Maandamano DODOMA yazorotesha huduma maofisini

Trust None

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
1,260
Reaction score
4,421
Wakati maandamano ya kumpongeza Rais John Magufuli kurejesha kikokotoo cha mafao cha zamani yakisubiri kupokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wakati habari hii inarushwa), huduma zimesimama kwa baadhi ya taasisi.
pic+maandamano.jpg

Wafanyakazi wameandamana leo Januari 07, 2019 kutoka eneo la Bunge hadi Uwanja wa Nyerere Square na sasa wanamsubiri Waziri Mkuu kuwapokea.

Mwananchi ilifika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kukuta shughuli za wodini na mapokezi zikiendelea lakini baadhi watendaji hawakuwepo.

Katika ofisi ya mganga mfawidhi wa mkoa hakukuwa na huduma ambapo foleni ilikuwa ndefu mlangoni lakini ikaelezwa kuwa wapo kwenye maandamano.

Ofisi za Jiji (Elimu) hakukuwa na watumishi na watu waliokwenda kwa huduma ikiwemo wazazi wenye wanafunzi waliokuwa na mahitaji wameweka foleni ndefu bila huduma.

"Wamesema viongozi wako kwenye maandamano, hatujui muda gani tutapata huduma na tunatoka mbali," amesema Job Muhumpa.

Mzazi huyo amesema maandamano hayo yangefanyika siku ambayo si ya kazi wasingeathirika kwa kiasi hicho lakini haina maana kufanya siku za kazi tena siku ambayo watoto wanatakiwa kuripoti shuleni.

Maandamano Dodoma yazorotesha huduma maofisini
 
Unaandamana wakati ni haki yako na ilizuiliwa na unaempongeza
 
Wakati maandamano ya kumpongeza Rais John Magufuli kurejesha kikokotoo cha mafao cha zamani yakisubiri kupokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wakati habari hii inarushwa), huduma zimesimama kwa baadhi ya taasisi.
View attachment 988580
Wafanyakazi wameandamana leo Januari 07, 2019 kutoka eneo la Bunge hadi Uwanja wa Nyerere Square na sasa wanamsubiri Waziri Mkuu kuwapokea.

Mwananchi ilifika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kukuta shughuli za wodini na mapokezi zikiendelea lakini baadhi watendaji hawakuwepo.
Katika ofisi ya mganga mfawidhi wa mkoa hakukuwa na huduma ambapo foleni ilikuwa ndefu mlangoni lakini ikaelezwa kuwa wapo kwenye maandamano.

Ofisi za Jiji (Elimu) hakukuwa na watumishi na watu waliokwenda kwa huduma ikiwemo wazazi wenye wanafunzi waliokuwa na mahitaji wameweka foleni ndefu bila huduma.
"Wamesema viongozi wako kwenye maandamano, hatujui muda gani tutapata huduma na tunatoka mbali," amesema Job Muhumpa.

Mzazi huyo amesema maandamano hayo yangefanyika siku ambayo si ya kazi wasingeathirika kwa kiasi hicho lakini haina maana kufanya siku za kazi tena siku ambayo watoto wanatakiwa kuripoti shuleni.

Maandamano Dodoma yazorotesha huduma maofisini
keshokutwa JPM atapiga marufuku maandamano, halafu hawa hawa wataandama kupongeza maandamano kupigwa marufuku.

kweli CCM kumejaa misukule!
 
Arusha zamu yao lini kupongeza kurudishwa kikorokocho cha zamani?
 
hakika... hawa kuswagwa waka andamane... kila MTU kwa hiari yake ameungana na wenzie kiandamana....

safi.. na wachache wame baki maofisini wala akuna anaye wagombeza kwa kubaki maofisini
 
Ngoja kwanza, inamaana wameandamana na kufika eneo la tukio kisha wakaanza kumsubiria anayetakiwa kuwapokea?
 
Back
Top Bottom