mjingamimi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 45,751
- 55,791
Wakati maandamano ya kumpongeza Rais John Magufuli kurejesha kikokotoo cha mafao cha zamani yakisubiri kupokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wakati habari hii inarushwa), huduma zimesimama kwa baadhi ya taasisi.
View attachment 988580
Wafanyakazi wameandamana leo Januari 07, 2019 kutoka eneo la Bunge hadi Uwanja wa Nyerere Square na sasa wanamsubiri Waziri Mkuu kuwapokea.
Mwananchi ilifika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kukuta shughuli za wodini na mapokezi zikiendelea lakini baadhi watendaji hawakuwepo.
Katika ofisi ya mganga mfawidhi wa mkoa hakukuwa na huduma ambapo foleni ilikuwa ndefu mlangoni lakini ikaelezwa kuwa wapo kwenye maandamano.
Ofisi za Jiji (Elimu) hakukuwa na watumishi na watu waliokwenda kwa huduma ikiwemo wazazi wenye wanafunzi waliokuwa na mahitaji wameweka foleni ndefu bila huduma.
"Wamesema viongozi wako kwenye maandamano, hatujui muda gani tutapata huduma na tunatoka mbali," amesema Job Muhumpa.
Mzazi huyo amesema maandamano hayo yangefanyika siku ambayo si ya kazi wasingeathirika kwa kiasi hicho lakini haina maana kufanya siku za kazi tena siku ambayo watoto wanatakiwa kuripoti shuleni.
Maandamano Dodoma yazorotesha huduma maofisini
Arusha zamu yao lini kupongeza kurudishwa kikorokocho cha zamani?

Arusha zamu yao lini kupongeza kurudishwa kikorokocho cha zamani?
Hapo sawa kabisa, ni methali ya kinyamwezi: kinachovunja shughuli nayo ni shughuli. Tatizo ni watumishi na serikali kwa ujumla kusahau kuwa wapo kwa ajili ya wananchi. Ndio maana kuna maneno kama vile ofisi yangu, wizara yangu, mkoa wangu nk nk. Mwananchi kupata huduma ofisini inakuwa si haki yake tena.Hayo maandamano yenyewe ni kazi
Tunawalipa mishahara (kupitia kodi zetu) ili watuhudumie. Kuandamana ni haki yao, lakini watumie muda nje ya muda wa kazi.
Ipo hakika yeyote kuwa waandamanaji wameandamana kwa hiyari yao?Hapo sawa kabisa, ni methali ya kinyamwezi: kinachovunja shughuli nayo ni shughuli. Tatizo ni watumishi na serikali kwa ujumla kusahau kuwa wapo kwa ajili ya wananchi. Ndio maana kuna maneno kama vile ofisi yangu, wizara yangu, mkoa wangu nk nk. Mwananchi kupata huduma ofisini inakuwa si haki yake tena.
Kuna waasisi wa maandamano, bila kusahau kuwa tunaelekea uchaguzi mwaka huu na kesho. Viongozi ofisini hupanga ili kujipendekeza, wanasiasa watakuwepo majukwaani kampeni za uchaguzi. Waandamanaji hawana uchaguzi, zaidi ya kufuata upepo.Ipo hakika yeyote kuwa waandamanaji wameandamana kwa hiyari yao?
Hao wanaoandamana 2023 watakuwa wamestaafu au kwa faida ya wenzao wanaostaafu sasa?Wakati maandamano ya kumpongeza Rais John Magufuli kurejesha kikokotoo cha mafao cha zamani yakisubiri kupokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wakati habari hii inarushwa), huduma zimesimama kwa baadhi ya taasisi.
View attachment 988580
Wafanyakazi wameandamana leo Januari 07, 2019 kutoka eneo la Bunge hadi Uwanja wa Nyerere Square na sasa wanamsubiri Waziri Mkuu kuwapokea.
Mwananchi ilifika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kukuta shughuli za wodini na mapokezi zikiendelea lakini baadhi watendaji hawakuwepo.
Katika ofisi ya mganga mfawidhi wa mkoa hakukuwa na huduma ambapo foleni ilikuwa ndefu mlangoni lakini ikaelezwa kuwa wapo kwenye maandamano.
Ofisi za Jiji (Elimu) hakukuwa na watumishi na watu waliokwenda kwa huduma ikiwemo wazazi wenye wanafunzi waliokuwa na mahitaji wameweka foleni ndefu bila huduma.
"Wamesema viongozi wako kwenye maandamano, hatujui muda gani tutapata huduma na tunatoka mbali," amesema Job Muhumpa.
Mzazi huyo amesema maandamano hayo yangefanyika siku ambayo si ya kazi wasingeathirika kwa kiasi hicho lakini haina maana kufanya siku za kazi tena siku ambayo watoto wanatakiwa kuripoti shuleni.
Maandamano Dodoma yazorotesha huduma maofisini
Nani kadhalilishwa?Ongezea under duress.Huu udhalilishaji wa wafanyakazi mwisho lini?