Mimi naamini kuwa hapa si suala la polisi kusafishwa peke yake,kuna misingi imeanza kuanguka tena kwa kasi ajabu!!mfano msingi wa kuaminiana kati ya polisi na chadema umeporomoka,bila kukaa chini wakazungumza na kurudisha kuaminiana tusidanganyane kuwa kuna upande utaona kuwa haupo sahihi kwa madai yao!!
Mfano polisi wameshajenga dhana kuwa wanadharauliwa na chadema,inaweza ikawa ni kweli lakini naamini si kwa matukio yote,na chadema nao wameshaweka akilini mwao kuwa wanaonewa kila tukio!!kitu ambacho naamini kuwa si kwa matukio yote!!hatari zaidi ni pale kuna madai kuwa polisi kupitia kwa Ocd na Rpc wanaapa kupambana na chadema kwa gharama zozote zile,kama ni kweli (sina uhakika) ni hatari kwa amani ya nchi,hakuna sehemu yoyote katika dunia hii nguvu ya dola ilifanikiwa kuziba watu midomo.
Kinachotakiwa sasa ni pande mbili kuzungumza na kujenga kuaminiana,chadema wahakikishe wanatii sheria hata kama wanaziona zinawakandamiza kwani sheria hazibadilishwi kwa mapambano,na polisi kufanya kazi kwa misingi ya haki bila kupendelea kwani kuna matukio huwa yanaonekana ni kama vile wanatumika kuwabeba ccm,wajiweke kando na siasa.
Totauti na hapo akina mijusi wengi wataibuka na amani ya nchi itakuwa hatarini.