Maandamano CHADEMA na Escape from Sobibor

Maandamano CHADEMA na Escape from Sobibor

Hii habari yako inanikumbusha yaliyotokea KENYA, watu waliandamana kudai haki ya matokeo ya uchaguzi mkuu baada ya kibaki kujitangaza kuwa raisi, watu wengi sana walikufa , majerui walikuwa wengi na wengine nyumba zao zilichomwa hadi leo wako kwenye maema hawakujengewa nyumba. Wale waliokuwa wanahamasisha maandamano walikaa chini na kugawana madaraka na kuwasahau wale waandamanaji. DUNIANI hamna haki, haki mbinguni, hutakuja kufa au kuumia alafu wenzako wakapatana baadae wakagawana vyeo. Akiri kumkichwa.
Babu zako na bibi zako wangekuwa wabinafsi kama wewe usingeikuta hii nchi unayojivunia wewe kungu.ru.
 
Hakika hiyo ndiyo taswira yetu kama wana was nchi tena itatugharimu iwapo tutakuwa kama mateka waliosimama bila kujishughulisha kutoroka katika #Sobibor
 
Watatumia kila njia lakini hawatashindana na nguvu ya umma.

Waanze kukimbia nchi.
 
Hii habari yako inanikumbusha yaliyotokea KENYA, watu waliandamana kudai haki ya matokeo ya uchaguzi mkuu baada ya kibaki kujitangaza kuwa raisi, watu wengi sana walikufa , majerui walikuwa wengi na wengine nyumba zao zilichomwa hadi leo wako kwenye maema hawakujengewa nyumba. Wale waliokuwa wanahamasisha maandamano walikaa chini na kugawana madaraka na kuwasahau wale waandamanaji. DUNIANI hamna haki, haki mbinguni, hutakuja kufa au kuumia alafu wenzako wakapatana baadae wakagawana vyeo. Akiri kumkichwa.

Mkuu yote ni sawa tu tofauti ni kwamba hayo ya mabomu na virungu yanaonekana kwa uwazi lakini kuna mabomu ya umasikini, magonjwa, ukosefu wa huduma muhimu za kijamii, njaa na kuondolewa kwenye makazi kwa kisingizio cha kuwapa ardhi wawekezaji nk nk. Haya yote ndugu mwandishi uliyemjibu ameyaeleza ki falsafa mno na ni kweli tupu.
 
Mzee Uchwara hapa hakuna cha maana sanana inafutwa tu kiki ya kisiasa ukizingatia 2015 sio mbali watu wapigwe waumiee baadae wakuu watoe matamko na baada ya wiki utawasikia wako ikulu wakitafuta maridhiano na Mr President halafu wahanga wa maandano wanaendelea kuteseka hospital bila hata msaada wa chama mbya zaidi hutasikia Mtoto au ndugu wa Mbowe au Slaa kaumizwa kwenye maandamano.

Hii pia umenikumbusha kwenye ile kesi ya Lema Arusha Lema kakataa kuwekewa dhamana eti anataka awaonyeshe watawala kwamba haogopi jela!! hazijapita hata siku mbili eti watu wanaambiwa waandamane kushinikiza Lema apewe dhamana kha!!! yaani mtu kaenda kwa hiari yake halafu aanze kusumbua watu kuandamana kisa kachoka kukaa Lupango halafu watu wanakubali kuandamana?? kweli waji..nga hawataisha dunia hii

Ndugu wa Mbowe na Dr Slaa ni wanachama wote, wapenzi wote na wote wanaowaunga mkono katika harakati za kuikomboa hii nchi kutoka kwa mkoloni,jitu jeusi tiii linaloitwa CCM na serikali yake dhalimu!!.

Hata Yesu Kristo alisema, ndugu na mama zake ni wale wote wanaotii na kuheshimu maagizo ya Mungu wala si wale walio mzaa na wale waliozaliwa naye tumbo moja!!

Amka wewe,twende acha umbumbu na intimidations zako!!
 
hiyo ni kati ya sinema chache zilizonipa ujasiri huu nilionao leo .
 
Naangalia picha ya zamani iitwayo Escape From Sobibor, naona mtu asie askari kasimama juu anapuliza kipenga ishara ya kuwaita mateka wote katika ngome ya kufanyishwa kazi chini ya utawala wa kijerumani. Vuguvugu limepamba moto, mateka wanatoroka kwa kukata Senyenge zenye miba mikali. Risasi zinalia kuzuia vuguvugu.

Jambo la kushangaza naona kuna baadhi ya mateka wamesimama tu hawajishughulishi kutoroka Sobibor. Ninapata dhana kuwa either hawana mbio kushindana na askari ama wamependezwa na maisha ya pale kwa kuwa wanyapara.

Ghafla nashtuka kumbe nilikuwa ndotoni, nafunua pazia nje naona bendera za M4C na maandamano makubwa ya watanzania wakiimba "tumechoka kudhulumiwa haki zetu leo ndio mwisho wa dhuluma." Wengine wanaimba "Dhahabu, Almasi, Tanzanite, Uranium, Gesi, Mbuga za Wanyama, Bahari, Maziwa, Mito, Ardhi yenye rutuba, milima lakini bado watoto wetu wanakufa kwa malaria, kipindupindu hakuna pesa za kuwatibu, wanafunzi wanasoma darasani hakuna madawati, madaftari yamweunganishwa kwa nyuzi za viatu"

Kundi la tatu linapita likipaza sauti zaidi ya makundi yaliyopita, "watoto wa viongozi ajira zao BOT, NSSF, PSPF, Bandari, TRA, Ikulu, Bungeni, Ofisi za Kibalozi, Hazina, baba kigogo wa nchi, mtoto mwakilishi fisadi, mama mjumbe fisadi, shemeji mnene RIJESI RA PORISI, uncle Waziri wa madarasa, Dada Katibu Mkuu, maswahiba wamekamata tender zote, utawala kurithishana hali ya kuwa watoto wa masikini waende VETA kujifunza kushika misumeno, kuchimba mitaro, umachinga, ukarani"

Nasikia sauti kwa mbali inakuja inaimba kwa nguvu "rushwa barabarani, hospitalini, tender serikalini .. vijana wote tokeni nje tupiganie nchi yetu"

Duh! Maneno makali yamenigusa uzalendo umenishinda nakimbia nje nikiwa na kaptura yangu kifua wazi. Mara nasikia kichwani sauti ya marehemu babu yangu inasema "mjukuu wangu beba galoni ya maji, vaa suruari na shati la mikono mirefu, huko uendako kuna mabomu na maji ya kuwasha".

Napita kumwamsha rafiki yangu KINENE katika chumba chake alichopanga ambaye tulimaliza nae chuo kikuu Mlimani miaka 4 iliyopita ambaye anafanya kibarua kama Volunteer kugawa vipeperushi vya kampuni moja mpya ya Simu. Namwambia Twende kwenye maandamano ya kujikomboa, ananyanyuka toka kwenye jamvi alilolalia, anafunua pazia la Khanga iliyoshonwashonwa kwa kuchakaa ananijibu "wewe huogopi mabomu mimi siendi huko naenda kugawa vipeperushi"

Shiiiiit, Graduate anagawa vipeperushi barabarani??? 4 years mtaani!!!!!!???

Nakumbuka tena picha niliyoiona ndotoni ya Escape from Sobibor, bado kulikuwa na mateka waliogoma kutoroka, duh!
Hii nimeipenda mkuu!! nakumbuka vile vile wale manokoa wa wajerumani kule Sorbibor walivyoshughulikiwa kabla ya kuwavaa wajerumani na askari wake!! Vivyo hivyo makuwadi wa mafisadi na wasaliti liwe ndio target yetu kabla ya kupambana na CCM!!
 
Hii nimeipenda mkuu!! nakumbuka vile vile wale manokoa wa wajerumani kule Sorbibor walivyoshughulikiwa kabla ya kuwavaa wajerumani na askari wake!! Vivyo hivyo makuwadi wa mafisadi na wasaliti liwe ndio target yetu kabla ya kupambana na CCM!!

nimeipenda sana hii mkuu !
 
Back
Top Bottom