JOHN KITABI
Member
- Nov 10, 2007
- 26
- 3
Wana jamvi,
Wafanyakazi wa muda walokuwa wakiingiza data kwenye kituo cha data processing (Kilichopo Tanita - Kibaha) kwa ajili ya data za sensa ya watu na makazi ilofanyika Mwezi Agosti mwaka huu wamekusudia kuandamana kesho kwenda makao makuu ya ofisi ya taifa ya takwimu -NBS zilizopo kivukoni front.

Wafanyakazi hawa ambao wamekuwa wakifanya kazi hiyo tangu mwezi Septemba mwishoni hawajalipwa malipo yao kwa miezi miwili sasa pasipo sababu zinazoeleweka kutoka ofisi ya taifa ya takwimu. Aidha wanausalama ambao wamekuwa wakisimamia usalama kule kibaha kwenye data processing centre wamekuwa mstari wa mbele kuwatishia wafanyakazi hawa wasiandamane. Wanausalama hawa wakiongozwa na Suleiman Kilongo, Athuman Amiri na mwenzao Juma aka Bwana Pepsi wamekuwa mstari wa mbele kuwazuia watu kudai haki yao ya msingi.

Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dokt Albina Chuwa aliwaahidi wafanyakazi hao jumapili iliyopita kuwa angekuwa amewalipa pesa zao ndani ya siku tatu, lakini hadi leo hakuna kilichoeleweka.
Ujumbe mfupi wa simu ambao wafanyakazi hao wamekuwa wakitumiana kuanzia jana ni kwamba kesho watakusanyika kwenye ofisi ya taifa ya takwimu kujua hatima ya malipo yao.

Kumekuwa na sintofahamu kubwa kwa malipo ya wafanyakazi hao kwa kuwa haijulikani pesa za wafanyakazi hao ziliyeyukia wapi. Mradi wa sensa ni mkubwa na pesa zilikuepo zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo.
Kamishna wa Sensa Hajjat Amina Said Mrisho ambaye amekuwa bubu ghafla kwa kushindwa kutoa majibu ya malipo ya wafanyakazi hao amekuwa akiumwa kwa takriban wiki mbili sasa.