Kama wewe sio mtanzania mnafiki, bali unapenda nchi yetu iwe na maendeleo ya dhati, basi utakubaliana na mimi kuwa huyu raia wa kigeni anastahili kuungwa mkono kwa kufanya maandamano. Hakuna kilichofichika, na wala huhitaji kuwa na Phd ili kujua kuwa utawala wa nchi yetu ni mbovu, na nchi yetu inazidi kudidimia kila kunapokucha. Viongozi wa Mamlaka nyingi wanaendesha mambo kiholela, na kwa kujali maslahi binafsi, na si kwa manufaa ya nchi na wananchi wake.
Mambo mengi maovu yanayotokea kwa sasa wengi tumekuwa tukiyasikia yakitokea katika nchi zingine, lakini hatukuwahi kudhani yangeweza kutokea ndani ya kisiwa cha amani, namaanisha Tanzania.
Kibaya zaidi ni kwamba sisi watanzania hatuna uthubutu wa kuongea ukweli. Nahisi tamaduni zetu za kusema Baba akikosea jambo hupaswi kumkosoa. Hili ndio kosa kubwa alilofanya ''Huyu raia wa kigeni'' Amethubutu kusema ukweli. Sasa wahusika wanakasirika kwasababu hawajazoea kusemwa. Si utamaduni wao kusemwa.
Tusipokubali kuwakosoa watendaji wanaohujumu mali za umma, wasiowajibika, na wasiojali maendeleo ya nchi yetu, basi hali itazidi kuwa tete zaidi ya ilivyo kwa sasa. Tuache unafiki, tuwe wakweli, tuandike, tuwaseme bila kukata tamaa.
Lakini kwa upande mwingine mtu unajiuliza:
1. Shinikizo la kumshambulia huyu Raia wa kigeni linatoka wapi?
2. Kwanini watanzania hatuandamani kwa mambo kama EPA, Tanesco, Richmond, wabunge kupandishwa mishahara, matokeo mabovu ya form 4, na mengine mengi ambayo orodha yake ni ndefu; ili kushinikiza wahusika waachie ngazi, na tupate watendaji bora?
Nawasilisha.
Published on 3 Mar 2013Taasisi ya Human settlement of Tanzania-HUSETA- imewataka wananchi kujitokeza katika maandamano yatakayoanzia viwanja vya Mnazi mmoja hadi ubalozi wa Uingereza kuwasilisha azimio la kuitaka serikali ya Uingereza kutoa tamko hadharani la kutohusika na maovu yanayofanywa na baadhi ya raia wa nchi hiyo dhidi ya taifa la Tanzania ikiwemo kashfa na udhalilishaji kwa viongozi wa Ngazi za juu wa serikali.
Wito watolewa kuandamana kupinga kashfa kwa viongozi...
source: ITV TANZANIA youtube
N.B
Naona taasisi hii ya HUSETA imekosa kazi za muhimu kutetea mambo muhimu yanayowakera wananchi kama kama kukosa hati miliki za makazi yao, viwanja vyao n.k ili kama kutatokea neema madini, gesi kugunduliwa ktk maeneo wananchi wanayoyamiliki kwa hati waweze kupata kifuta jasho kinachostahili na siyo kufukuzwa toka maeneo yao kwa kisingizio ardhi ni mali ya serikali.

Huyo Dagan Kimbwereza atakuwa kibaraka wa magogoni au ana unanasaba na kiongozi dhaifu.