sasa inaleta matatizo mengi, Arusha imetuharibia maisha, biashara zimekufa, watalii wamekimbilia kenya na moshi, Wamachinga wanaharibiwa mitaji yao. Hivyo kweli kama CDM ina numbers hapo ilemela kwanini msitumia nguvu ya kura na kumuondoa. Ikiwa mnashirikisha maandamano inamaanisha ya kuwa ccm ndio wenye numbers , ila CDM inafanya uchochezi.

Linalowezekana leo lisingoje kesho, nyerere angesema asubiri hadi mkoloni atoe uhuru free bibi ako angekuwepo?
 
tuko pamoja comrade."asante Mungu wana Ilemela tumepata kibali na baraka zote za rpc kama taratibu zingine''
"nikwombe Mungu kesho niamke kama siku zingiiine"
"apatae taarifa hii asisahau kumfahamisha mtu mwingine"
"na umfahamishe yataanzia FRAHISHA kama siku zingine"
"usisahau azimio letu ni saa 3 asb kama maazimio mengine"

"Big up mleta mada kama waanzisha thread wengine"
 
Jee haiwezekani kungolewa kwa kura mpaka maandamano. Hii culture ya maandamano sasa inaleta matatizo mengi, Arusha imetuharibia maisha, biashara zimekufa, watalii wamekimbilia kenya na moshi, Wamachinga wanaharibiwa mitaji yao. Hivyo kweli kama CDM ina numbers hapo ilemela kwanini msitumia nguvu ya kura na kumuondoa. Ikiwa mnashirikisha maandamano inamaanisha ya kuwa ccm ndio wenye numbers , ila CDM inafanya uchochezi.

kuandika unajua ila ulichoandika ndo ukijui. omba ueleweshwe, karibu sana mwanza. kesho tupo barabarani mpaka kieleweke.
 
Meya Matata ana haki wakazi wa Kitangiri ndiyo wamemchagua kuwa diwani wao haiwezekani Dr Slaa na Mbowe wamfukuze.

Safi sana Meya endelea kuwatumikia wakazi wa Jiji la Mwanza.

Chadema hamna uwezo wa kumng'oa Meya Matata.
 
Matata kwisha ! Naihurumia sana familia yake kwa aibu iliyosababishwa na baba yao !
 
lazima niwepo kuhakikisha tunamng'oa huyo meya feki,WANG'OLEWE TU MAANA NA CC TUMECHOKA
 
Mkirindi; Soma vizuri thread kabla ya ku comment, box la kura lishahujumiwa tangu siku nyingi. Hawataki kuitisha uchaguzi huru na haki!
 
Last edited by a moderator:
Meya Matata ana haki wakazi wa Kitangiri ndiyo wamemchagua kuwa diwani wao haiwezekani Dr Slaa na Mbowe wamfukuze.

Safi sana Meya endelea kuwatumikia wakazi wa Jiji la Mwanza.

Chadema hamna uwezo wa kumng'oa Meya Matata.

Vitz sisi wana Kitangiri haohao ndo tunamuondoa kwa maandamano!!
 
Meya Matata ana haki wakazi wa Kitangiri ndiyo wamemchagua kuwa diwani wao haiwezekani Dr Slaa na Mbowe wamfukuze.

Safi sana Meya endelea kuwatumikia wakazi wa Jiji la Mwanza.

Chadema hamna uwezo wa kumng'oa Meya Matata.

mbona mnajing'oa ubongo , hivi nani alimchagua matata kuwa meya wa Ilemela ?
 
Ritz; Kwa hiyo unataka kupuuza katiba ya nchi inayotaka kiongozi aliyefukuzwa uanachama pia uongozi wake hukoma? Isitoshe Matata hakuchaguliwa kuwa Meya na wana Kitangiri bali madiwani wa CCM!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom