Mjomba wa taifa
JF-Expert Member
- Apr 20, 2012
- 231
- 161
Naangalia picha ya zamani iitwayo Escape From Sobibor, naona mtu asie askari kasimama juu anapuliza kipenga ishara ya kuwaita mateka wote katika ngome ya kufanyishwa kazi chini ya utawala wa kijerumani. Vuguvugu limepamba moto, mateka wanatoroka kwa kukata Senyenge zenye miba mikali. Risasi zinalia kuzuia vuguvugu.
Jambo la kushangaza naona kuna baadhi ya mateka wamesimama tu hawajishughulishi kutoroka Sobibor. Ninapata dhana kuwa either hawana mbio kushindana na askari ama wamependezwa na maisha ya pale kwa kuwa wanyapara.
Ghafla nashtuka kumbe nilikuwa ndotoni, nafunua pazia nje naona bendera za M4C na maandamano makubwa ya watanzania wakiimba "tumechoka kudhulumiwa haki zetu leo ndio mwisho wa dhuluma." Wengine wanaimba "Dhahabu, Almasi, Tanzanite, Uranium, Gesi, Mbuga za Wanyama, Bahari, Maziwa, Mito, Ardhi yenye rutuba, milima lakini bado watoto wetu wanakufa kwa malaria, kipindupindu hakuna pesa za kuwatibu, wanafunzi wanasoma darasani hakuna madawati, madaftari yamweunganishwa kwa nyuzi za viatu"
Kundi la tatu linapita likipaza sauti zaidi ya makundi yaliyopita, "watoto wa viongozi ajira zao BOT, NSSF, PSPF, Bandari, TRA, Ikulu, Bungeni, Ofisi za Kibalozi, Hazina, baba kigogo wa nchi, mtoto mwakilishi fisadi, mama mjumbe fisadi, shemeji mnene RIJESI RA PORISI, uncle Waziri wa madarasa, Dada Katibu Mkuu, maswahiba wamekamata tender zote, utawala kurithishana hali ya kuwa watoto wa masikini waende VETA kujifunza kushika misumeno, kuchimba mitaro, umachinga, ukarani"
Nasikia sauti kwa mbali inakuja inaimba kwa nguvu "rushwa barabarani, hospitalini, tender serikalini .. vijana wote tokeni nje tupiganie nchi yetu"
Duh! Maneno makali yamenigusa uzalendo umenishinda nakimbia nje nikiwa na kaptura yangu kifua wazi. Mara nasikia kichwani sauti ya marehemu babu yangu inasema "mjukuu wangu beba galoni ya maji, vaa suruari na shati la mikono mirefu, huko uendako kuna mabomu na maji ya kuwasha".
Napita kumwamsha rafiki yangu KINENE katika chumba chake alichopanga ambaye tulimaliza nae chuo kikuu Mlimani miaka 4 iliyopita ambaye anafanya kibarua kama Volunteer kugawa vipeperushi vya kampuni moja mpya ya Simu. Namwambia Twende kwenye maandamano ya kujikomboa, ananyanyuka toka kwenye jamvi alilolalia, anafunua pazia la Khanga iliyoshonwashonwa kwa kuchakaa ananijibu "wewe huogopi mabomu mimi siendi huko naenda kugawa vipeperushi"
Shiiiiit, Graduate anagawa vipeperushi barabarani??? 4 years mtaani!!!!!!???
Nakumbuka tena picha niliyoiona ndotoni ya Escape from Sobibor, bado kulikuwa na mateka waliogoma kutoroka, duh!