Maandamano makubwa kupinga mashambulizi Gaza

Maandamano makubwa kupinga mashambulizi Gaza

Status
Not open for further replies.

Gama

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
13,264
Reaction score
4,747
Maelfu waandamana kupinga vita Gaza

Maelfu ya watu wameandamana mjini Cape Town, Afrika Kusini, London na kwengineko kupinga mashambulio ya kijeshi ya Israel dhidi ya Gaza.

Maandamano ya Afrika Kusini yaliitishwa na National Coalition for Palestine, inayojumuisha makundi ya kidini, jamii, vyama vya wafanyakazi na vyama vya kisiasa.

Inafikiriwa kuwa maandamano hayo yalikuwa kati ya maandamano makubwa kabisa kufanywa katika mji huo tangu ubaguzi wa rangi kumalizika Afrika Kusini.

Kati ya watu waliohudhuria ni askofu wa zamani wa Cape Town aliyepata tuzo ya Nobel ya amani, Desmond Tutu.

Maandamano piya yamefanywa mjini London, Uingereza na Sydney, Australia.

Gaza kwenyewe, Israil imeendelea kuishambulia baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kumalizika Ijumaa asubuhi.

Imetokea miripuko miwili mikubwa katika eneo la bandari ya Gaza.

Mwandishi wa BBC anasema inafikiriwa kuwa shambulio moja lililenga eneo la mafunzo la Hamas.

Wapalestina wanasema watu kama watano wameuwawa tangu mapigano kuanza tena pamoja na mfuasi mwandamizi wa Hamas.

Umoja wa Mataifa unakisia kuwa nyumba za watu karibu 65,000 wa Gaza zimeangamia katika mashambulio ya karibuni.

Kundi la Hamas limekataa kuzidisha muda wa kusitisha mapigano kwa sababu linasema madai yao kuwa vizuizi vilioko dhidi ya eneo la Gaza viondoshwe bado hayakutekelezwa.

Lakini inavofahamika ni kuwa mazungumzo baina ya Hamas na wapatanishi wa Misri yanaendelea.

News
Nyumbani
ENG | KIS © Tigo
 
Yaani katika watu walionishangaza ni Desmond Tutu ni kiongozi mkubwa wa Dini halafu anaongoza maandamano ya kupinga Taifa teule la Mungu, kwa kitendo alichokifanya ajiandae kwa laana itakayompata
 
Yaani katika watu walionishangaza ni Desmond Tutu ni kiongozi mkubwa wa Dini halafu anaongoza maandamano ya kupinga Taifa teule la Mungu, kwa kitendo alichokifanya ajiandae kwa laana itakayompata

Acha udini kama mungu wenu yuko hivyo kazi ipo.
 
Wanatimiza haki yao ya msingi kuonesha wasichopendezwa nacho.

Sijaelewa kama wakimaliza hayo watafanya hivyo pia kwa...

1. Libya, wanauwana kama kuku na kimbulu

2. Syria, Asad anawapuktisha wapinzani wake na raia wasio namakosa na mara nyingine akitumia chemical weapons kwamaelfu wanakufa.

3. Iraq, ISIS wanafyeka wapinzani wao kama manyasi, shia na wakristu, kwa maelfu, wengine wapo milimani

4. Somali pia balaaa

Sasa kama hii haki ya kulaani itawalenga walau pia Alshabab, Bokoharam na ISIS itajijengea

heshima kubwa duniani kote, isilenge watu wa taifa moja tukiacha mamilioni wengine wakihitaji

pia kutetewa na kusikilizwa bila kusahau Libya na syria. Mungu atusaidie.
 
Wapuzi hao, wacha waandamane hadi kuzimu lakini kipigo lazima. Mbona hakuna anayeongea kuhusu mashambulizi yanayofanywa na Hamas. Ina maana Israel wakae kibwege bila kujibu mashambulizi.
 
Wapuzi hao, wacha waandamane hadi kuzimu lakini kipigo lazima. Mbona hakuna anayeongea kuhusu mashambulizi yanayofanywa na Hamas. Ina maana Israel wakae kibwege bila kujibu mashambulizi.

Aiseee!!!
 
Hivi haya majitu yana akili kweli..mbona hawaandamani kupinga makombora ya hamas?
 
Yaani katika watu walionishangaza ni Desmond Tutu ni kiongozi mkubwa wa Dini halafu anaongoza maandamano ya kupinga Taifa teule la Mungu, kwa kitendo alichokifanya ajiandae kwa laana itakayompata

Huyo ashalaaniwa kitambo toka alijitangaza kama mtetezi wa mashoga.

Bshaka yupo anapigania maslahi ya mashoga wenzie... we unataka wayaudi wawauwe mabasha wote ili TUTU awe mpweke kwa kuwakosa mashostito wake?
 
Yaani katika watu walionishangaza ni Desmond Tutu ni kiongozi mkubwa wa Dini halafu anaongoza maandamano ya kupinga Taifa teule la Mungu, kwa kitendo alichokifanya ajiandae kwa laana itakayompata

Usiwe kipofu......Mungu hakutuumba tuje tuuane.....

Usishabikie mauaji ya aina yoyote....
 
Hao wanao andamana wajinga sana. Afu inaonesha hawana kazi.
Andamaneni ila Israel hata wasikiliza
 
Hivi haya majitu yana akili kweli..mbona hawaandamani kupinga makombora ya hamas?

Nadhani wewe ndiyo huna akili maana hata kiongozi wa dini ya kikristo kama desmond tutu ameona umuhimu wa kuandamana.
 
Huyo ashalaaniwa kitambo toka alijitangaza kama mtetezi wa mashoga.

Bshaka yupo anapigania maslahi ya mashoga wenzie... we unataka wayaudi wawauwe mabasha wote ili TUTU awe mpweke kwa kuwakosa mashostito wake?

Ukiona umeanza kushambulia mtu baada ya kuwa objective inaonyesha kuna tatizo kwenye upeo wako.
 
Mambo yakiwa magumu utawakataa hata ndugu zako.
 
Attachments

  • uploadfromtaptalk1407741461165.jpg
    uploadfromtaptalk1407741461165.jpg
    30.2 KB · Views: 83
Wamekosa kazi hao!!!!! wanalaumu Israel kuishambulia Gaza, mbona hawailaumu Hamas kuishambulia Israel. Hivi baada ya kuweka makubaliano ya kusitisha mapigano, nani ameanza kurusha marocket? Akili za ajabu sana hizi. Kuichokoza Israel ni kujiua kwa makusudi tu (Committing suicide)
 
Hivi mashambulizi ya Gaza yalianza leo au mapigano ya Waisrael na wapalestina yameanza leo?, Mbona kipindi chote hicho watu hawakuandamana wanaandamana leo. Somalia watu wanakufa mbona hakuna nchi iliyoandamana?
 
Quite for Quite.
Israel has the right to defend itself against Hamas.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom